Pakistan wana bidhaa nzuri na bora, lakini tumekariri Dubai, Uturuki, China na Thailand

Tatizo la Pakistan ni kiwa ukienda passport yako
Umemaliza mkuu yaani jamaa wana bidhaa nzuri sana sema hawatajwi kabisa
tatizo ukienda Pakistan passport yako kupata visa kwenda Marekani na Ulaya inakuwa Shida.Toka Osama bin Laden akutwe kwao kwao imekuwa issue kubwa.Ndio maana wengi wana avoid sana Pakistan kuogopa passport zao kuwa blacklisted nchi za magharibi na marekani
 
Hivyo viwanda nadhami vianzishwe huku huku Tanzania ili kupunguza gharama za usafiri
 
Unapofanya biashara za kimataifa, kuna mambo mengi yakuyapitia. Sio kuanza tu kuagiza.

Ndio maana. Tunashauriana hapa ni jukumu la mfanyabiashara kufanya tafiti zaidi kufahamu kwa undani hayo mambo
 
Hao jamaa hata kwenye Car Spare Parts wako vizuri tu nilishafanya nao biashara sana miaka ya 2010.
Nb: Sio kununulia Pakistan bali kwa wapakistan walio na maduka Dar.

Ndio hasa ukipata namna ya kufuata bidhaa zao kwao unaweza usijute na bei zao sio kali sana kama tunavowaza
 
Sasa kama wamejifungia nani atawafata
 
Viwanda vidogo vidogo unaweza anzisha hata wewe tatizo ni kushindana na wachina.

Utatengeneza ili uuze kwa 50,000 ila mchina atauza kwa 45,000 ubora mbovu ila Mtz ataona bora hiyo
Mtanzania anapenda kitu quality kwa bei ndogo , ukimuuzia cha bei ndogo kibovu analalamika ukimuuzia cha bei kubwa lakini quality still analalamika bei
 
Kweli kabisa. Hao jamaa wanajituma sana. Check hii page kwenye Facebook
 
Sasa kama wamejifungia nani atawafata
Ni sehemu moja risk pia madawa mengi ya kulevya hutokea Pakistan

Mizigo ya kuagiza Pakistan kuna risk zake mziho waweza.kuwa na mixigo.mingine ndani ya mzigo husika mtu ukadakwa
 
Ni sehemu moja risk pia madawa mengi ya kulevya hutokea Pakistan

Mizigo ya kuagiza Pakistan kuna risk zake mziho waweza.kuwa na mixigo.mingine ndani ya mzigo husika mtu ukadakwa
Kule wapo Kitalebani sana hamna kitu , utaingia matatani tuu
 
Kule wapo Kitalebani sana hamna kitu , utaingia matatani tuu
Talebani wanatengenea sana mihadarati kama source kubwa ya income ya kuendesha serikali na harakati zao ni kama Alshabab Somalia ni wanategemea mauzo hasa ya mirungi nchi za nje
 

Maelezo yako bado hayajajitosheleza yaan unasema pakistan kuna hili na lile alf hujui hata specific way ya kununua vitu.
 
Maelezo yako bado hayajajitosheleza yaan unasema pakistan kuna hili na lile alf hujui hata specific way ya kununua vitu.
Kuna njia kadhaa ambazo unaweza kutumia kununua vitu kutoka Pakistan ikiwa upo Tanzania.

Moja ya njia hizo ni kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao. Kuna tovuti nyingi za biashara mtandaoni zinazotoa huduma ya mauzo na usafirishaji wa bidhaa kutoka Pakistan kwenda sehemu nyingine duniani, ikiwemo Tanzania. Unaweza kutumia huduma za tovuti kama Amazon, eBay, Alibaba, au Daraz.pk kununua bidhaa unazotaka na kuzisafirisha kwako.

Njia nyingine ni kutafuta wasafirishaji binafsi ambao wana nia ya kusafirisha vitu kutoka Pakistan hadi Tanzania. Unaweza kutafuta wasafirishaji kupitia tovuti za biashara mtandaoni, kama vile Alibaba, na kuwasiliana nao moja kwa moja kuhusu gharama za kusafirisha bidhaa na muda wa usafirishaji.

Ni muhimu kukumbuka kuwa kabla ya kufanya manunuzi kutoka nje ya nchi, unapaswa kujua sheria na taratibu za usafirishaji na kodi za nchi yako ili kuepuka matatizo yoyote yanayoweza kujitokeza wakati wa kusafirisha bidhaa.

Pia ujue kabisa sijawahi kuagiza vitu kutoka Pakistan, tafuta mtu aliyewahi kuagiza vitu kutoka Pakistan ndio atakupa maelezo unayotaka kuyasikia, sio mimi
 
Mtanzania anapenda kitu quality kwa bei ndogo , ukimuuzia cha bei ndogo kibovu analalamika ukimuuzia cha bei kubwa lakini quality still analalamika bei
Tungekuwa twataka quality tusingenunua vitu vya mafungu KKOO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…