P MAWENGE: Nahamia weusi

P MAWENGE: Nahamia weusi

WEUSI ndio kundi bora la hiphop Tanzania. Hawa wengine ni takataka tu zimejikusanya na kujiita kundi la hip hop
Mziki wa weusi umekaa ki-commercial yani zile flavour za underground huzipati, afu hata kwenye hiyo hiyo commercial walau wangekua na content ya kueleweka
 
P mawenge , sema jamaa anajuwa kudiss mbaya , kila nikikumbuka hii verse

"Na wewe mwenye virasta kaa msyuka"
"Nitavikusanya nivikate hata nachupa "

Huwa nabaki nacheka tuuu kwa kweli.
Na ile ya marapa mizigo

Tushavurugwa sitaki branda branda nao, nawachapa makofi tu madogo na mabrother zao.../

Mawenge sio mtu wakutaka taka madharau, namuogopa mungu sio vipaka paka na manyau.../
 
Wanabebana sana mpaka inafika hatua wanaimba visivyo na maana
Afande sele naye aliwachana the same

Pia kuna presenter simkumbuki jina naye alikutwa na tuhuma hizo za kuwa-favour weusi kwasababu ya ukanda
 
Afande sele naye aliwachana the same

Pia kuna presenter simkumbuki jina naye alikutwa na tuhuma hizo za kuwa-favour weusi kwasababu ya ukanda
Presenter wa radio flani ilikua na matamasha makubwa Tz,. Na jamaa flani muda mwingine hujiweka rapper
 
Nilikuwa mweupe nikaokota book nikabukuka.

Na maji ni ya shingo yanawapalia madingi kooni.
nilikua mtupu nikaokota buku nikabukuka, leo nasimulia tungo tukufu ni kama rufufu kafufuka.../

Legend kama koffi olomide, naikamata dar daudi wa kolomije.../

Nawalaza dolo si follow bata nafollow mishe, na ufundi ni controversial utasema appolo mission../
 
Presenter wa radio flani ilikua na matamasha makubwa Tz,. Na jamaa flani muda mwingine hujiweka rapper
Huyo presenter ndiye aliyemponda nikki mbishi kwa kuvaa bazee kwenye video ya fanya wewe
 
Mkuu Unamjua Cado kitengo? Mteganda? Toxic?

Kuna maunderground wanamitindo huru hatari.

Kuna battle niki mbishi alijichanganya kwa Cado kitengo kwenye Wasafi muulize kilichomkuta.
Hahahaha ni big sunday, nikki alijiharibia sana
 
Kesho ntakuwekea hapa clip zake tena nyingine akiwa na cado, utofauti wa frege ni kwamba hafanyi battle za ku attack mpinzani, mara nyingi yeye anafanya zile freestyle kutokana na mazingira yaliyomzunguka

Ila ni hatari sana
Cado na frege
 
Mkuu huyu frege ndio nani maana ndio mara ya kwanza leo namsikia anavideo zozote za freestyle youtube nikamcheck coz Kitengo na toxic hawa huwa nawafuatilia
Papaa frege na cado
 
Nimejaribu kuusoma uzi mpaka hapa nilipofikia. Mimi ni mdau mkubwa sana wa Mashairi ila si mdau wa muziki wa aina yoyote ile.

Nasimama katika fani adhimu,fani ya ushairi kama ambavyo baadhi ya wasanii wanavyojinasibisha.

Kupitia uzi huu nilicho kiona ni kuwa wengi ni wapenzi wa sanaa ya kucheza na maneno ila si wapenzi wa ukweli na maana halisi. Tungo nyingi zilizo wekwa humu kama marejeo ya wahusika wa tungo hizo hazina ukweli wala maana bali zina sanaa ya kucheza na maneno na utovu wa adabu.

Natamani sana pangekuwepo watu wenye maarifa maana wa kuchambua tungo hizo. Mifano iko mingi sana.
Ebu fikiria tu kidogo nikki alipoimba
Alisema nchi ya viwanda, njoo uone nchi ya vibanda
Hii tungo ina maana na ina uhalisia.
Dizasta: Utakapochukua wasaa utagundua ulimpa saa alipohitaji muda wako
Kadhalika tungo hii ina maana nusu nusu.
Songa: Hata chakula ni uchafu na ndio maana una nawa baada ya kula
Tungo hii ina uongo na mtunzi anaonyesha hakuwa anajua nini anachokiandika.

Hapa tutamuuliza mtunzi kwa msingi gani chakula ni uchafu ? Kuna ndiyo kigezo cha kufanya chakula kiwe kichafu ?
Songa: Duniani ni kubaya na ndio maana ukizaliwa tu unalia
Hii ni ada ya kimaumbile wala hakuna uhusiano kati ya kulia na ubaya wa dunia,sababu tutakuuliza amejuaje hili ?

Swali la msingi ni kwanini hizi tungo za Wasanii wanaziita mashairi ? Je ni kwa mazoea au ?
 
Nimejaribu kuusoma uzi mpaka hapa nilipofikia. Mimi ni mdau mkubwa sana wa Mashairi ila si mdau wa muziki wa aina yoyote ile.

Nasimama katika fani adhimu,fani ya ushairi kama ambavyo baadhi ya wasanii wanavyojinasibisha.

Kupitia uzi huu nilicho kiona ni kuwa wengi ni wapenzi wa sanaa ya kucheza na maneno ila si wapenzi wa ukweli na maana halisi. Tungo nyingi zilizo wekwa humu kama marejeo ya wahusika wa tungo hizo hazina ukweli wala maana bali zina sanaa ya kucheza na maneno na utovu wa adabu.

Natamani sana pangekuwepo watu wenye maarifa maana wa kuchambua tungo hizo. Mifano iko mingi sana.

Hii tungo ina maana na ina uhalisia.

Kadhalika tungo hii ina maana nusu nusu.

Tungo hii ina uongo na mtunzi anaonyesha hakuwa anajua nini anachokiandika.

Hapa tutamuuliza mtunzi kwa msingi gani chakula ni uchafu ? Kuna ndiyo kigezo cha kufanya chakula kiwe kichafu ?

Hii ni ada ya kimaumbile wala hakuna uhusiano kati ya kulia na ubaya wa dunia,sababu tutakuuliza amejuaje hili ?

Swali la msingi ni kwanini hizi tungo za Wasanii wanaziita mashairi ? Je ni kwa mazoea au ?
Imenibidi nicheke kwanza
 
Back
Top Bottom