PostGE2025 Padre Kitima: Sisi tunamiliki Hospitali, waliletwa majeruhi, wakasema wasitibiwe tunataka kuwaona Mochwari

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Mwamba amejitoa.. hoogopi kifo tena.
Wacha tushuhudie.
Na ninafikiri atakuwa amesikia harassment wanazopata watumishi wa afya (nurses and doctors) kutoka kwa watawala baada ya documentary ya CNN. Hasa wa vituo na hospitali za serikali.

Kuliko kuendelea kuumiza raia, watu wenye hekima na busara wamshauri ikibidi alazimishwe kuachia ngazi kwa maslahi ya taifa
 
Mkuu with all respect, Naamini hii order imekuwa approved tu may be Bila general Concern what might happen after, Kama umekuwa kwenye leadership najua utanielewa let the CinC punish those who advised her, Kwasababu any attempt to remove her it will bring more Chaos the best options nadhani Kwa sasa ni wale waliokuwa kwenye nafasi ya kumshauri na wanajulikana publicly wawe removed kwenye nafasi zao
Mkuu, vyovyote tutakavyo jaribu kumlinda CinC ila The buck stops with her.

Sawa anaweza kuwa ali approve bila thoroughly consideration, hiyo iakuwa moja ya grave mistake ever executed by CinC hasa hasa inapohusu UHAI wa raia.
 
Huyu mama hana hata chembe ya huruma wala aibu!

Daah!

Tungeruhusiwa kununua na kumiliki Silaha kwenye maduka ya silaha... kama south-africa huu usenge ungeisha! TUNGEHESHIMIANA!
 
1.Ni nani aliagiza watu wapigwe risasi na kuuawa vile?

Unaposema watanzania ni wapi hao ? Sababu huu ujinga mnao utetea sio Watanzania wote wapo kama nyinyi. Ili ujibiwe swali hili, ainisha hili, na kadhalika ili swali lako lilete maana.

2.Wapigaji risasi wale ni wakina nani na wapo wapi?
Ukiwajua ndio itabadilisha nini na ili iweje ?
 
Kutokana na swali lako, unamaanisha hakuna mtu aliyeuawa kiasi kwamba hospitali hawawezi kuonyesha hata maiti moja? Let's be serious. Hata kama una fikra mbadala swali lako halionyeshi nia ya kujadili hoja. Linaashiria kupinga kwa madhumuni ya kupinga tu.
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Padri Charles Kitima, amesema kuwa wakati wa maandamano kuliletwa majeruhi waliokuwa wameumia, lakini baadhi ya askari walizuia wapewe matibabu wakidai “tunataka kuwaona mochwari.”

Ameeleza kuwa, kwa kuwa Kanisa Katoliki linamiliki hospitali mbalimbali, wamekuwa mashahidi wa kile kilichotokea, ikiwemo kupokea miili ya watu waliopoteza maisha kutokana na kupigwa risasi za moto.
Yaani kauli kama hIzi zipo wazi alafu huyo mama enu analeta kiburi?!
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Padri Charles Kitima, amesema kuwa wakati wa maandamano kuliletwa majeruhi waliokuwa wameumia, lakini baadhi ya askari walizuia wapewe matibabu wakidai “tunataka kuwaona mochwari.”

Ameeleza kuwa, kwa kuwa Kanisa Katoliki linamiliki hospitali mbalimbali, wamekuwa mashahidi wa kile kilichotokea, ikiwemo kupokea miili ya watu waliopoteza maisha kutokana na kupigwa risasi za moto.
Huu ni uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu, tunaona siku zote hata kwa wale wanaopigana iwe Israel vs Hamas, wanaojeruhiwa wanatibiwa hospitali, Russia na Ukraine, adui wanaoumizwa wanatibiwa hospital kama Vienna convention inavyotaka, jamani huyu shetani anaua bila huruma, watu wengi wameuawa tangu wakati wa Kikwete-Magufuli-Samia, Huyu mama ameua watu wengi bila huruma. Kwa damu nyingi zilizomwagika kutoka kwa Mdude Nyagali au Polepole, kwa jinsi wanavyofanya sidhani kama hao wawili ni wazima....Sidhani. Samia alivyokuja juu kwenye hotuba yake alivyosema "eti tuwaachie fulani na fulani" inathibitisha kuwa Polepole hayupo humu duniani kwa maagizo ya Samia.
Ninaona aibu nchi yangu, rais ana uwezo mdogo sana wa kufikiri, hivi kwenye hotuba yake, anarusha rusha mikono juu na kushika kiuno......Sijui rais wa wapi ana tabia kama hizi?
Eti wazazi mlikuwa wapi kuwazuia watoto wenu......Kwa hiyo nchi hii adhabu iliyobakia kufanya lolote lile ni kuuawa??? Kweli hata huruma hana, wameandamana wanadai jambo la msingi....UCHAGUZI SIYO WA HAKI, WAGOMBEA WANAOMPINGA WAMEONDOLEWA, na WATANZANIA HASA WATANGANYIKA WAACHWE KUTEKWA. Badala yake watu wanakutana na risasi za moto.....Kweli hata huruma hana, watu wameuawa kwenye nyumba zao mbele ya familia zao, vijana wadogo wamebakwa na kulawitiwa mbele ya familia zao, wamepigwa risasi za vichwa, wamenyofolewa wakiwa wodini na kupelekwa mortuary.
Yeye haoni hilo, hii tume aliyounda ya akina IBRAHIM JUMA na STERGOMENA TAX kila mtu anajua majibu yake, inapoteza tu pesa za watanzania, hakuna kitu pale.
Huyu mama sasa tumeona rangi yake ni ipi........Mtesaji, muuaji, mbakaji na asiye na utu hata kidogo. Hao wazee wa Dar Es Salaam ni wanufaika wa mradi wa TASAF, wao kazi yao ni kupiga makofi tu......Hawana utu hata kidogo bali kushibisha matumbo yao.

