Unatofautisha vipi uvaaji wa hereni wa Marekani (haswa kwa watu weusi) na uvaaji wa hereni wa Afrika? Kwa maana hawa wote wametokea katika mzizi mmoja! Na kama kulikuwa na tamaduni za baadhi ya makabila kuvaa hereni, kwanini isiwe kwamba hao wamarekani walibeba hizo tabia na kwenda nazo utumwani? Na kwa kuwa mitindo siyo static, ina evolve, hizo hereni wanazovaa sasa ni matokeo ya tamaduni za uvaaji wa hereni wa kitambo.
Ebu weka ushahidi unachokisema. Kama ingekuwa hivyo unavyodai, basi wavaaji hereni wangekuwa hata hawapati ajira Marekani. Unauliza iweje huku Afrika tuwaone watu wa kawaida, wapi wanaonekana siyo watu wa kawaida? Je, unawashangaa pia wamaasai kusuka nywele na kuvaa nusu uchi? Pengine utasema ni utamaduni wao! Na ukiona mzungu kavaa kama maasai utakuwa wa kwanza kumsifia!
Ukweli huo nani kaudefine? Maana masuala ya tamaduni ni rahisi sana kuwa na prejudice. Na suala la kupata heshima popote (unamaanisha dunia?) linadhiirisha jinsi ulivyo ndani ya box. Hapo Kenya tu, jaji mkuu wao anavaa hereni! Sasa sijui kuwa jaji mkuu siyo heshima? Maadili machafu unayaona kwa wavaaji hereni tu? Hivi wateja wa hao mashoga nao ni wavaaji hereni? Braza, mbona unafikiri kama mtoto wangu wa miaka 3?!?
Eti silka kama yangu! Mimi siyo mvaaji wa hereni, lakini kutokana na nilichokieleza juu ya chanzo cha utamaduni wa kuvaa hereni, sioni shida wala aibu kulisemea hili suala.