Padri Kitima: Unafiki na kusifia kila jambo ili kupata vyeo kutaliua Taifa

Padri Kitima: Unafiki na kusifia kila jambo ili kupata vyeo kutaliua Taifa

Mwambie maoni yake ni mazuri Ila aanzie ndani kwake kwanza maana Mapadri wamekuwa wanalawiti watoto na wengine wanauwawa kiutata sana.
Nasema uongo ndugu zanguuuu
Kwa sasa maadili ya kiimani yametoweka kwa dini zote.

Wakristu na waislam wote hawana tena huo utumishi wa kiimani.

Kila siku utasikia padre kawabaka waumini wake na kesho utasikia shehe kawarawiti wanachuo wake.
 
Rudi kwenye mada usichanganye mafaili kukwepa ukweli!!!
Hakuna cha ukweli hapo bali tuseme ukweli kuwa kipindi cha jiwe kila tukio la hovyo Hawa watu wa kanisa walijitahidi angalau kusema,

Ingawa siyo wote waliokuwa na huo uthubutu wa kukemea unyama.
 
Rais Samia, kama anataka uongozi wake uwe na tija kubwa, ni lazima awaondoe wanafiki wote ndani ya Serikali yake.

Ndani ya Serikali wamejaa watu wanafiki. Watu watoa rushwa ya sifa. Sifa wanazozitoa kwa Rais kw kila kitu, hata zisipostahili, ni rushwa ya sifa kwa Rais.

Kiongozi yeyote ana haki ya kusifiwa anapofanya jambo jema la pekee, lakini kumsifia Rais kwa kila kitu, tena kwa baadhi ya mambo ambayo ni ya kawaida kabisa au hata kwa yale ambayo yamefanyika vibaya, ni unafiki, ujinga, uwendawazimu, na rushwa kwa kiongozi anayesifiwa, na njia ya kumpofusha mtawala.

Hongera sana Baba Kitima, kwa kuunena ukweli.
Ugonjwa huu uliasisiwa na utawala wa jiwe
 
Yeye na Kanisa lake pia ni Wanafiki. Wakati wa Mwendazake ambaye ndiye mwanzilishi wa hii tabia hawakudiliki kusema kitu. Sana sana walimsifia.

Kwenye hili siliungi mkono Kanisa.
Hata usipounga mkono haitoondoa ukweli kuwa jiwe alikuwa ni mnyama.
 
Chawa wataanza kumparua Padre sasa hivi bila kupima uzito wa ujumbe wake.
Hili ni jambo la kweli kabisa. Utatuzi wake uko kwenye katiba. Vyeo visitolewe tena na mtu mmoja bali wananchi ndiyo wachague.
 
Mimi Ni mkristo lkn hii trend ya akiingia rais Muislam then RC na madhehebu mengine ya kikristo kujifanya yanamuwashia Moto sio fair.Enzi za JPM walitulia kimya na ujinga wote ule aliokua anafanya.

Pamoja na yote niliyosema lkn ujumbe wa Kitima Ni Valid.

Acha uongo we ni muumini wa makobazi na vibandiko iyo iko wazi. Kwa iyo kama uongozi uliopita ulikuwa na madhaifu hayo, basi tuendelee tu hivyohivyo? Ficha udini wako huko
 
Acha uongo we ni muumini wa makobazi na vibandiko iyo iko wazi. Kwa iyo kama uongozi uliopita ulikuwa na madhaifu hayo, basi tuendelee tu hivyohivyo? Ficha udini wako huko
Asante Sana mke wangu mzuri, hakika unanijua Sana Mumeo na dini ninayosali.
 
Wakati Azory Gwanda na Ben saanane wanatoweka mbona hawakusema haya?Magufuli alikuwa anafunga watu hovyohovyo anawapoteza,anawabambikizia watu kesi,anapora fedha za watu viongozi wetu wa dini walikuwa kimya!

Viongozi wetu wa dini mseme kila nyakati,hata zile nyakati za hatari.
Mkuu huyo Ben saanane ni baba yako mzazi au?
 
