Haya, mtu mwenye fikra za namna hii utamchukuliaje unapokutana naye kama siyo kumwonea huruma tu.Kuhusu rasilimali za taifa hakuondoi mkataba kuwa ni siri ya pande mbili. Mjinga ni wewe uliyedhani kuvuja kwa mkataba wa IGA ni haki yako ya kuujadili, lile lilikuwa ni kosa la kimfumo ambalo limesharekebishwa tayari, hutakuja tena kuona mkataba wa aina ile.
Mjinga ni wewe unayedhani kuwa mmiliki wa mali za taifa ndio kuwa na kibali cha kujadili kila kinachojadiliwa na kufanyika, kama ni hivyo hakuna sababu ya kuwepo kwa nyaraka za serikali.
Hili la DP World mmepigwa na kitu chenye ncha kali utosini, tafuteni mada nyingine ya kujadili.
Anafikiri serikali ya kitapeli ina ruhusa ya kufanya uhalifu wowote ule iutakao na isihojiwe na yeyote!
Anaamini mikataba kuwa siri ni njia nzuri za kulihujumu taifa, na hao wahujumu hakuna lolote wanaloweza kufanywa kwa uhujumu wao.
Sasa anawika kabisa kama kidume na kuwaambia watu "wamekwishapigwa na chenye ncha kali" akijua yeye kwa akili zake finyu kwamba uhalifu umeshinda.