Padre Kitima: Suala la kuminywa haki za Wamasai wa Ngorongoro si sahihi

Padre Kitima: Suala la kuminywa haki za Wamasai wa Ngorongoro si sahihi

Ni kweli lakini unawakumbuka wale maaskofu 20 wa kule kwa Tshikedi? Walizungumza, Kabila hakuchukua round!

Sisi wengi tulidhani nguvu yao iko hivyo hata huku kwetu....kumbuka jeshi ni loyal tayari, sasa kwa upuuzi unaoendelea, nani mwingine wa kuokoa jahazi?
Kuna muda wakristo wa tz wanaaminishana eti kanisa liko juu ya serikali
 
Nyie juzi mmeua msanii Mandojo kanisani kwenu mkiwa na majoho, biblia, mikate na wine, mbona hamjatoa kauli?
Watoe kauli ipi ikiwa mapadri wanauawa hukohuko kanisani na hakuna kesi hadi leo?
 
TEC washakuwa maaachawa wa mama. Katibu TEC anasema haoni umuhimu wa katiba mpya. Sababu zake eti hata kama katiba mpya itapatikana haitasaidia chochote kama utashi hakuna.

Kaongea utumbo sana huyu katibu wa TEC.
Hivi hajui kuwa katiba bora huwa na mifumo bora ya kujilinda? Katiba bora inaimarisha uhuru wa mihimili 3 na hivyo kufanya kazi ya check and balance ipasavyo. Katiba bora haichezewi hovyo.
Sexless neno Utashi au Conscience ne kitu kikubwa sana, na ndiyo kinatenganisha binadamu na mnyama. Why people behave the way they behave. Mpe mbwa constitution, CCM ni kama wanyama hawana utashi. Hata tukija na katiba gani kama ni CCM mambo yatakuwa vile vile
 
TEC hawana jipya, walikula za uso siku ya kusaini mkatsba na DP World, bado inawauma ile.

Umesahau?

Muunguja majibu yake ni vitendo tu.
Hate shetani ana vitendo pia ndio maana ulimwengu una wema na uovu
 
NI MBAYA MNO TAASISI ZA KIDINI KUJIUNGA NA WANASIASA NI MBAYA SANA SANA SANA, TEC HAITAMBUI HAKI ZA WANYAMA JUU YA MBUNGA KUZIDIWA NA IDADI YA BINADAMU NA HATIMAYE KUSABABISHA WANYAMA KUHAMA, AU KUSABABISHA KUJIFICHA MBALI, HIVYO WAGENI KUPATA TABU SANA KUWAONA WANYAMA, HUSIKA, WAMASAI HUKO MBUGANI WANAPASWA KUWEPO KAMA STRANGERS, KWA IDADI FULANI, NA SIO KUGEUZA MBUGA ZETU VIJIJI NA MAJIJI, KWANI HATIMAYE WANYAMA WETU WATAKWENDA WAPI?, WAKENYA HUTAMANI SANA MBUGA ZETU ZIFE, KWANINI WAKENYA, MASAI MBUGANI KWAO NI KAMA STRANGERS TU.
 
Kanisa sio chama cha siasa.

Hii kazi ya kuiwajibisha serikali tufanye sisi wananchi sio makanisa wala misikiti kazi zao sio harakati za siasa.

Ni mbaya dini zikitawala siasa za nchi.
Huelewi maana ya dini na siasa, ujinga huu ndio mtaji mkubwa wa watawala
 