Padri yupo sahihi...lakini kwa nini hakutuyasikia haya kipindi cha JPM,ilifika hatua hadi anapewa mic kanisani ahutubie.....huku wakina Pengo wakimtaka Makonda awe raisi wa awamu ya Sita.
Ni kweli Padri Kitima yupo sahihi,"Unafiki wa kisiasa unaondelea miongoni mwa watanzania,utaliangamiza taifa"
Hata kipindi cha JPM huyo padre alibaki na msimamo wake.
 
Mapadre fanyeni kazi ya Mungu.

Maoni yenu kwa sasa yamechafuka.
Kwani hiyo ni kazi ya shetani?viongozi wa kiroho wanapoona mambo hayaendi vzr inawalazimu kukemea ili taifa lisiende kwenye machafuko.kuna wengine humu wana wajomba zao uarabuni hali ilibadilika wengine tutabaki tunachinjana na mifano ipo.
 
Wakati Azory Gwanda na Ben saanane wanatoweka mbona hawakusema haya?Magufuli alikuwa anafunga watu hovyohovyo anawapoteza,anawabambikizia watu kesi,anapora fedha za watu viongozi wetu wa dini walikuwa kimya!

Viongozi wetu wa dini mseme kila nyakati,hata zile nyakati za hatari.
Hao walioporwa ni majizi yalipata fedha kwa njia ovu.
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Charles Kitima ametahadharisha unafiki wa kisiasa unaoendelea miongoni mwa Watanzania kwa sasa kwa kupenda kusifia kila jambo kuwa utaliua taifa.

Amesema tabia hiyo inaendelea kupata mashiko nchini kutokana na upeo mdogo wa watu kushindwa kujua misingi ya haki za binadamu na badala yake wanatanguliza maslahi yao binafsi mbele .

Akizungumza leo Dar es Salaam, Septemba 30, 2022 katika kongamano la viongozi wa dini zote linaloangazia haki za binadamu nchini, kiongozi huyo amesema tabia hiyo iliyojengeka isipokomeshwa ni wazi mahusiano mazuri miongoni mwa Watanzania yanaenda kupotea.

"Unafiki unaharibu nchi, unafiki wa kisiasa uliopo miongoni mwa Watanzania kupenda kusifia viongozi ili tu kujipendekeza wapate vyeo unaenda kuliua Taifa na tatizo hili linaendelea kwa sababu watu hawajui misingi ya haki za binadamu," amesema Padri Kitima

Kiongozi huyo wa kiroho amesema hata kujitoa kwenye mahakama ya haki iliyopo Arusha na kuwahamisha wananchi kutoka Loliondo kwenda Handeni mkoani Tanga ni uvunjivu wa haki za binadamu.

"Kwa sababu nchi imeridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa inayohusu haki za binadamu," amesema

Amesema wao kama viongozi wa dini baada ya kuona tabia hiyo hususan miaka mitano iliyopita, mwaka 2020 walianza kuandika kitabu Cha elimu ya haki za binadamu kwa lengo la kuanza kutoka elimu watu wote.

"Haki za binadamu haziombwi, zinapiganiwa, dini ni kiungo muhimu na tumeona tufanye hivi na tunatarajia kuwafikia viongozi 16,000 nchi nzima na kushuka kwa Watanzania wote," amesema

Chanzo: Mwananchi
Hasa viongozi wa dini na serikali. Zamani viongozi wa dini walijitahidi kukemea na kukosoa mwenendo mbovu wa serikali—siku hizi wamekuwa kama wanasiasa tu.
 
Walimfanya Nini alipowatishia kuondoa exemption Kwny magari ya Taasisi za kidini, alipowahangaisha wakina Bagonza, Niwemugizi?

Na hayo aliyoyafanya Magu leo Samia akiwafanyia RC reaction ya kanisa itakuaje?

Wacha mboyoyo
walimsalia novena akafa


"A novena is a ritualistic devotional worship where one or more Christian devotees make petitions, implore favors, or obtain graces by honoring Jesus Christ, Virgin Mary or the saints of the faith who are believed to empower divine intervention"
 
Unafiki unaanza kwao
Akija wa kuwashikisha adsbu wanafunga midomo
Waendelee kuhubiri ya Mungu haya ya unafiki ni kila sehemu yapo na akija mbabe wanaufyata tena
 
Back
Top Bottom