View attachment 3626933
View attachment 3626934
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Baba Mtakatifu Leo XIV amemteua Mheshimiwa Padre Vincent Lawrence Mpwaji wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, leo Julai 11, 2026.
Mhashamu Askofu mteule Padre Vincent Lawrence Mpwaji alizaliwa Juni 05 mwaka 1978 Jimbo Katoliki Morogoro.
Baada ya masomo yake ya upadre, alipata daraja Takatifu la upadre Julai 07 mwaka 2008 Jimbo Kuu la Dar es Salaam, na kuhudumu katika nafasi mbalimbali za utume ndani ya Jimbo kuu la Dar es Salaam.
Alipata Shahada ya Uzamivu katika Teolojia kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa, Gregorian Roma-Italia.
Hadi uteuzi wake Askofu mteule Mpwaji alikuwa Chancellor wa Jimbo kuu la Dar es Salaam na Paroko Msaidizi wa Kanisa kuu la Mtakatifu Yosefu, Dar es Salaaam.
.