Uchaguzi 2020 Padre wa Kanisa Katoliki aliyeomba Ubunge huko Kagera kupitia CCM asimamishwa rasmi kuendelea na wito

Gwajima na Msigwa sio dhehebu la RC.
Mbona Dr Slaa nae aliacha upadre akaiingia kwenye siasa
 
Kama barua hii ni halali basi nyie katoliki mko smart sana. Hata hivyo baada ya kupitia maandiko ya kikatoliki, huyu padre atakuwa na cheo cha Mlei. Na kazi za walei ni zile zile za kitume nje ya kanisa.

Akifanya kazi zake za kitume vizuri huko makazini hupewa cheo na kuwa Mtakatifu. Hakika katoliki wako smart sana. Nawapongeza.
 
Msigwa akigombea ubunge kupitia CHADEMA hakuna shida lakini kasisi wa katoliki akigombea ubunge hasa kupitia CCM ni tatizo kubwa.
Huyo kasisi kaandika barua ya kuomba kuachana n kutoa huduma kama kasisi kisha kaenda kugombea hii haina tofauti na alivyofanya Dr. Wilbroad Slaa.

Siyo habari ya kushika akili za watu majukwaani.
 
Nimeona mkuu wangu.
Ahsante kwa kunistua.
Mkuu, kwa itifaki za kanisa kile ni cheo chake na atakufa nacho. Papa alipostaafu aliendelea kuwa na hadhi ya upapa isipokuwa tu hafanyi misa takatifu. Kumu address Pengo wala hakuna shida.
 
Kasisi hata angegombea kupitia Chadema angesimamishwa tu. Hawaruhusiwi kabisa kuwa wanasiasa na hata Magufuli akisimama pale madhabahuni hawezi kamwe kutoa maamuzi ya kiuongozi akiwa pale zaidi ya kuongea tu kama muumini wa kawaida.
 
Hakujibiwa hiyo barua, maana Askofu pengine alihitaji kumsikia vizuri hoja zake katika mazungumzo. Lakini kwa kuwa kugombea nafasi za kisiasa ni jambo la hadharani, hilo ndilo limemfanya Askofu aandike barua ya kumsimamisha huduma, maana lipodhahiri zaidi kuliko barua ya Padre
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…