Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,536
- 7,194
Wakuu,
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima, ameeleza kuwepo kwa vikundi vilivyopangwa mtandaoni vinavyoshambulia watu na kuvuruga utamaduni wa uaminifu, huku akihoji sababu za watu hao kuachwa bila kukemewa.
Dkt. Kitima alibainisha hayo hivi karibuni:
"Unaona mtu anaanzisha vikosi vyake, viitwe sijui vikosi gani, anaachwa tu... Mwingine anaamua kumpuuza au kumtukana fulani, mwingine anaamua kutukana watu tu na anaachwa, na anafahamika ni fulani. Sasa unajiuliza, unashambulia serikali, unashambulia chama au watu? Hiyo siyo utamaduni wa Mtanzania. Watanzania tulikuwa tunaishi katika kupenda ukweli."