Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Du aloo hii sio mchezoVifo vyao vilipangwa ndomana vilifanana.
2pac gari yao ilipofika kwenye traffic light mataa ya kuruhusu upande wao kwenda yakafunga hivyo ikawalazimu kusimama. Ghafla wakatokea mabinti pembeni ya barabara wakaanza kuita 2pac.. 2pac.. 2pac... basi 2pac ile kushusha kioo awapungie mkono hapo hapo akaanza kushambuliwa na gari ya majamaa waliokuwa ubavuni kwao.
Big nae gari yao ilipofika kwenye traffic light mataa ya kuruhusu upande wao kwenda yakafunga hivyo ikawalazimu kusimama. Ghafla pia wakatokea mabinti pembeni ya barabara wakaanza kuita Big.. Big.. Big.. basi ile Big kushusha kioo awapungie mkono hapo hapo na yeye akaanza kushambuliwa na gari iliyokuwa pembeni yao hadi kusababisha umauti wake.
Picha ya kwanza ni ya gari aliyoshambuliwa nayo 2pac.
Na picha zingine ni za gari aliyoshambuliwa nayo Big. Na chini kabisa ni madem waliomwita Big kabla ya shambulizi ili afungue dirisha. Na alipofungua tu akashambuliwa.
Shambulio la 2pac lilifanyikia Nevada katika jimbo la Texas.
Kweli mkuu hapo niliteleza kweli. Nakushukuru sana kwa kunisahihisha kiungwana.Hapa umeteleza, aliuawa Las Vegas ambayo iko jimbo la Nevada sio Texas, Nevada ni jimbo na Texas ni jimbo pia..ambayo yako kwenye different geographical areas.
Mpaka sasa hujaleta ushahidi wowote kuhusu nadharia zako. Unaleta stori za vijiweni tu.Mimi sina tatizo na ulichoandika maana sio wewe peke yako unaejiona unaijua vizuri ishu ya vifo vya 2pac na Big. Kuna watu wengi humu wanaojifanya wanaijua vyema ishu hii na mimi nimekuwa nikisoma tu na kuendelea na mjadala bila kuwapinga au kuwaonesha kuwa hawajui. Hii ni kwa sababu nafahamu katika mambo kama haya kila mtu ana aina yake ya upokeaji wa taarifa. Na haimaanishi kwamba kila taarifa zinazopokelewa ni za kweli.
Zipo za uongo kutoka kwa watu wa karibu na wahusika na zipo za kweli kutoka kwa watu wa mbali vile vile.
Kuwa mjomba au kaka wa 2pac, Big au Orlando haimaanishi kwamba mtu huyo kila atachoongea kuhusu muhusika ni cha kweli. Hii ni dunia ya kupigania tonge. Kwahiyo kuna mungine anaweza kutumia mazingira ya vifo hivyo kujipatia tonge.
Wewe unashangaa eti mjomba wake Orlando hawezi kumsingizia mpwa wake. Je wewe haujawahi kusikia mjomba anamfanyia ushenzi mpwa wake kwa sababu ya masilahi fulani.
Wewe unajua ni kiasi gani alichopata ili kuja kueleza ukweli au kupotosha taarifa za Orlando ilimradi mkono uingie kinywani? Je haujui kama toka miaka hiyo watu wengi walikuwa wanaishi kwa kiki mbali mbali zikiwemo hizi za kujifanya wanajua habari za kina 2pac na Big?
Sasa mimi sina tatizo na hilo, tatizo langu ni kujifanya kuniambia kuwa mimi napotosha ilihali kuwa hata na wewe haukuwa eneo la tukio, haukuwahi kuishi nao wote wawili na haukupata hata nafasi ya kuongea nae wewe mwenyewe mmoja wa wahusika wa Big, 2pac au Orlando.
Umeokoteza okoteza taarifa mbali mbali za kweli na uongo ukazileta humu na watu tuliona kama zipo kinyume na zile tunazofahamu na kuzielewa sisi ila tukaheshimu kile ulichoamini.
