Nimejaribu kuusoma uzi mpaka hapa nilipofikia. Mimi ni mdau mkubwa sana wa Mashairi ila si mdau wa muziki wa aina yoyote ile.
Nasimama katika fani adhimu,fani ya ushairi kama ambavyo baadhi ya wasanii wanavyojinasibisha.
Kupitia uzi huu nilicho kiona ni kuwa wengi ni wapenzi wa sanaa ya kucheza na maneno ila si wapenzi wa ukweli na maana halisi. Tungo nyingi zilizo wekwa humu kama marejeo ya wahusika wa tungo hizo hazina ukweli wala maana bali zina sanaa ya kucheza na maneno na utovu wa adabu.
Natamani sana pangekuwepo watu wenye maarifa maana wa kuchambua tungo hizo. Mifano iko mingi sana.
Hii tungo ina maana na ina uhalisia.
Kadhalika tungo hii ina maana nusu nusu.
Tungo hii ina uongo na mtunzi anaonyesha hakuwa anajua nini anachokiandika.
Hapa tutamuuliza mtunzi kwa msingi gani chakula ni uchafu ? Kuna ndiyo kigezo cha kufanya chakula kiwe kichafu ?
Hii ni ada ya kimaumbile wala hakuna uhusiano kati ya kulia na ubaya wa dunia,sababu tutakuuliza amejuaje hili ?
Swali la msingi ni kwanini hizi tungo za Wasanii wanaziita mashairi ? Je ni kwa mazoea au ?