Huyu Samia ni wa ovyo sana kwa nchi yetu.....Muonevu na muuaji wa watoto wetu.
 
Japo siwapendi kwelikweli polisi wa kibongo
Lakini Kuja na press na kulituhumu jeshi la polisi hadharani, bila kuwa na ushahidi wa unayotuhumu maana hapo sio tena fulani kasema bali itakuwa ataje:
Hospitali gani?
Watumishi gani wa hospitali wameripoti hivyo?
Na ni polisi gani kwa majina yao waliwapa amri ya kutotibu majeruhi au kupeleka majeruhi mochwari ?

Muda si mrefu tutasikia polisi, wanafungua jalada la uchunguzi kwa aliyosema Kitima, na yeye kujumuishwa katika huo uchunguzi atolee maelezo yake ufafanuzi na ushahidi.
Isije ikawa mimi niliambiwa, maana katika huo ushahidi ambao unaweza kuwa wa kweli kabisa lakini atawaingiza na madaktari na manesi matatani kumtolea huo ushahidi.
 
Itakua vizuri sana wakimhoji na kufungua hiyo kesi
Pili, kwa nini serikali haifungii kanisa katoliki kama walivyofungia kanisa la gwajima? Gwajima hakuzungumza magumu kama haya ya kitima, kwa ninu serikali haifungii katoliki? Hofu? Uoga?
 
Mkuu with all respect, Naamini hii order imekuwa approved tu may be Bila general Concern what might happen after, Kama umekuwa kwenye leadership najua utanielewa let the CinC punish those who advised her, Kwasababu any attempt to remove her it will bring more Chaos the best options nadhani Kwa sasa ni wale waliokuwa kwenye nafasi ya kumshauri na wanajulikana publicly wawe removed kwenye nafasi zao
Mkuu leo umemsikia mwenyewe, bado unaamini hiki ulichoandika jana?
 
Itakua vizuri sana wakimhoji na kufungua hiyo kesi
Pili, kwa nini serikali haifungii kanisa katoliki kama walivyofungia kanisa la gwajima? Gwajima hakuzungumza magumu kama haya ya kitima, kwa ninu serikali haifungii katoliki? Hofu? Uoga?
Kwa gwajima, na lile valangati la Bashite, na kumtukana Pengo, kama Jiwe asingekuwa msukuma mwenzake angesha funga kanisa lake zamani tu
Kwa gwajima pale hakuna kanisa wala dhehebu, ulikuwa ni upigaji, maji yalivyomfika shingoni akaanza kujifanya na yeye ni mkatoliki, lakini haikusaidia.
Kwani kakobe yuko wapi na alifanywa nini na Jiwe, ndio ujue kuna taasisi za dini na kuna makanisa ya upigaji, huyo mwamposa akijichanggaya siku moja aongee utumbo, ndio utakuwa mwisho wake.
Nadhani utakuwa unamjua Sheikh Ponda na pilika zake na serikali na mpaka kupigwa risasi, na kulikuwa na Sheikh Kassimu bin Juma pale Kariakoo mpaka serikali iliufunga msikiti wa Mtoro kwa muda.
Kanisa katoliki ni taasisi ya kidini, na Kitima sio kanisa katoliki, yeye ni kitima kama kitima.Kama serikali ikitaka kudeal nae yeye kama yeye haishindwi, na muda sio mrefu ataitwa kujieleza kirefu kwa aliyoyasema, watch this space
 
Mkuu gwajima alimtukana pengo wakati wa kikwete na si wakati wa magu.
Wakati wa magu si gwajima tu hata mwingira wa efatha nae alikorofishana na serikali ya magu, nae kwa nini hakufungiwa? Alikua msukuma?

Kakobe kanisa lake FGBF haliawahi kufungiwa

Kuhusu kitima, yeye ni sehemu ndogo tu ya TEC. Waraka huwa ni wa TEC ambapo kuna raisi wake. TEC ndio hutoa hizo waraka zote unazozisikia, je TEC haiwakilishi katoliki? Kama inawakilisha, kwa nn hamuifungii?
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Padri Charles Kitima, amesema kuwa wakati wa maandamano kuliletwa majeruhi waliokuwa wameumia, lakini baadhi ya askari walizuia wapewe matibabu wakidai “tunataka kuwaona mochwari.”

Ameeleza kuwa, kwa kuwa Kanisa Katoliki linamiliki hospitali mbalimbali, wamekuwa mashahidi wa kile kilichotokea, ikiwemo kupokea miili ya watu waliopoteza maisha kutokana na kupigwa risasi za moto.
Kwa hiyo yeye anataka watu wafe ili afurahi? Huyu mama ana roho ya kishetani sio bure! Basi wangempelekea maiti akaange nyama ale ashibe. Shetani mkubwa!
 
Masheikh lazima wajibu, sababu hawataki ujinga na uchochezi unao fanywa na Hawa viongozi wa Kikatoliki.

Tena safari hii, wamepotea njia.
Mashehe ubwabwa wakiona tu sinia la wali maharage basi. Pelekeni watoto shule
 
Back
Top Bottom