The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Anasema kusema vijana wamenunuliwa ni makosa na kuwakosea sana. Anasema vijana si wajinga kiasi hicho.
Ingawa, anaona kusema wamehamasishwa hilo halina mjadala kwani kulikuwa na uhamasishaji kabla ya Uchaguzi.
"Kusema vijana wamenunuliwa ili kuandamana si sahihi, wamehamasishwaje hiyo ni agenda nyingine kwa sababu huwezi kukataa kwamba wamehamasishwa, kuandmana tarehe 29 maana yake kuna mtu amehamasisha. Wamehamasishwaje kuingia barabarani mikoa zaidi ya mitano
Kumetokea mauaji ya watu, mamia hatuongelei watu wameuawa wawili watatu, mauaji makubwa kiasi hiki useme mtu amehongwa aandae maandamano, vijana si wajinga kiasi hicho. Hizo hela zinazotajwa ziligawanywa kwa mtindo upi kwa vijana wote wale waliokuwa wameandamana?

"Tusikatae ukweli kwamba vijana waliandamana kwa sababu gani? wanasema sababu ya kwanza ukiuliza vijana wanasema hatuko salama watu wanatekwa, watu wanapotezwa, watu wanauawa, ni zoezi lina zaidi ya miaka miwili hilo linaendelea vijana wamechoka kuvumilia"