Sasa iweje na wewe usiheshimu kile walichoandika wenzako. Una mamlaka gani ya kukimbilia kumkosoa mwenzako kuwa kakosea ili hali hata wewe mwenyewe umesoma na kufuatilia hizi taarifa kupitia mitandaoni tu kama mimi na wachangiaji wengine!
Hiyo picha ya BMW haionyeshi sehemu ambayo Tupac aliuawa. Baada ya shambulio Suge Knight alipiga U turn na kupanda ukingo wa barabara na kurudi walikotoka. Kwa kupanda ukingo gari likapata pancha na wakashindwa kuendelea. Hapo ni mahali ambapo gari lilikwama, sio mahali lilipofanyika shambulio. Ungekuwa unajua hii ishu usingeposti kwamba hiyo picha ni sehemu ambayo Pac alishambuliwa.Ndo ilivyokuwa mkuu, hapa nakuwekea picha ya kwenye mashambulio yao uone mazingira ya shambulio yanavyofanana.
Juu ni gari aliyokuwa amepanda 2pac
Na hizo zingine za chini ni gari aliyokuwa amepanda Big. Mashambulizi yote yalifanyika kwenye trafiki light.
Na chini picha ya wale madem waliomwita Big. Ambapo alipofungua dirisha tu akakumbana na risasi za kichwa kutoka kwenye gari iliyopaki ubavuni kwa gari yao. Hii ilikuwa hivyo hivyo kwa Pac pia.
Basi tufupishe wewe kwa kuamini unachoamini na mimi niamini ninachoamini. Simple like that.Mpaka sasa hujaleta ushahidi wowote kuhusu nadharia zako. Unaleta stori za vijiweni tu.
-Orlando alikuwepo MGM Grand, Las Vegas usiku wa September 7.
-Orlando alishambuliwa na Tupac pamoja na entourage ya Deathrow usiku huo (motive).
-Mshikaji wake wa karibu anayeitwa BG Knoccout ameshaongea kwenye mahojiano mbali mbali kama Vladtv na Art of the Dialogue podcast na akasema wazi kwamba Orlando baada ya kurudi Compton alikuwa ana-brag kwamba ndiye shooter.
-Kwenye documentary ya Murder Rap, Keefe D, mbele ya lawyer alisimulia kisa chote cha usiku wa September 7 na kukiri kwamba Orlando alikuwa shooter.
Ni kweli nimeokoteza taarifa kama ulivyosema lakini wewe hata hint hauna. Unaleta hekaya tu bila facts zozote.
Kwani Huwaoni Mkuu.....!?Kwanini umewaza hivi mkuu 😂😂
Anyway kwa kufupisha tu wewe baki na matango pori yako uliyolishwa. Hakuna hata neno moja la maana uliloandika.Hiyo picha ya BMW haionyeshi sehemu ambayo Tupac aliuawa. Baada ya shambulio Suge Knight alipiga U turn na kupanda ukingo wa barabara na kurudi walikotoka. Kwa kupanda ukingo gari likapata pancha na wakashindwa kuendelea. Hapo ni mahali ambapo gari lilikwama, sio mahali lilipofanyika shambulio. Ungekuwa unajua hii ishu usingeposti kwamba hiyo picha ni sehemu ambayo Pac alishambuliwa.
Uongo mwingine ni kusema eti Tupac alipigwa risasi baada mademu kumuita na akafungua dirisha. Dirisha la upande wa Tupac lilikuwa wazi muda wote wa Safari yao ya kutoka hoteli ya The Luxor walikofikia kwenda Club ya 662. Nina uhakika hujui lolote kuhusu hilo. Mademu walimuita baada ya kumuona Tupac kwa sababu dirisha la upande wake lilikuwa wazi. Ushahidi ni hii iconic picture ya Tupac dakika kadhaa kabla Cadillac nyeupe haijafika pembeni yao na shambulio kutokea.View attachment 2566951
Tuko pamoja mkuu.Kweli mkuu hapo niliteleza kweli. Nakushukuru sana kwa kunisahihisha kiungwana.
