Pahala sahihi na watu sahihi ndio watakaotambua thamani yako

Pahala sahihi na watu sahihi ndio watakaotambua thamani yako

Chaos Master

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2021
Posts
636
Reaction score
1,310
Nimeshawishika kuandika hii baada ya kuona uzi wa ndugu mmoja hivi aliekua akilalamika baada ya watu kumtenga punde tu baada ya kusimamishwa kazi. But unfortunately nimesahau jina lake mnaweza kunisaidia kum tag kwa aliewahi ona uzi wake

Mzee mmoja kabla hajafariki dunia, alimpa kijana wake saa⌚ kongwe kama kumbukumbu maishani. Akamwambia," huu ni urithi kutoka kwa babu yako.. Hii saa Ina umri wa zaidi ya miaka 150. Ili ujue thamani yake, nenda kaulize kwenye duka la saa mwisho wa mtaa. Waambie unataka kuiuza, waulize watakupa sh ngapi? ."

Kijana akarudi kwa babake na kumwambia jamaa wa dukani wametaka kulipa Shilingi 5000, kwa sababu saa ni ya zamani Sana.. Yaani imechakaa.."

Mzee akatabasamu😀Kisha akamwambia kijana wake, " nenda kwa muuza kahawa ukamsikilize pia."

Kijana akaenda kwa muuza kahawa. Muuza kahawa nae akaja na ofa ya sh 5000 pia, akidai saa ni ya zamani.. Kijana akampelekea jibu mzee wake. Mzee akatabasamu na kumwambia mwanae, " Nenda kwenye duka la kumbukumbu za vitu vya kale, Kisha uwaonyeshe hiyo saa.. Lile duka la mzungu pale posta.."

Kijana akarudi kwa babake akiwa na furaha.., " Baba, mzungu amesema atalipa milioni 20 kwa hii saa kongwe hadi nimeshangaa Wallahi. Sijaamini.. "

Mzee akasema," Nilitaka ufahamu kuwa pahala sahihi au watu sahihi ndio watakaofahamu thamani yako mwanangu. Daima usijipendekeze kwa watu wasiojua thamani yako. Jisogeze kwa watu wanaoijua thamani yako."

Anaejua thamani yako, atakuthamini na kukuheshimu. Usijilazimishe kukaa na wasiokuthamini. Usijilazimishe kuishi usipopendwa.."
"Hadithi tu sio maisha halisi ya yeyote"
 
Back
Top Bottom