Padri Dkt. Kitima: Sikujua sababu ya kuitwa Ikulu, msimamo wetu ni ule ule, hatukubaliani na IGA

Padri Dkt. Kitima: Sikujua sababu ya kuitwa Ikulu, msimamo wetu ni ule ule, hatukubaliani na IGA

Wala usimtilie maanani huyo Fr. Kitima. Hata Vatican yenyewe inamchukulia poa tu ndio maana ma junior wake wamepata u-Askofu kama vile Baba Askofu Msonganzila, Baba Mfumbusa kutaja wachache.
Kwa hiyo kila anaekuwa katibu Mkuu TEC anapaswa kuwa Askofu au Kadinali? Acha uzwazwa
 
Alialikwa bila kuambiwa mwaliko ulihusu nini

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayo furaha kukukaribisha

Bwana na Bibi/Bi/Prof/Dkt.

FR CHARLES KITIMA

katika Hafla Maalum itakayofanyika siku ya jumapili tarehe 22 Oktoba 2023, Ikulu Chamwino, Dodoma saa 04:00 asubuhi.

Jibu kwa: Mnikulu, Ikulu, Dodoma, Simu: +255 714 186 948

2000

Ikulu Chamwino, Dodoma

Tafadhali Njoo na Kadi Hii

Sent using Jamii Forums mobile app


hii haina tofauti na utapeli ofisi ya raic imetapeli kanisa likaingia mkenge.
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayo furaha kukukaribish....
Raisi ana mambo ya kihuni sana sijui alivyokuwa bint alikuwaje ila kwa uzee huo ni uhun hasa
 
CCM imejaa watu vichwa maji wengi.

Ukiona kijana ni mwanaccm,basi ujue uzeeni lazima awe mchawi au mnafikinafiki.

Wasisahau kuwa,Dunia imeshaenda viral Sana.So wasiishi kwa kukariri.

Ni hopeless asilimia kubwa,hawana maarifa ya kuchanganua Mambo yenye tija kwa Taifa,Bali wao wanawaza kutawala na vyeo.

Wakumbuke utafika mda ambao kutawala itakuwa Kama mwiba.

Chama Cha Ovyo SIJAPATA kuona.

Kimekuwa chama Cha wanyang'anyi,maana Kama unabiashara yoyote,ili kuepukana na usumbufu au dhahama ya mamlaka unatakiwa kuzuga na kitambulisho Cha CCM au kuweka bendera ya CCM.

Ufala uliopitiliza kwa majivuni ya Kunguni WA KIJANI.

Katiba mpya inatakiwa.
 
Katibu Mkuu wa Baraza La Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Padri.Dkt.Charles Kitima amesema kuhudhuria halfa ya utiaji saini Mkataba wa Host Government Agreement (HGA) iliyofanyika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma siku chache zilizopita haimaanishi kwamba wamekubaliana na mkataba wa Bandari kwani kulikuwa na mazingira ambayo yeye kama yeye asingeweza kujua nini hasa ameitiwa na asingeweza kuweka masharti kwa Rais baada ya kupewa mwaliko ambayo yeye (Kitima) hakuwa anajua lengo lake.Padri.

Kitima ameyasema hayo baada JAMBO TV kutaka kupata ufafanuzi wa kile ambacho kilitokea Ikulu Dodoma ambapo kwenye hafla ya kusaini mkataba wa HGA kauli mbalimbali zilisikika zikisema hata wale ambao mwanzoni waliukosoa Mkataba ule (IGA) nao wamehudhuria halfa ya utiaji saini Mkataba wa (HGA) kitendo ambacho kiliashiria kubadili kwao msimamo kuhusu waliyokuwa wanaeleza kama mapungufu ya Mkataba wa makubaliano kati ya serikali ya Tanzania na Dubai wa uendeshaji wa Bandari za Tanzania "

Hatujaona mabadiliko kimaandishi, Tunasimama na Tamko la Maaskofu, tukiona kimaandishi mabadiliko yaliyofanywa kwenye IGA ndipo tutaonana kama mapungufu yamefanyiwa kazi" amesema Dkt.Kitima akisisitiza kwamba bado msimamo wa Kanisa Katoliki Tanzania ni kwamba IGA inayo mapungufu hivyo hawajabadili msimamo.
 
Katibu Mkuu wa Baraza La Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Dkt.Charles Kitima amesema kuhudhuria halfa ya utiaji saini Mkataba wa Host Government Agreement (HGA)...
Haja ons mabadiliko kimaandishi, Lakini una mapungufu

Haoni kwamba anakanganya Kauli zake ? Kama hajaona, hayo mapungufu kayajuaje?
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayo furaha kukukaribish....
Kama mwaliko ulitolewa kwa maandishi yaliyoonyeshwa hapa, ni dhahiri kuwa hii ni serikali ya kitapeli, inayoendeshwa na viongozi matapeli.

Hizi nyadhifa za "Amiri Jeshi Mkuu" zinazotumiwa na matapeli kufanya uhalifu ifikie mahali wanao tumiwa vibaya na matapeli hawa inawapasa pia kukataa upumbavu huu wa matumizi mabaya ya kazi zao za ulinzi wa nchi hii.
 
Kwa nafasi yake alipaswa kunusa harufu!, ok ngoja tuone hizo changes zinazodaiwa kufanywa, mkataba hauwezi fichwa milele utaonekena tu
 
Back
Top Bottom