Tofauti na wengine ambao wanaokoteza makosa madogo madogo kama haya na kuamua kuyafanya ajenda ya kupingana na ukweli nilioandika.
Huyo jamaa story zake ni zile conspiracy theories. It is well known shooter ni Orlando au mtu aliekuwa nao kwenye ile gari usiku ule kama tukiamua kutokumuanini Keefe D. 2Pac kafa sababu ya gang stuff, hakuna cha FBI wala nani. Ni ujinga ulimcost. Biggie kafa kama collateral.Mpaka sasa hujaleta ushahidi wowote kuhusu nadharia zako. Unaleta stori za vijiweni tu.
-Orlando alikuwepo MGM Grand, Las Vegas usiku wa September 7.
-Orlando alishambuliwa na Tupac pamoja na entourage ya Deathrow usiku huo (motive).
-Mshikaji wake wa karibu anayeitwa BG Knoccout ameshaongea kwenye mahojiano mbali mbali kama Vladtv na Art of the Dialogue podcast na akasema wazi kwamba Orlando baada ya kurudi Compton alikuwa ana-brag kwamba ndiye shooter.
-Kwenye documentary ya Murder Rap, Keefe D, mbele ya lawyer alisimulia kisa chote cha usiku wa September 7 na kukiri kwamba Orlando alikuwa shooter.
Ni kweli nimeokoteza taarifa kama ulivyosema lakini wewe hata hint hauna. Unaleta hekaya tu bila facts zozote.
Poa poa, nimechanganya ma_fileHapana movie yao inatwa Poetic Justice.
Naona umekuja na ID nyingine ya ku quotes ile comment yako ya juu.Huyo jamaa story zake ni zile conspiracy theories. It is well known shooter ni Orlando au mtu aliekuwa nao kwenye ile gari usiku ule kama tukiamua kutokumuanini Keefe D. 2Pac kafa sababu ya gang stuff, hakuna cha FBI wala nani. Ni ujinga ulimcost. Biggie kafa kama collateral.
Usitudondoshe ukaishia kusepa ,unafatiliwa ujueKWANINI TUPAC ALIMCHUKIA SANA BIGGIE MPAKA KIFO ? (4)
_______________
Inaendelea......
Kutokana na Tupac kuhitaji bosi wa Death Row, Marion 'Suge' Knight apambane kumtoa ndani ili waweze kufanya biashara pamoja, Suge aliangaika huku na huko mpaka kufanikiwa kumchomoa Tupac jela.
Kiasi cha Dola Milioni 1.4 kilitolewa na Suge hivyo kufanikiwa kumtoa jela Tupac mwaka 1995, achilia mbali Dola 15,000 ambazo Suge alizitoa kumsaidia 'kishkaji' Tupac wakati akiwa jela.
Kimsingi Suge alikubali kujipukutisha fedha kwa sababu alijua kumwandika Tupac mkataba wa kumsimamia kupitia Death Row Records italipa. Knight alijua nini anafanya kwenye makubaliano hayo.
Makubaliano ya Tupac na Suge yakawa mazuri. Tupac akakubali kutengeneza albamu 3 chini ya Death Row Records lakini muda wote akihitaji Suge awe upande wake kwenye vita vyake dhidi ya Biggie.
Nyimbo ya kwanza ya Tupac kuitoa chini ya Death Row Records ikawa California Love. Kombinesheni ya Tupac, Dr Dre na Roger Troutman kwenye chorus ukawa unyama wa kufa mtu. Kwa hakika "The King was back from Jail''.
Ujio wa California love ulimtikisa kila mtu. Tupac alikuwa amejerea kuusimika upya ufalme wake uliotishiwa kuondoshwa kwa mtutu wa bunduki na vijana kutoka Pwani ya Mashariki (East Coast).
