Pablo atimuliwa Simba SC, mwenyewe agoma kupokea barua

Pablo atimuliwa Simba SC, mwenyewe agoma kupokea barua

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
VIKAO vya siku mbili ndani ya Simba vimeamua rasmi kuachana na kocha mkuu Pablo Franco kwa kile kilichodaiwa ni kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo.

Simba imepoteza mataji yake yote mawili la Ligi Kuu Bara ambalo walilitwaa kwa mara nne mfululizo pamoja na taji la Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) walilobeba mara mbili mfululizo.

Habari za kikao hicho zilinaswa na Mwanaspoti kwamba wamefikia makubaliano hayo na tayari Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alimwandikia barua ya kuvunja mkataba kocha huyo aliyomtumia jana jioni.

Pablo amekiri kupokea barua hiyo na kwamba alimrudishia bosi wake kwani kuna vitu ndani ya barua hiyo vilikuwa havijakaa sawa hivyo anachosubiri sasa ni Barbara kufanya marekebisho hayo ili asaini.

"Ni kweli tulikuwa na kikao na mabosi wangu na kuna mambo sikukubaliana nayo hususani upande wa usajili, jioni CEO alinitumia barua ya kuvunja mkataba lakini ilikuwa na upungufu hivyo sikusaini nilimrudishia ili arekebishe.

"Sikupanga kuondoka Simba kwani tayari nilikuwa nimeikatia Visa familia yangu ya kuishi hapa kwa mwaka mmoja, hivyo nasubiri akirekebisha hiyo barua na kuyaweka yale niliyoyapendekeza ambayo ni maslahi basi nitasaini kuvunja mkataba," amesema Pablo ambaye aliingia Simba Novemba mwaka jana.

Credit, MwanaSpoti

Updates,
FB_IMG_16539938161713719.jpg
 
Kuna mtu mwaka juzi nilimwambia "Simba itatisha misimu 4, unaofata (msimu wa 5) itayumba sana. Lakini msimu utakaofata (msimu ujao) itakuwa tishio kubwa"

Sehemu 1 ya utabiri wangu umeshatimia, tusubiri msimu ujao tuone. Na bado naamini msimu ujao simba itakuwa bora sana kushinda ilivyokuwa msimu jana.

Huyo jamaa niliemwambia hayo yupo dar m/nyamala anauza duka la reja reja
 
VIKAO vya siku mbili ndani ya Simba vimeamua rasmi kuachana na kocha mkuu Pablo Franco kwa kile kilichodaiwa ni kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo...
Hivi kwa kikosi alichokikuta Pablo mlitegemea maajabu gani?
 
Kuna mtu mwaka juzi nilimwambia "Simba itatisha misimu 4, unaofata (msimu wa 5) itayumba sana. Lakini msimu utakaofata (msimu ujao) itakuwa tishio kubwa"

Sehemu 1 ya utabiri wangu umeshatimia, tusubiri msimu ujao tuone. Na bado naamini msimu ujao simba itakuwa bora sana kushinda ilivyokuwa msimu jana.

Huyo jamaa niliemwambia hayo yupo dar m/nyamala anauza duka la reja reja
Simba ni bora Yanga kukiwa na mgogoro tu Yanga ikitulia ni hatari kama Masai nayo Simba hukimbilia porini!
 
nabi kuanzia Sudan simba walimtaka ila alikuwa hajamaliza mkataba wake ,ile anamaliza simba wameshamchukua Gomes ,ndo maana Nabi alipofika Dar anahojiwa nawaandishi anasema Simba is the best club ,akaanza kukumbushwa upo Yanga. Hata hizi holidays alizokuwa anaenda wanasema anakwepa kurenew kwa sababu kuna ishu ya chini chini na Simba.
 
VIKAO vya siku mbili ndani ya Simba vimeamua rasmi kuachana na kocha mkuu Pablo Franco kwa kile kilichodaiwa ni kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo...

Kuendelea Kubaki Na Matola ni Kosa Kuubwa sana…
Ni Mmojawapo anaegawa Wachezaji!
Ukiacha Fitna,Ana Mbinu gani Kisoka?
Kama walivyokuwa kina Patrick phiri,Nk
Cc: GENTAMYCINE
 
FUFKUPCWUAEd6mA.jpg


Klabu ya Simba imetangaza kuvunja mkataba na Kocha Mkuu, Pablo Franco Martin pamoja na Kocha wa Viungo, Daniel De Castro Reyes baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Baada ya maamuzi hayo, Timu ya Simba ambayo haijawa na msimu mzuri itakuwa chini ya Kocha Msaidizi, Selemani Matola.
 
Duh, Soka la bongo hamna story za build up.

Kocha kakuta tim ina mazee kibao, Hamna kocha ataeza toboa na simba kwa striker za bocco, mugalu na kagere.

Sema aende tu hana maajabu.

Kwani msimu jana tulitoboaje? Hawakuwepo??
 
Kama kawaida yetu wabongo wanaanza kuvaa viatu, then ndio wanavaa soksi.

Watamwondoa Pablo, then watawaondoa wachezaji na usajili wa wachezaji utasimamiwa na viongozi, baada ya kumaliza kusajili ndipo watakapo msajili kocha mwengine na kumpa malengo ya timu,kupitia wachezaji walio wasajili wao viongozi na kesho watamlaumu kwa matokeo mabovu kipitia wachezaji walio wasajilo wao.
 
Back
Top Bottom