Paka kunifatafata ni jambo la kawaida?

Paka kunifatafata ni jambo la kawaida?

Habari zenu waungwana wa humu ndani,

Nina jambo lanitatiza sana, kila nikiishi pahali lazima nifatwe na Paka, yaani atokee Paka aweke kambi kwangu, nikianzia kwetu kwa wazazi alikuja kipaka kidogo nikawa nampa chakula baadae kikaanza kuingia ndani, haikua rahisi kwa wazazi kumpokea lakini baadae wakampokea, basi tuliishi nae hadi alipofariki, baadae kakaja kengine kadogo nikakachukua pia, alikulia pale, akazaa, akafariki akaacha mtoto akakua pale mimi niliondoka baadae akaja kufariki,

Nilipohamia, ile nyumba nilikuta wapangaji wawili na mimi nikawa watatu, baada ya wiki kadhaa tangu nihamie wakaja paka watatu, wakaanza kuweka kambi eneo langu, wenzangu waliwafukuza lakini haikufua dafu, walishangaa kabla hawakuwahi kufatwa na hao Paka, nikaamua tu niwe nawapa chakula, mpaka siku moja asubuhi Paka mmoja alifariki mbele ya macho yangu nahisi aliwekewa sumu, nikahama hilo eneo kwa sababu zangu sio kwa ajili ya Paka,

Nilipohamia napo akaja kipaka kidogo kikaanza mazoea na mimi, Mbwa walikua wanamsumbua nikawa namsaidia wasimguse na kumpa chakula pia, sikukaa sana eneo hilo nikahama kutoka wilaya moja kwenda nyingine,

Nyumba niliyohamia, mwenye nyumba aliishi eneo hilo pia,alikua anafuga Paka, baada ya muda kidogo yule Paka akaanza kuja kwangu, akawa kwao haendi kabisaa anashinda na kulala kwenye baraza yangu, mwenye nyumba akahuzunika kama vile nimemteka Paka wake lakini haikuwezekana kumtoa , alipata Mimba akajifungua akaacha watoto kwao akawa anashinda kwangu tu, hadi nilipohama eneo hilo,

Nilipohamia napo nikakuta mpangaji mmoja ana Paka wake mzuri Maa shaa Allah, heeeh akaanza kuja kwangu, nikimpa chakula anakula lakini cha kwao hali, sikukaa sana hapo nikahama.

Hapa nilipohamia sasa hivi mmh, mwezi mmoja umepita kwa amani, sasa nikashangaa siku moja asubuhi naamshwa na sauti za Paka, nafungua mlango asalaleee nakuta vipaka vitatu vimejitandaza barazani kwangu havina habari, nikatoka wawili wakakimbia mmoja akabaki, sasa imekua utaratibu wao wapita nyumba zoote wanakuja kwangu kuweka kambi hawa nimesema siwapi chakula tuone kama wataishi,

Lakini nimejiuliza sana, kwanini Paka wananipenda na kunifata? Kuna nini nyuma ya pazia? Na hii sio tu kwa nyumba nilizoishi hata nyumba yoyote yenye Paka nikifika tu lazima anizoee au hata njiani nikikutana na Paka hawezi nikimbia atasimama na ku meow,

Nini hii jamani?

View attachment 1510235

Nyota yako ni ya Paka.
 
Juzii tu hapa nilienda kutembea kwa watu nashangaa Paka ananifata hadi miguuni wenyeji wanasema hao Paka hawana makazi walizaliwa wanazagaa zagaa na hawajawahi kusogelea nyumba yao zaidi ya kukatiza tena kwa mbio ndefu,
Basi nilivyopewa historia hiyo nikamnyanyua hakubisha ninakuweka mapajani kumuangalia vizuri jamani kana mimbaaaa, yaan kaPaka kadogo wamekajaza Mimba kumbe mifedhuli sio binaadam tu hadi wanyama! [emoji2][emoji2][emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] tena paka wanapenda kutiana hao hatare, na style zao km binadamu vile,
Kalikua ka mwanafunzi nini, kamepotezewa future yake.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] tena paka wanapenda kutiana hao hatare, na style zao km binadamu vile,
Kalikua ka mwanafunzi nini, kamepotezewa future yake.
Eenh wanapenda kubanjuana ndio maana wamekapa mimba mapema bado kanasoma form two,

Si ajabu sie wanaadam ndio tumeiga styles zao.

