Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
- Thread starter
- #681
Asante na hongera kwa kupata mafunuo mapya... Muda mwingi kinachotutesa na kutuumiza sana hakitoki mbali bali kiko ndani ya ufahamu wetu.. Hivyo tunapofunuliwa na mada kama hizi na kuweza kubadili mitazamo yetu, hujikuta tukitoka kwenye vifungo vilivyotutesa muda mrefu sana huku vikituachia makovu mengiMkuu Mshana Jr Asante sana kwa uzi huu ingaweje nimeuona tuu juzi. Nimeusoma mwanzo mwisho na michango yote pamoja na majibu uliyotoa. Hii thread imenifungua katika kifungo kikubwa sana. Nimeanza kusoma kitabu cha The power of your subconscious mind na naendelea kufunguka zaidi. Kusema ukweli shetani amekuwa ananitumia sana maana nimekuwa mtu mwenye hasira sizizo za kawaida, furaha kwangu ilikuwa ni kitendawili kikubwa sana. Kwa kifupi nimepitia mengi sana na watu wamenitenda vibaya sana kiasi kwamba vingine hata siwezi kuelezea ila kwa kifupi nimepitia mengi na mazito sana sana ila hii thread imenifungua sana. Nilianza Tahajudi baada tu ya kusoma hii thread na huwa nafanya usiku kabla ya kulala na Alfajiri na kwa mara ya kwanza baada ya miaka zaidi ya kumi nimejiona ni mwenye furaha. Mwili umekuwa mwepesi sana nimeanza kuwasahau watesi wangu na najiona kama nakuwa mpya kabisa. Nikijiangalia kwenye kioo najiona kama nimeanza kung'aa najiona mpya kabisa..nimeanza kuwaoana watu kama viumbe wa kawaida kwani hapa nyuma nilikuwa nawaona watu kama wanyama na sikuwa mtu wa kukutana na mtu yoyote yule na kumuona kama mwenzangu lazima niwe na tahadhari ya hali ya juu sana..kwa sasa nacheka na watu na nayaona maisha kama yenye furaha kwa sasa.
Sehemu nilipo kwa sasa sio tulivu sana ila najitahidi kuweka akili sehemu moja wakati wa kufanya tahajudi ila disturbance za hapa na pale zipo na siwezi kuzizuia maana nipo naishi Lodge kwa sasa kutokana na shughuli ninyafanya. Nimeanza na tahajudi ya kulala chali na kuvuta pumzi na kuiachia taratibu sana, jana nilifanya tahajudi na kuna wakati kama nilitaka kupaa vile nikawa nimeshtuka nikajikuta nimerudi kitandani ila kusema ukweli imenisaidia sana sana. Asubuhi naamka nikiwa mwepesi kabisa kitu ambacho sio kawaida yangu. Nimeanza kuwa mchangamfu sana hata wahudumu wa lodge waninishangaa mpaka mmoja juzi kaniuliza umekuweje mbona siku mbili tatu hizi umekuwa mwenye furaha sana?? Nikamwambia acha tu dada yangu mambo mengine tumwachie tu Mungu.
Mkuu Mshana Jr kuna jambo ambalo lilikuwa linanisumbua na hata baada ya kuanza tahajudi naona bado linanisumbua. Kwanza kabisa mm huwa napendelea sana kulala chali na mara kwa mara huwa napata ndoto za ajabu ajabu sana ila zinazonisumbuaga sana ni zile ndoto ambazo najikuta napiga story na ndugu zangu ambao ni marahemu. Wakati mwingine story zinakuwa nzuri ila wakati mwingine tunakuwa tunagombana. Hizi ndoto huwa zinaninyima amani kabisa. Baada ya kusoma thread yako na comments za watu kuhusu madhara ya kulala chali nilianza kujizoeza kulala kwa ubavu(sijui ndo unaita mshazari) basi hali kama imebadilika nikiweza kulala kwa ubavu sipati tena hzo ndoto...ila sasa tatizo ni kwamba nakilalala nalala kwa ubavu ila usiku nikishtuka najikuta nimelala chali na hyo mindoto ya ajabu ajabu ninakuwa tayari nimeipata ingawaje kwa sasa imepungua kidogo. Sasa mkuu hapa nifanyeje maana hii mindoto kweli huwa inanikera sana. Kwa mfano jana nilipata ndoto naongea na kaka yangu ambaye ni marehemu ananiomba nimtafutie kazi. sasa mm nikawa ninamuuliza nitakutafutiaje kazi wakati wewe ni marehemu, akawa anang'ang'ani tu nimtafutie kazi....mwisho tukaishia kugombana ndo nikastuka nikajikuta nimelala chali... Mkuu wangu ebu nisaidie kwanza nawezaje kulimaliza hili tatizo la ndoto za ajabuajabu kabla hatujaendelea na mengine maana ninayo mengi ambayo nitahitaji msaada kutoka kwako kama hutojali. Natanguliza asante,
Kuhusu kuota ni lazima uote.. Ndoto huleta afya ya akili lakini si zote... Sasa endelea kujizoeza kulala ubavu hata kama ukistuka usingizini umelala chali rudi kwenye position ya awali
Mwisho nakushauri sasa pamoja na kuendelea na tahajudi punguza matumizi ya vileo, nyama kahawa na kitunguu maji... Pia jizoeze kuogea maji ya chumvi kila mara