Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
Rapa na mfanyabiashara wa muziki wa Marekani, Sean “Diddy” Combs, ameongezewa matumaini ya kutoka gerezani mapema baada ya tarehe yake ya kuachiwa kusogezwa mbele kwa mara nyingine.
Kwa mujibu wa taarifa mpya kutoka Bureau of Prisons, Diddy ambaye anahudumu kifungo katika Federal Correctional Institution (FCI) Fort Dix, New Jersey, sasa anatarajiwa kuachiwa Februari 5, 2028. Tarehe hiyo imepunguzwa kwa siku 15 kutoka tarehe ya awali ya Februari 20, 2028.
Diddy alihukumiwa kifungo cha miezi 50, sawa na miaka minne na miezi miwili, baada ya kupatikana na hatia mwaka 2025 kwa makosa mawili ya kusafirisha watu kuvuka mipaka ya majimbo kwa ajili ya ukahaba. Hata hivyo, aliachiliwa huru na jury katika mashtaka mazito zaidi ya sex trafficking na racketeering conspiracy.
Tarehe yake ya kuachiwa imekuwa ikibadilika mara kadhaa. Awali ilitarajiwa kuwa Juni 2028, kabla ya kusogezwa hadi Aprili, Februari, kisha Januari 2028. Baada ya tukio la ugomvi na mfungwa mwenzake katika gereza la Fort Dix, tarehe hiyo ilibadilishwa tena hadi Februari 20, kabla ya kupunguzwa hadi Februari 5, 2028.
Kwa sasa, Februari 5, 2028 ndiyo tarehe mpya inayoripotiwa kuwa ya kuachiwa kwake, ingawa tarehe za wafungwa zinaweza kubadilika kutokana na mikopo ya muda, mwenendo gerezani au taratibu nyingine za kifungo.