Tetesi: P Diddy ahusishwa na kifo cha Notorious B.I.G

Boss hapa ungekuwaa muungwana kama ungeongeleaaa kile kibao cha Pac na N.W.A cha "https://jamii.app/JFUserGuide the Police"
 
Boss lile Song https://jamii.app/JFUserGuide the Police lililetaa Uhasama mkubwaa Mno kati ya Serikali na Wahuni wa Compton
 
Natamani naninyi mlete stori habari za B.I.G ingependeza
Ukute hata habari za Big mwenyewe hawazijui, yan mpaka waende kuokota mawili matatu kwenye vijiwe vya kahawa ndo waje kujaribu kutulisha matango pori kwa habari sijui za kusimuliwa na mjomba wake muuwaji wa Big 😂😂😂😂
 
Ndio maana nikasema kwamba assumptions zako ni za kijinga. Eti kwa kuwa Tupac alizaliwa na Afeni Shakur basi tayari Serikali inamchukulia kuwa ni rebel. Halafu hayo maneno aliyosema Pac mpaka Serikali ikatetemeka ni yapi? Mbona hamuyaweki hapa?

Mnataka kumuweka Tupac kwenye level moja na MLK, Malcolm X na Fred Hamptons. Kamwe hakuwa kwenye level hiyo.

George Floyd alikuwa victim wa Police brutality. Sijui hata anahusiana kivipi na huu mjadala. Dude, you are all over the place, hata hujui unataka kuongea nini.
 
Umeshamezeshwa uongo na mjomba wake Orlando, so ni vigumu sana mtu kukuelewesha hadi ukaelewa tunachojadili.
 
KWANINI TUPAC ALIMCHUKIA SANA BIGGIE MPAKA KIFO.? (5)
_______________

Inaendelea......

Pamoja na Tupac kuishi maisha yaliyoonekana kuwachukiza baadhi ya watu kutokana na kuwa na vitendo vya ukorofi uliopitiliza lakini alipendwa mno.

Ilistaajabisha watu. Kwanini mtu anayehubiriwa kuwa mbaya mbele ya jamii, jamii husika ilimpenda mno.? Maisha yake bado yanagusa hisia za wengi hata sasa.

Ukiachana na uhuni uliopitiliza, Tupac alipendwa mno na mademu. Historia inaonesha aliwahi kuwa na uhusiano na mademu wengi walioonekana kujigonga wenyewe kwake.

Katika orodha hiyo, mastaa kadhaa wa muziki hawakukosekana. Lady Madonna anafungua orodha hii kwa kuwahi kuwa na uhusiano na Tupac kwa muda wa miezi 18.

Uhusiano na Madonna na Tupac uliripotiwa sana lakini wawili hao wakamwagana kwa Tupac kuhisi kuwa taswira yake ya 'ki-gangsta' inapotezwa kwa kuwa na mahusiano na mzungu.

Staa mwingine aliyeudandia mtumbwi wa vibwengo wa Tupac alikuwa ni Whitney Houston. Wengi walishangaa kusikia mume wa Whitney, Bobby Brown akilithibitisha jambo hilo pasina shaka.

Katika Documentary ya kumbukumbu zake iitwayo "Every Little Step", Bobby anaelezea kuwa alifahamu uhusiano wa Tupac na Whitney lakini alipuuza kwa sababu hayo yalifanyika huko nyuma.

Mastaa wengine waliokuwa na mahusiano na Tupac kwa vipindi tofauti tofauti ni pamoja na Aaliyah, Yo-Yo, Faith Evans, Rosie, Jada Pinkett, Janet Jackson, Kidada Jones nk.

Hili la Jada na Janet limekuwa na ukakasi kipindi chote kutokana na wao wenyewe kukanusha vikali, japo watu waliokuwa karibu na Tupac huwezi kuwaambia hivyo wakakuelewa.

Hata kama Janet na Jada hawakuwahi 'kuliwa' na Tupac, hiyo haiondoi kuwa walimpenda mno muhuni huyo. Tupac alipendwa sana na wasichana, naye aliwapenda mno.

Maisha ya Tupac yalijaa visa na mikasa mingi. Hii ni kwa sababu dunia haipendi kuambiwa ukweli. Tupac aliishi maisha ya kuelezea hisia zake bila mipaka, jambo hili lilimgharimu.

Alivutiwa mno na maisha ya Uhuni na Ujambazi (Thug Life) na kuamua kujifaharisha kwa hilo. Tattoo yake maarufu aliyoichora tumboni kwake ya "Thug Life" ilizusha maswali mara kadhaa kwa waandishi aliyoamua kuyajibu 'kiaina'.

"Naona wengi mnahoji sana kuhusu "Thug Life". Mimi na 'wanangu' Syke Stretch, Mopreme Shakur, The Rated R, Macadoshis na Kato tumeanzisha kundi la Hip Hop lenye jina hilo".

"T.H.U.G. L.I.F.E. ni kifupi cha "The-Hate-U-Give-Little-Infants-Fucks-Every". Na hiki kama kundi ndicho tunachomaanisha" alieleza Tupac. Kundi hili pia lilitoa albamu moja iliyoitwa "Thug Life".

Mbali ya kurap, Tupac alijaaliwa kipaji kikubwa cha Uigizaji. Drama ya kihalifu ya "Juice" aliyeigiza mwaka 1992 kama Roland Bishop, kijana mwenye shida mtaani anayegeuka na kuwa muuaji ilimpa umaarufu mkubwa.

Miaka miwili baadae akaigiza filamu ya "Above The Rim" kabla ya kuigiza kwenye "Poetic Justice" sambamba na Bibie Janet Jackson. Filamu hizi zinadhihirisha kipaji alichojaaliwa Tupac katika sanaa ya muziki na Uigizaji.

Itaendelea........[emoji3578]

#Balozi
 
Umeandika nini hiki?
 
Ukisoma huu Uzi watu wanatoa detail utafikiri walikuwa wana hang na 2pac huko Marekani.

Kumbe ni washamba fulani wapo hapo Yombo hata ndege hawajawahi kupanda.
 
Diddy mjasiriamali sana.

So story ya kuondoka kwenye label baada ya mkataba ni the same na PAC na Suge/deathrow.
 
He (
Hamna lolote brother. Huyo mama anataka hela tuu hana lolote.

Puffy juzi kat8 hapa ameamua kuwamilikisha "master recording" wasanii wake wote including BIG mother ambae ni mrithi wa BIG na amekubali hilo deal kwa makubaliano toka Bad Boy records.

Pia Suge hana lolote he's in jail serving 23 years with possible parole in 2034. Na Death Row records ameshainunua Snoop akijua kwamba ubabe na umafia wa Suge uliisha mahakamani.
 
2pac aliwaibia sana ma nigger wa pandee zileee. Ila ki ukweli jamaa alikuwa miyeyushoo sana kama angekuwa kipindi Kuna social network asingeweza kuwashika masikio kiasi kilee.. Pac kengee sana

Yaan matatizo anatafuta mwenyewe alafu ananza kulaum watu wengine shida zikimkuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…