101 East
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 1,057
- 2,221
Katibu Mkuu wa Baraza La Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Dkt.Charles Kitima amesema kuhudhuria halfa ya utiaji saini Mkataba wa Host Government Agreement (HGA) iliyofanyika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma siku chache zilizopita haimaanishi kwamba wamekubaliana na mkataba wa Bandari kwani kulikuwa na mazingira ambayo yeye kama yeye asingeweza kujua nini hasa ameitiwa na asingeweza kuweka masharti kwa Rais baada ya kupewa mwaliko ambayo yeye (Kitima) hakuwa anajua lengo lake.
Kitima ameyasema hayo baada JAMBO TV kutaka kupata ufafanuzi wa kile ambacho kilitokea Ikulu Dodoma ambapo kwenye hafla ya kusaini mkataba wa HGA kauli mbalimbali zilisikika zikisema hata wale ambao mwanzoni waliukosoa Mkataba ule (IGA) nao wamehudhuria halfa ya utiaji saini Mkataba wa (HGA) kitendo ambacho kiliashiria kubadili kwao msimamo kuhusu waliyokuwa wanaeleza kama mapungufu ya Mkataba wa makubaliano kati ya serikali ya Tanzania na Dubai wa uendeshaji wa Bandari za Tanzania
" Hatujaona mabadiliko kimaandishi, Tunasimama na Tamko la Maaskofu, tukiona kimaandishi mabadiliko yaliyofanywa kwenye IGA ndipo tutaonana kama mapungufu yamefanyiwa kazi" amesema
Dkt. Kitima amesisitiza kwamba bado msimamo wa Kanisa Katoliki Tanzania ni kwamba IGA inayo mapungufu hivyo hawajabadili msimamo.
Jambo TV