Marion Suge Knight na Tupac Shakur wakafanikiwa 'kuupika' mgogoro wa East Coast na West Coast ukapikika, mgogoro ambao chimbuko lake haswa ni chuki baina ya wasanii wawili, Notorious Big na Tupac Shakur.
Matatizo binafsi ya Biggie na Tupac yakajikuta yakirithiwa na hata wengine 'yasiyowahusu'. Wasanii wa East na West wakaonekana kuchukiana katika kiwango kilichotisha kabisa.
Wakati mgogoro huu ukikua na kuzidisha uhasama kwa wasanii, Serikali mwanzo ilionekana kama kupuuza, lakini kadiri hali ilivyozidi kuwa mbaya na viongozi walilazimika kusema chochote.
Lakini kabla ya kusema chochote, huko nyuma Tupac alikuwa ameshaingia kwenye mgogoro mara kadhaa na serikali kutokana na misimamo yake, harakati zake na maisha yake.
Nyimbo zake kupitia albamu yake ya 2Pacalypse ziliichefua sana serikali. Tupac alizungumzia zaidi Siasa, Ubaguzi na umasikini katika namna ambayo ilionekana kama kuchochea chuki kwa raia.
Mshtuko mkubwa ulitokea baada ya kijana mmoja mdogo kumpiga risasi polisi na kumuua kisha baada ya kukamatwa na kuhojiwa akathibitisha kufanya hivyo baada ya kusikiliza albamu ya Tupac iitwayo 2Pacalypse.
Tukio hilo lilikuwa gumzo nchini Marekani. Aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo, Bw Dan Quayle akatangaza kupigwa marufuku kwa nyimbo za Tupac kusikilizwa kwenye Jamii ya wamarekani.
Bw. Quayle alisema Tupac ni msanii asiyefaa kabisa kusikilizwa. Nyimbo zake zimejaa chuki na kuchochea uovu kwenye jamii. Akaanzisha kampeni za kuhakikisha jamii inamchukia na haipati nafasi ya kumsikiliza Tupac.
Masikini Quayle hakuwa amejua kuwa wakati anasema hayo, Tupac alikuwa ameshaiteka sehemu kubwa ya jamii ya wamarekani kuliko anavyodhani. Mahojiano yake na MTV ya mwaka 1993 yamlitosha kabisa kumfanya asimjibu lolote.
"Siwezi kuitawala dunia wala siwezi kuubadilisha ulimwengu, bali nichoweza kufanya ni kutema cheche zitakazofanya bongo za watu kuibadilisha dunia"..hii ndiyo kazi yetu tunayopaswa kufanya, kuamsha mtu mwingine anayetutazama".
Tupac alikiambia kituo cha televisheni cha MTV mwaka 1993 katika moja kati ya mahojiano yake yanayoendelea kukumbukwa mpaka leo. Quayle alishindwa vibaya katika kampeni ya kumaliza Tupac, lakini inaelezwa alichangia mno kupromoti mauzo ya kazi zake bila ya yeye kujua.
Watu mashuhuri mbalimbali waliyataja maneno hayo machache ya Tupac kama maneno bora zaidi kuwahi kutolewa na mtu "asiyetegemewa" na wengi kusema hivyo. Wengi waliyatumia kama rejea kwenye maeneo yao mbalimbali.
"Inawezekana baadhi yetu tusiwe watu wa kuibadilisha dunia, lakini tunapaswa kujaribu kila wakati kushawishi mtu mwingine kuchukua hatua zitakazoweza kuibadili dunia".
Maneno haya ya Tupac hata kwangu binafsi bado yanaishi sana.!
Itaendelea........[emoji3578]
#Balozi
Lete vitu kikubwa hapa ni 2pac wanaokupinga Hawa ni akina au wadau wa B.I.G.....[emoji23][emoji23][emoji23]