Ila hili suala la baadhi ya Mapadre/Maaskofu wa Kanisa Katoliki kuwa na watoto, aisee siyo majungu! Hili jambo lipo!
Mimi nimeishi kwa miaka mingi Wilaya ya Kilombero na Ulanga! Kule Majimbo Katoliki mawili ya Mahenge na Ifakara! Kiukweli kuna idadi kubwa sana ya Mapadre wenye watoto! Kuna Pandre mmoja alikuwa na watoto wawili aliozaa na mwalimu wa sekondari! Kuna mwingine alikuwa na watoto 4!
Na wanatumia jina la ukoo wake, na la mdogo wake! Lakini wananchi/waumini wanaona kila kinacho endelea! Amemjengea huyo mwanamke nyumba, na kumfungulia biashara!
Kwangu mimi kama Mkatoliki, natamani kuona Mapadre/Watawa wakipewa uhuru wa kuoa/kuolewa! Ili kupunguza haya mateso ya useja kwa binadamu walio kamilika.