Natokea Kanda Maalum
JF-Expert Member
- Dec 22, 2016
- 749
- 1,310
Gashinaga ule ong'wise? Ofumile Ntuzu? Hale bariadi?Ah wapi.
Mimi nina uwezo wa kuongea na kuandika lugha moja kwa ufasaha wa hali ya juu kabisa bila kuchanganya na lugha ingine.
Kama ni kimombo basi naweza kukiandika na kukiongea mwanzo mwisho.
Kiswahili nacho vivyo hivyo. Ikija kwenye Kisukuma ndo usiseme kabisa. Hiki ndicho huwa najivunia zaidi kukijua. Kwangu ni fahari ya aina yake ingawa zamani niliwahi kuchekwa na kudhihakiwa kuwa eti naongea 'kilugha'. Dokezo hapo ni kwamba ukiongea 'kilugha' basi wewe ni mshamba.
Kwa hiyo kwangu mimi ni tofauti kabisa. Huwezi kuniweka kwenye hilo kundi.
Halafu unajua nini? Watu huwa wanastaajabu na kubaki midomo wazi wanapogundua kuwa naweza kuongea Kisukuma tena kile cha Ntuzu kabisa bila hata kwakwaru.
Mimi ni namba ingine kabisa.