Paka kuchukuliwa kama mwanafamilia kwa kutengewa bajeti yake, inakubalika?

Paka ni wastaarabu ila ni pia ni mawaki laana, Uwaki wao ni pale ukimnyima msosi anakua mwizi balaa tena anatafuta na genge la paka wengine wezi wanakua na kakikundi chao wanakaa kabisa had maskani alaf usiku anakuja nao hapo home kufunua masufuria.

Alaf ni bingwa wa kukariri mitaa hata ukamtupe wapi atarudi tu home labda umteke umfunge macho ndo ukamtupe
 
Jamaa umenichekesha Sana.
Sasa mkuu wewe si ndio kichwa cha familia yako embu tumia udikteta wa kiafrika kidogo, ondoa huyo paka bakiza mbwa .
Ukiwaendekeza hao watoto wako na mkeo watakupanda kichwani.
Heri umgharamie mbwa manake anakulinda usiku sasa huyo paka wa kazi gani wakati umesema nyumbani hakuna panya
Mimi home kwangu nafuga mbwa kwa sababu ya ulinzi nimemuwekea order ya Msosi Kwenye bar Jirani kuna do go wa jikoni kila siku nampa buku ananiwekea mabaki ya mifupa na nyama zilizobaki na pia nimenunua pumba na dagaa wale wa kutengenezea chakula cha kuku dogo wa bar akizingua anapikiwa .
Ila Mimi binafsi sipendi kabisa hiki kiumbe kinachoitwa paka na sitegemei kabisa nyumbani kwangu nitaruhusu kufugwa kwa hicho kiumbe
 

Kwani hujui wanapouza sumu? Au unategemea tukushauri mpaka kwenye mambo madogo madogo kama haya?
 
Kama uwezo wa kumhudumia unao, Basi kubali aendelee kufugwa.

Yawezekana huoni faida yake lakini haujajua kuwa furaha inayopatikana ndani ya ndoa yako imekamilika kupitia paka huyo.

Humtaki paka kwa kuwa ndani mwako hamna panya?

Kazi ya paka siyo kukamata panya tu, Penye paka huwezi muona nyoka.

NOTE: Kama matunzo ya paka huyo yana gharama kubwa basi mshauri mkeo kwa busara apunguze bajeti kwa paka huyo, Maana ukitumia mabavu ukamuondoa paka ujue watoto wako na mkeo watakuchukia na huo ndo utakuwa mwanzo ndoa yako kuparaganyika.
 
NAKAZIA [emoji654][emoji654][emoji654]suluhu ni katiba mpya tu .....


Alafu wewe mtoa mada huyo paka ,, mroast vizuri umle nyama.
 
Jumamosi nilitoka na jamaa flani kwenda kwa Mhindi mmiliki wa kampuni flani kubwa. Baada ya kazi yetu tunataka kuondoka wafanyakazi wakatuita tule, sasa tumekaa sebuleni na paka yuko pale pale hasogei wala hatuachii seat kama paka wa kwetu uswahilini. Yule jamaa akamfukuza ila paka hatishiki nikamkaripia yule bro nikamkumbusha yule paka yuko kwao sisi ndio walugaluga tumedowea tu msosi. Paka mwenyewe anaelewa Kihindi afu jamaa anamuita pussy, nyau wala harespond
 
Kwamba paka anaelewa kihindi ila jamaa kang'ang'ana tu pussy, nyau hahah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…