Kwamba waalitakiwa kufanya nini? Kuna falsafa inasema hivi: "An army of sheep led by a lion is better than an army of lions led by a sheep. This undescore the importance of subjects to support strong leaders who choose to take risk to lead them. Kama hawataungwa mkono kwa sababu mbali mbali hawapaswi kulaumiwa hata kidogo. Tatizo linakuja kwamba mara nyingi hoja yenye mashiko ambayo inafaa kuungwa mkono na watu wengi au watu wote kwa maslahi ya wengi hudandiwa na wanapropaganda kwa kuhamisha mjadala kuanza kujadili watu kwa misingi mbali mbali ikiwemo histora, itikadi, dini hali ya maisha n.k.!! Na katika hili Chama Tawala kimefanikisha kwa kiasi kikubwa, Kasome kitu kinachoitwa adhominem fallacy. Kesho utakuta watu wanajadili "Maaskofu wanamkosoa Rais Kwakua ni mwislamu" Kesho utaskia "Kwa sababu ni Mzanzibari' Badala ya mjadala kujikita katika hali halisi ya Maasai Cummunity and challenges mjadala utahama na ajenda kushahulika!!! uswalaumu they are playing their part to the marked limit that they cant cross or go bryond. iwapi nafasi yako na wewe?
You nailed it 🙌🙏🙏
 
Kanisa sio chama cha siasa.

Hii kazi ya kuiwajibisha serikali tufanye sisi wananchi sio makanisa wala misikiti kazi zao sio harakati za siasa.

Ni mbaya dini zikitawala siasa za nchi.
Kabisa unataka kuongelea haya mambo akagombee ubunge au mwakilishi halali wa watu kwa sasa hana mamlaka ya kumsemea yoyote wabaki na mambo ya dini tu, sio unavaa joho la kidini kujilinda huku unafanya uharakati wa kisiasa.
 
Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoriki Tanzania Daktari wa Falsafa na Padre ndugu Kitima amesema si haki na ni udhalilishaji wa wazi wanafanyiwa Wamasai wa NGORONGORO kwa kunyimwa haki zao.

"....leo hii tunapozungumza ndugu zetu Wamasai wa kule NGORONGORO wanatuma ujumbe mbaya wenye twasira hasi Kimataifa. Unapowaeleza ni hiari yao kubaki NGORONGORO halafu ukiwanyima haki zao za msingi huo ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu! Jiulize kwa walichokifanya leo huko Duniani waelevu wanatufikiriaje!?" Amehoji Kiongozi huyo mtendaji wa TEC.

Chanzo: Jambo TV

Pia soma:Kuelekea 2025 - Wamasai Ngorongoro wamechoka kunyang’anywa ardhi yao na kupewa Mwarabu, Wameamua liwalo na liwe
Ukweli serikali hii ni ovu haswa inafanya mambo ya ajabu sn
 
Mimi haya mambo siyataki kabisa nayafahamu madhara yake.

Imani ni kitu kibaya tena Afrika kwa waafrika elimu na matumizi ya akili yapo chini ni hatari.

Wao wabaki makanisani na misikitini kazi ya kuiwajibisha serikali tuachiwe sisi wananchi kama wanataka kuungana nasi wavue kanzu na majoho waje kama wananchi wa kawaida sio viongozi wala taasisi fulani ya kidini.

Dini ikae mbali kabisa na siasa za nchi kuna madhara makubwa ikisogezwa ni rahisi kuleta mpasuko wa hatari.

..labda ungesisitiza CCM ikae mbali na madhehebu ya Dini ili wasije wakaleta mtafaruku na madhara unayoyazungumzia.

..kama kuna chama kimeonyesha nia uovu ya kuwafuatafuata Watanzania mpaka kwenye nyumba zao za ibada basi ni CCM.
 
Sexless neno Utashi au Conscience ne kitu kikubwa sana, na ndiyo kinatenganisha binadamu na mnyama. Why people behave the way they behave. Mpe mbwa constitution, CCM ni kama wanyama hawana utashi. Hata tukija na katiba gani kama ni CCM mambo yatakuwa vile vile

..kuna manufaa zaidi, kuwa na Katiba nzuri hata kama hakuna utashi wa kuitekeleza, kuliko kuwa na katiba mbovu, huku watawala wakiisigina.
 
Kwani haiongelewi bandari ya Ngorongoro hapa?
Siku moja utaehuka; hupo mbali sana na hatua hiyo baada ya kuwa mlevi wa siku nyingi.
Hiyo 'anthropology' ndiyo iliyo kudidimiza kabisa, halafu utamlaumu Nyerere juu ya hilo pia!
 
Back
Top Bottom