Padri Prof. Emmanuel Wabanhu Ateuliwa Kuwa Makamu Mkuu Mpya Wa Chuo Kikuu Cha Mt Agustino Tanzania(SAUT)

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,933
FB_IMG_1784141820960.jpg
PADRE WABANHU ATEULIWA KUWA MAKAMU MKUU WA CHUO CHA SAUT

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), ambaye pia ni Kansela wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino cha Tanzania (SAUT), na Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Wolfgang Pisa, OFMCap, amemteua Padri Profesa Emmanuel Charles Wabanhu kuwa Makamu Mkuu wa chuo hicho kuanzia Agosti 1, 2026.

Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Ibara ya 11 ikisomwa pamoja na Kanuni ya 10 ya Hati ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania ya mwaka 2012, iliyochapishwa kupitia Tangazo la Serikali Na. 580 la mwaka 2020 chini ya Sheria ya Vyuo Vikuu, Sura ya 346, Toleo Lililofanyiwa Marejeo la mwaka 2023.

Prof. Wabanhu ni Padri wa Jimbo Katoliki la Geita na Profesa Mshiriki mwenye uzoefu mkubwa katika taaluma ya Teolojia ya Maadili, akibobea katika Maadili Tetezi (Applied Ethics). Amekuwa mhadhiri mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Katoliki cha Afrika Mashariki (CUEA), Nairobi nchini Kenya kwa zaidi ya miaka 13, kabla ya kuhudumu kwa miaka miwili kama Naibu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Utawala na Fedha katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Askofu Mihayo cha Tabora (AMUCTA).

Mbali na uzoefu wake wa kitaaluma, Prof. Wabanhu ameandika vitabu vitano na kuchapisha zaidi ya makala 20 za kitaaluma katika majarida yanayotambuliwa kimataifa.

Kitaaluma, anashikilia Shahada ya Kwanza ya Teolojia kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, Roma nchini Italia, Shahada za Uzamili katika Masomo ya Dini na Teolojia, Shahada ya Uzamivu wa Teolojia Takatifu (STD), pamoja na Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Maadili ya Jamii na Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Katholieke Universiteit Leuven nchini Ubelgiji.

Katika taarifa iliyotolewa Julai 15, 2026, na Ofisi ya Uhusiano wa Umma ya SAUT imempongeza Prof. Wabanhu kwa uteuzi huo na kueleza imani kuwa atalitekeleza vyema jukumu lake jipya. Chuo hicho pia kimewataka wanajamii wa SAUT na wadau wote kumpa ushirikiano na msaada anapoanza majukumu yake mapya.

Picha na Habari, Martine Nyoni - SAUT DIGITAL.
 
Afrika kazi ipo hawa watu kuteuliwa kuwa mapapa ngumu sana

huyu Prof padri namwangalia usoni sioni sura yake ikitawanyika nanyinyi mwangalieni papa harafu mrudi Kwa profesa tofauti kabisa
 
Wamefeli wamechukua VC na DVCAA hapo AMUCTA sijaona maendeleo waliofanya hapo chuoni ni bora wangelichukua wahadhiri kutoka CUHAS, Mwenge Catholic au Catholic University of Mbeya maana hata kwa macho maendeleo yanaonekana. Sina matarajio makubwa kutoka kwao.
 
Jifunze kusoma maelezo hajatoka AMUCTA
 
View attachment 3629826PADRE WABANHU ATEULIWA KUWA MAKAMU MKUU WA CHUO CHA SAUT

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), ambaye pia ni Kansela wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino cha Tanzania (SAUT), na Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Wolfgang Pisa, OFMCap, amemteua Padri Profesa Emmanuel Charles Wabanhu kuwa Makamu Mkuu wa chuo hicho kuanzia Agosti 1, 2026.

Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Ibara ya 11 ikisomwa pamoja na Kanuni ya 10 ya Hati ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania ya mwaka 2012, iliyochapishwa kupitia Tangazo la Serikali Na. 580 la mwaka 2020 chini ya Sheria ya Vyuo Vikuu, Sura ya 346, Toleo Lililofanyiwa Marejeo la mwaka 2023.

Prof. Wabanhu ni Padri wa Jimbo Katoliki la Geita na Profesa Mshiriki mwenye uzoefu mkubwa katika taaluma ya Teolojia ya Maadili, akibobea katika Maadili Tetezi (Applied Ethics). Amekuwa mhadhiri mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Katoliki cha Afrika Mashariki (CUEA), Nairobi nchini Kenya kwa zaidi ya miaka 13, kabla ya kuhudumu kwa miaka miwili kama Naibu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Utawala na Fedha katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Askofu Mihayo cha Tabora (AMUCTA).

Mbali na uzoefu wake wa kitaaluma, Prof. Wabanhu ameandika vitabu vitano na kuchapisha zaidi ya makala 20 za kitaaluma katika majarida yanayotambuliwa kimataifa.

Kitaaluma, anashikilia Shahada ya Kwanza ya Teolojia kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, Roma nchini Italia, Shahada za Uzamili katika Masomo ya Dini na Teolojia, Shahada ya Uzamivu wa Teolojia Takatifu (STD), pamoja na Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Maadili ya Jamii na Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Katholieke Universiteit Leuven nchini Ubelgiji.

Katika taarifa iliyotolewa Julai 15, 2026, na Ofisi ya Uhusiano wa Umma ya SAUT imempongeza Prof. Wabanhu kwa uteuzi huo na kueleza imani kuwa atalitekeleza vyema jukumu lake jipya. Chuo hicho pia kimewataka wanajamii wa SAUT na wadau wote kumpa ushirikiano na msaada anapoanza majukumu yake mapya.

Picha na Habari, Martine Nyoni - SAUT DIGITAL.
My teacher form one paleee kanda ya ziwa
 
Back
Top Bottom