Paji la uso na siri ya jicho la tatu

Kiongozi asante kwa uchambuzi wako .
Kuhusu ubatizo wa kikristo sijakutana na maelekezo kibiblia ya kuweka alama ya msalaba kwenye paji la uso. Zaidi sana ni kuzamisha kwenye maji kama ishara ya kufa , kuzikwa na kufufuka.
Warumi 6:3-4 inasema, "Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima."
Hatua ya kuzamishwa katika maji inadhihirisha kufa na kuzikwa pamoja na Kristo. Hatua ya kutoka nje ya maji yaashiria picha ya ufufuo wa Kristo.
Kuna mahali umeandika
"Lakini pia ukisoma kitabu cha ufunuo na habari za kutiwa Muhuri katika paji la uso utafahamu zaidi.."

Ufunuo 13:16-17 “Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa masikini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.”

Wanafisikolojia hutuambia kuwa ubongo wa mbele wa cerebrum [paji la uso] ndipo shughuli kama uamuzi, hukumu, na uhuru wa kutaka vinapofanyikia. Hivyo, Wakristo wanawekwa alama katika vipaji vya nyuso zao, pale tu wanapomkubali Yesu kuwa Mwokozi wao na kutunza amri kumi zote kwa kuhiari, au kutaka wao wenyewe bila kulazimishwa. Hii ndiyo maana muhuri au alama ya Mungu haiwekwi mkononi, kwa sababu Yesu hatawalazimisha watu kumwabudu na kuzitii amri zake.
Mkono humaanisha kulazimishwa kufanya kitu fulani kinyume na nia zetu kama tunavyoona katika maandiko matakatifu…
 
Mshana huu mmea huu
 
[emoji1545][emoji1545][emoji1545] sorry for late reply...ndio mada imepandishwa leo
 
Mimi maranyingi napoanza tu kufanya medidation kichwa kinakua kama kinaanza kuuma alafu mwili unakua kama unanisisimka hii itakua inasababishwa nanini
 
Mimi maranyingi napoanza tu kufanya medidation kichwa kinakua kama kinaanza kuuma alafu mwili unakua kama unanisisimka hii itakua inasababishwa nanini
Ni hatua za awali za kawaida usiache endelea hiyo hali itatulia
 
Àsante sana [emoji120]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…