Paji la uso na siri ya jicho la tatu

Paji la uso na siri ya jicho la tatu

Mkuu Mshana Jr Asante sana kwa uzi huu ingaweje nimeuona tuu juzi. Nimeusoma mwanzo mwisho na michango yote pamoja na majibu uliyotoa. Hii thread imenifungua katika kifungo kikubwa sana. Nimeanza kusoma kitabu cha The power of your subconscious mind na naendelea kufunguka zaidi. Kusema ukweli shetani amekuwa ananitumia sana maana nimekuwa mtu mwenye hasira sizizo za kawaida, furaha kwangu ilikuwa ni kitendawili kikubwa sana. Kwa kifupi nimepitia mengi sana na watu wamenitenda vibaya sana kiasi kwamba vingine hata siwezi kuelezea ila kwa kifupi nimepitia mengi na mazito sana sana ila hii thread imenifungua sana. Nilianza Tahajudi baada tu ya kusoma hii thread na huwa nafanya usiku kabla ya kulala na Alfajiri na kwa mara ya kwanza baada ya miaka zaidi ya kumi nimejiona ni mwenye furaha. Mwili umekuwa mwepesi sana nimeanza kuwasahau watesi wangu na najiona kama nakuwa mpya kabisa. Nikijiangalia kwenye kioo najiona kama nimeanza kung'aa najiona mpya kabisa..nimeanza kuwaoana watu kama viumbe wa kawaida kwani hapa nyuma nilikuwa nawaona watu kama wanyama na sikuwa mtu wa kukutana na mtu yoyote yule na kumuona kama mwenzangu lazima niwe na tahadhari ya hali ya juu sana..kwa sasa nacheka na watu na nayaona maisha kama yenye furaha kwa sasa.

Sehemu nilipo kwa sasa sio tulivu sana ila najitahidi kuweka akili sehemu moja wakati wa kufanya tahajudi ila disturbance za hapa na pale zipo na siwezi kuzizuia maana nipo naishi Lodge kwa sasa kutokana na shughuli ninyafanya. Nimeanza na tahajudi ya kulala chali na kuvuta pumzi na kuiachia taratibu sana, jana nilifanya tahajudi na kuna wakati kama nilitaka kupaa vile nikawa nimeshtuka nikajikuta nimerudi kitandani ila kusema ukweli imenisaidia sana sana. Asubuhi naamka nikiwa mwepesi kabisa kitu ambacho sio kawaida yangu. Nimeanza kuwa mchangamfu sana hata wahudumu wa lodge waninishangaa mpaka mmoja juzi kaniuliza umekuweje mbona siku mbili tatu hizi umekuwa mwenye furaha sana?? Nikamwambia acha tu dada yangu mambo mengine tumwachie tu Mungu.

Mkuu Mshana Jr kuna jambo ambalo lilikuwa linanisumbua na hata baada ya kuanza tahajudi naona bado linanisumbua. Kwanza kabisa mm huwa napendelea sana kulala chali na mara kwa mara huwa napata ndoto za ajabu ajabu sana ila zinazonisumbuaga sana ni zile ndoto ambazo najikuta napiga story na ndugu zangu ambao ni marahemu. Wakati mwingine story zinakuwa nzuri ila wakati mwingine tunakuwa tunagombana. Hizi ndoto huwa zinaninyima amani kabisa. Baada ya kusoma thread yako na comments za watu kuhusu madhara ya kulala chali nilianza kujizoeza kulala kwa ubavu(sijui ndo unaita mshazari) basi hali kama imebadilika nikiweza kulala kwa ubavu sipati tena hzo ndoto...ila sasa tatizo ni kwamba nakilalala nalala kwa ubavu ila usiku nikishtuka najikuta nimelala chali na hyo mindoto ya ajabu ajabu ninakuwa tayari nimeipata ingawaje kwa sasa imepungua kidogo. Sasa mkuu hapa nifanyeje maana hii mindoto kweli huwa inanikera sana. Kwa mfano jana nilipata ndoto naongea na kaka yangu ambaye ni marehemu ananiomba nimtafutie kazi. sasa mm nikawa ninamuuliza nitakutafutiaje kazi wakati wewe ni marehemu, akawa anang'ang'ani tu nimtafutie kazi....mwisho tukaishia kugombana ndo nikastuka nikajikuta nimelala chali... Mkuu wangu ebu nisaidie kwanza nawezaje kulimaliza hili tatizo la ndoto za ajabuajabu kabla hatujaendelea na mengine maana ninayo mengi ambayo nitahitaji msaada kutoka kwako kama hutojali. Natanguliza asante,
Asante na hongera kwa kupata mafunuo mapya... Muda mwingi kinachotutesa na kutuumiza sana hakitoki mbali bali kiko ndani ya ufahamu wetu.. Hivyo tunapofunuliwa na mada kama hizi na kuweza kubadili mitazamo yetu, hujikuta tukitoka kwenye vifungo vilivyotutesa muda mrefu sana huku vikituachia makovu mengi
Kuhusu kuota ni lazima uote.. Ndoto huleta afya ya akili lakini si zote... Sasa endelea kujizoeza kulala ubavu hata kama ukistuka usingizini umelala chali rudi kwenye position ya awali
Mwisho nakushauri sasa pamoja na kuendelea na tahajudi punguza matumizi ya vileo, nyama kahawa na kitunguu maji... Pia jizoeze kuogea maji ya chumvi kila mara
 
Nashukuru sana mkuu wangu...nitafanyia kazi ushauri wako...nashukuru sana
 
Mshana jr kwahio tukilala chali ndo kusema mlango wa faham mmoja tunakuwa tumeacha wazi hivyo unaendelea kuwasiliana hata kama tumelala???
Tuanzie hapo kwanza
 
Mshana jr kwahio tukilala chali ndo kusema mlango wa faham mmoja tunakuwa tumeacha wazi hivyo unaendelea kuwasiliana hata kama tumelala???
Tuanzie hapo kwanza
Nadhani mada hii imelifafanua hilo hebu rudia kusoma tena
 
Habari Mkuu..nimefatilia Uzi wako uko vzr sana,,na hata hivyo Jana nilianza kufnya meditation kama dakika kadhaa hivi nikaanza kuona mambo niliyofny asbh yake pamoja na siku zilizopita pia nikaanza kuhis uzito ktk paji la USO Mkuu,nikaamua kufumbua macho nakuacha. Baada ya hapo nilianza kuona maluweluwe nakusikia saut za ajbu kisha zinapotea na hta usiku kiukwel nimeweweseka sana Mkuu na mpka sasa kichwa kinauma ktk paji la uso ,nifanyaje mkuu?....Napia Mara nyinyi nimekuwa na uwezo wakuhisi kitu then huwa kinakuwa kweli au kama nyumbn Kuna tatzo mara nyingi huwa sipati usingizi nikipiga cm usiku either mama anaumwa au kuna tatz lingine na hii inasababishwa na nini?...
 
Umeanza vizuri sana hukupaswa kuacha na sawa na ujenzi wa barabara mpya mwanzo huwa na mvurugano mwingi lakini kadiri unavyoendelea hupata mwelekeo na hatimaye barabara kamili kujitokeza... Endelea usiache
 
Tunafundishwa kutolala chali kuepuka ndoto za mauzauza na majinamizi kumbe siri ni jicho la tatu jicho la maono.

[emoji121] Mkuu Mshana Jr unaweza fafanua zaidi hapo, hili tatizo ninalo.
 
Back
Top Bottom