Padri wa Kanisa Katoliki aliyefukuzwa afunguka

ni wivu tu....
 

All animals are equal, but some animals are more equal than others.​

 
Ninyi mmeshindwa kuchunguza hicho kisa mkatuletea hiyo habari hapa?
 
Wapo mapadre na waumini wengi tu ambao wanaombea na kutoa pepo,ila mpaka kanisa lijiridhishe kuwa unafanya kwa nguvu za kiMungu na sio utapeli.
 
Mkuu mimi huwa najiuliza mapadre wanalipwa mshahara ? na pia kuna hawa wengine mtu unakuta ni padre bado pia anafanya kazi serikalini madaktari, walimu na Fani mbalimbali malipo yao yanakuaje ? Analipwa mara mbili ?
 
Hakuna cha ajabu hapo. Kufanya kazi kwa Padre nchini kunahitaji vitu viwili: Mwajiri (yaani Kanisa) aseme anamhitaji na aridhike na sifa zake; na Uhamiaji waridhike kwamba mhusika hana tatizo la kiusalama nchini. Kwa Padre huyu, mwajiri ameona kasoro zimejitokeza za kiutendaji, ambazo hana ridhaa za kuutangazia umma, mbali na kumwambia mhusika. Hivyo, mwajiri ameamua aachane naye. Kwa upande mwingine, Uhamiaji hawajaona dosari za kiusalama za mhusika. Hivyo, hawana sababu za kumuondoa nchini.

Kanisa linaweza kuridhika na Padre mmoja lakini Uhamiaji wakagundua huyo ni CIA, kwa mfano, wakamnyima kibali cha kufanya kazi nchini. Padre huyo atafukuzwa nchini. Ni pale tu vyombo vyote viwili vinaporidhika kwa pamoja ndipo Padre atafanya kazi nchini.
 
Rc mmetisha,mpaka sasa wabongo hatujajua kosa lake? Nyie ndo mnapaswa kuwa usalama wa taifa.
Kwani mtumishi wa umma akifukuzwa kazi na mwajiri wake Taifa hutangaziwa kwamba amefanya kosa kadhaa? Kwa nini ulidai Kanisa litangaze kosa la Padre huyu? Kwanza, hiyo itakuwa kukiuka haki zake, na anaweza hata kwenda mahakamani kwa kudhalilishwa.
 
Nimeshasikia sn hii kitu mkuu!! Ni yule binti mwenye pacha wake ambaye alimuweka maabara pale dispensary kwake epiphany au huyo unae mzungumzia ni mwingin?
 
Mkuu mimi huwa najiuliza mapadre wanalipwa mshahara ? na pia kuna hawa wengine mtu unakuta ni padre bado pia anafanya kazi serikalini madaktari, walimu na Fani mbalimbali malipo yao yanakuaje ? Analipwa mara mbili ?
Huwa wanapewa posho ya mwaka mzima. Miaka ya 1990's wakati nasoma kwenye shule zao, walikua wanapewa posho ya Tsh. Milioni 1.5 hivi kwa mwaka. Na kwa kipindi kile, ilikuwa si haba. Sijui kwa sasa wanapewa kiasi gani.

Kuhusu hao Mapadre/Watawa Madaktari, walimu na wale wenye fani mbalimbali; utaratibu ulivyo ni kwamba mali zote wanazomiliki ni za Kanisa! Hivyo hata hiyo mishahara yao inatakiwa iingie kwenye mfuko wa Kanisa!

Ingawa kuna baadhi yao huwa wanajiongeza kwa kuanzisha miradi mbalimbali. Maana baadhi wana familia zinazo wategemea.
 
Ndugu, acha majungu. Kama una ushahidi, uliufikisha kwenye Baraza la Parokia; au kwa Paroko; au kwa Askofu? Njia zote hizo ziko wazi kusikiliza tuhuma hizo. Ninaongea hivyo kwa kufahamu mambo yaendavyo kikanisa kwa kuwa nimefanya kwenye mabaraza ya Parokia nchi tatu tofauti.
 
Wewe umepuyanga kwenye hiki ulichoandika. Unaonekana una matatizo makubwa sana, jitathmini ndugu
 
Hebu utoe huo ushahidi unaousema hapa jukwaani
 
Jimbo la Pwani linapatikana nchi gani
 
Ila hili suala la baadhi ya Mapadre/Maaskofu wa Kanisa Katoliki kuwa na watoto, aisee siyo majungu! Hili jambo lipo!

Mimi nimeishi kwa miaka mingi Wilaya ya Kilombero na Ulanga! Kule Majimbo Katoliki mawili ya Mahenge na Ifakara! Kiukweli kuna idadi kubwa sana ya Mapadre wenye watoto! Kuna Pandre mmoja alikuwa na watoto wawili aliozaa na mwalimu wa sekondari! Kuna mwingine alikuwa na watoto 4!

Na wanatumia jina la ukoo wake, na la mdogo wake! Lakini wananchi/waumini wanaona kila kinacho endelea! Amemjengea huyo mwanamke nyumba, na kumfungulia biashara!

Kwangu mimi kama Mkatoliki, natamani kuona Mapadre/Watawa wakipewa uhuru wa kuoa/kuolewa! Ili kupunguza haya mateso ya useja kwa binadamu walio kamilika.
 
Mkuu mimi huwa najiuliza mapadre wanalipwa mshahara ? na pia kuna hawa wengine mtu unakuta ni padre bado pia anafanya kazi serikalini madaktari, walimu na Fani mbalimbali malipo yao yanakuaje ? Analipwa mara mbili ?
Hapokei mshahara,mshahara wake unaingia shirikani kwake au jimboni kwake .Yeye anapewa na shirika hela ya matumizi.Nyingine zinatumika shirikani kwa shughuli za shirika kama matumizi kwa wote na miradi mbalimbali kama mashule hospitali na kusaidia wahitaji

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…