[emoji23][emoji23]
 
Binafsi nawapenda paka, wana hisia flani hivi za kweli na wanapenda sana urafiki na binadamu.

Kuna paka mmoja walizaa watoto wapi huko sijui, wale watoto wakaja kwenye chumba changu. Wakawa wakimsikia mama yao wanajifucha hawataki kwenda. Yule mama paka akaanza kuni-mind akidhani labda nimewarubuni mabinti zake. Alikuwa akija usiku anapiga makelele huyo, anakwangua dirisha hadi sio poa.

Nakumbuka nilifungua hadi uzi humu chit chat kujaribu kumueleza mama paka kuwa hao binti zake wamekuja wenyewe.
 
Kwasisi tunaoishi maeneo ya mashamba paka ni walinzi wa viumbe wadogo wadogo kama nyoka na kadhalika, ingawa paka akiingia ndani anapenda sana uboss ndio maana hawaelewani na mbwa
Kuna mtu alisema nyumba kukiwa na Paka na Mbwa basi Paka humuona Mbwa kama mnyama na yeye binaadam,

Kwa uboss upo sahihi wao hujiona ni wana familia kabisa.
 
Binafsi nawapenda paka, wana hisia flani hivi za kweli na wanapenda sana urafiki na binadamu.

Kuna paka mmoja walizaa watoto wapi huko sijui, wale watoto wakaja kwenye chumba changu. Wakawa wakimsikia mama yao wanajifucha hawataki kwenda. Yule mama paka akaanza kuni-mind akidhani labda nimewarubuni mabinti zake. Alikuwa akija usiku anapiga makelele huyo, anakwangua dirisha hadi sio poa.

Nakumbuka nilifungua hadi uzi humu chit chat kujaribu kumueleza mama paka kuwa hao binti zake wamekuja wenyewe.
Wallah nimecheka mnooo, kwa hiyo Mama Paka akahisi umewarubuni binti zake [emoji3][emoji3]
sasa na wewe uliishi nao vipi Paka wadogo ulikua unawalisha nini?
 
Wallah nimecheka mnooo, kwa hiyo Mama Paka akahisi umewarubuni binti zake [emoji3][emoji3]
sasa na wewe uliishi nao vipi Paka wadogo ulikua unawalisha nini?
Nilikuwa nawalisha ninachokula. kuna naye mwingine alikuwa ni paka wa jirani alikuwa mjamzito, alipoona anakaribia kujifungua akahamia kwangu mpaka akajifungua.

Paka wana tabia za ajabu sana.
 
Nilikuwa nawalisha ninachokula. kuna naye mwingine alikuwa ni paka wa jirani alikuwa mjamzito, alipoona anakaribia kujifungua akahamia kwangu mpaka akajifungua.

Paka wana tabia za ajabu sana.
Paka ni Mnyama anayependa raha kuliko wanyama wote duniani ndio maana huishi/humfata mtu anayewapenda hapendi shida maisha yake,

Sio loyal kama mbwa, siku akiona changes kwako ataondoka na huko aendako akizinguliwa atarudi na hakuna kitu utamfanya,[emoji23]
 
Labda harufu ya manukato unayotumia nyumbani na nkuvaa inawavutia paka
 
Paka ni Mnyama anayependa raha kuliko wanyama wote duniani ndio maana huishi/humfata mtu anayewapenda hapendi shida maisha yake,

Sio loyal kama mbwa, siku akiona changes kwako ataondoka na huko aendako akizinguliwa atarudi na hakuna kitu utamfanya,[emoji23]
Hakika mkuu, ila mi nawapenda maana they are so cute...

Ukiwa free mnacheza wee, na ukimtizama usoni unaona kabisa anafurahia.😂

Akiwa amepumzika zake uanze kumsumbua utaona anamind, anakuwa anakutishia na vimikono vyake..😂
 
Back
Top Bottom