Padri Henry Rimisho wa Kanisa Katoliki atunukiwaa PhD ya Architecture

Padri Henry Rimisho wa Kanisa Katoliki atunukiwaa PhD ya Architecture

Wana Jamii From!

Bila yakupoteza muda naomba kufahamu jambo moja zito ambalo kwa uelewa wangu nimeshindwa lipatia majibu!

Hivi inawezekana vipi Mtumishi wa Mungu Padre awe mwanajeshi tena komandoo??

Picha hapo chini ni Padre Henry,ambaye ni mwanajeshi komandoo,ambaye katunukiwa PhD yake ya Architecture!

Watumishi wa Kanisa Katoliki wanatoa huduma katika nyanja mbalimbali kulingana na mahitaji ya utume wao. Moja ya maeneo ya huduma ni kwa wanajeshi walio kwenye mapambano. Padri ambaye ni chaplain jeshini hupata mafunzo ya kijeshi si kwa ajili ya kupigana jeshini, bali kwa ajili ya kujiokoa na kuwaokoa wale anaowahudumia wakati wa mapambano. Si hivyo tu, hata kwa wale walio kwenye mafunzo - kama magereza, polisi na jeshi - kwa kawaida kuna padri ambaye anakuwa attached katika sehemu hizo kama chaplain. Na hata kwa hospitali, zahanati, dispensary na health centres na pia vyuo mbalimbali - kuna mapadri pia ambao wako attached katika sehemu hizo. Hivyo, mtu mwingine asiye na uelewa na wa aina hii ya utume anaweza akashangaa, lakini kwa wale wanaoelewa ni jambo la kawaida tu.
 
We yaelekea IQ yako ni ndigo sana, umeshindwa kuelewa content ya swali? Unafikili tuna-comment humu JF wote ni wa RC.
Bora iendelee kubaki "Ndigo" [emoji3][emoji23][emoji23] kajifunze kwanza kuandika.Kwa taarifa yako Padre mmoja wa RC ni sawa na wachungaji na maaskofu 10 wa madhehebu mengine! Sasa aende huko kufuata nini?
 
Pandre anasema alisoma HGE lkn akapenda afanye programme ya science (Architecture ) na akakubalowa baada ya kafanyiwa usaii was paper ya hesabu .....
 
Kwa sheria ya Tanzania hata kama sio za Jwtz bado iko pale pale, sheria zetu haziruhusu kuvaa mavazi yanayofanana na hayo
Huyo bwana anaruhusiwa kuvaa hayo mavazi ni sare ya nchi aliyokua au ambayo anatoa huduma
 
Huyo bwana anaruhusiwa kuvaa hayo mavazi ni sare ya nchi aliyokua au ambayo anatoa huduma
Ndiyo aliruhusiwa kuvaa huko kwa ajili ya kutoa huduma, ikawaje hadi avae ndani ya Tanzania....ni swala la muda ila kwa sheria zetu alichokifanya sio sawa!
Je ni Mtanzania? Iweje avae mavazi ya nchi nyingine isiyokuwa Tanzania. Sheria za Tanzania haziruhusu mtu asiyekuwa mwanajeshi kuvaa mavazi ya jeshi yawe ya Tanzania au ya nchi nyingine au yafananayo.
 
Waliosoma sana wanajikita katika falsafa na Theology, sayansi ni nadra sana. Hongera padre Rimisho. Ila nakuomba ujikite zaidi kwenye sayansi, Theology waachie wenyewe.
 
Back
Top Bottom