Pakistan wana bidhaa nzuri na bora, lakini tumekariri Dubai, Uturuki, China na Thailand

Pakistan wana bidhaa nzuri na bora, lakini tumekariri Dubai, Uturuki, China na Thailand

Tatizo la Pakistan ni kiwa ukienda passport yako
Umemaliza mkuu yaani jamaa wana bidhaa nzuri sana sema hawatajwi kabisa
tatizo ukienda Pakistan passport yako kupata visa kwenda Marekani na Ulaya inakuwa Shida.Toka Osama bin Laden akutwe kwao kwao imekuwa issue kubwa.Ndio maana wengi wana avoid sana Pakistan kuogopa passport zao kuwa blacklisted nchi za magharibi na marekani
 
Wakuu
Pakistan hua hatuitaji kibiashara wala hata bidha zao hatuzitaji lakini kiuhakika jamaa kwa viwanda vidogo na vikubwa nao sio haba,
Bidhaa zao nyingi ni bora na za kiwango cha juu hivo ni muhimu sana kuelekeza macho nchi nyingine kama hizo,
Nadhani tusiendelee kukariri sehemu ya kuchukua bidhaa,
Hao jamaa hawana promo lakini siku watu wengi wakistuka watajua kumbe wanapoteza muda kwingine na machimbo bora yako pakistan, tusiwachukulie poa jamaa wako vizuri
Hivyo viwanda nadhami vianzishwe huku huku Tanzania ili kupunguza gharama za usafiri
 
Unapofanya biashara za kimataifa, kuna mambo mengi yakuyapitia. Sio kuanza tu kuagiza.

Ndio maana. Tunashauriana hapa ni jukumu la mfanyabiashara kufanya tafiti zaidi kufahamu kwa undani hayo mambo
 
Hao jamaa hata kwenye Car Spare Parts wako vizuri tu nilishafanya nao biashara sana miaka ya 2010.
Nb: Sio kununulia Pakistan bali kwa wapakistan walio na maduka Dar.

Ndio hasa ukipata namna ya kufuata bidhaa zao kwao unaweza usijute na bei zao sio kali sana kama tunavowaza
 
Sasa kama wamejifungia nani atawafata
 
Viwanda vidogo vidogo unaweza anzisha hata wewe tatizo ni kushindana na wachina.

Utatengeneza ili uuze kwa 50,000 ila mchina atauza kwa 45,000 ubora mbovu ila Mtz ataona bora hiyo
Mtanzania anapenda kitu quality kwa bei ndogo , ukimuuzia cha bei ndogo kibovu analalamika ukimuuzia cha bei kubwa lakini quality still analalamika bei
 
Ni kweli kuwa Pakistan ina viwanda vingi, vidogo na vikubwa, na bidhaa nyingi kutoka Pakistan ni bora na za kiwango cha juu. Ni muhimu kwa nchi nyingine kutambua hilo na kuanza kuzingatia fursa za biashara na uwekezaji na Pakistan.

Kuna bidhaa nyingi kutoka Pakistan ambazo zinaweza kuvutia masoko ya kimataifa, kama vile nguo, vito vya thamani, ngozi, bidhaa za ngozi, vifaa vya michezo, madawa, na zaidi. Ni muhimu kwa wafanyabiashara kufanya utafiti na kuzingatia fursa za biashara na uwekezaji kutoka Pakistan.

Tunaweza kufanya kazi kwa karibu na serikali ya Pakistan na wafanyabiashara wake ili kukuza biashara ya pande zote. Kupitia ushirikiano huu, tunaweza kufikia mafanikio makubwa katika biashara na uwekezaji, na pia kukuza uhusiano mzuri kati ya nchi zetu mbili.
Kweli kabisa. Hao jamaa wanajituma sana. Check hii page kwenye Facebook
 
Sasa kama wamejifungia nani atawafata
Ni sehemu moja risk pia madawa mengi ya kulevya hutokea Pakistan

Mizigo ya kuagiza Pakistan kuna risk zake mziho waweza.kuwa na mixigo.mingine ndani ya mzigo husika mtu ukadakwa
 
Ni sehemu moja risk pia madawa mengi ya kulevya hutokea Pakistan

Mizigo ya kuagiza Pakistan kuna risk zake mziho waweza.kuwa na mixigo.mingine ndani ya mzigo husika mtu ukadakwa
Kule wapo Kitalebani sana hamna kitu , utaingia matatani tuu
 
Kule wapo Kitalebani sana hamna kitu , utaingia matatani tuu
Talebani wanatengenea sana mihadarati kama source kubwa ya income ya kuendesha serikali na harakati zao ni kama Alshabab Somalia ni wanategemea mauzo hasa ya mirungi nchi za nje
 
Kuna njia mbalimbali za kutangaza bidhaa za Pakistan, ikiwa ni pamoja na matangazo katika vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, maonyesho ya biashara na uuzaji mkondoni.

Ili kuagiza bidhaa kutoka Pakistan, unaweza kutumia mtandao wa intaneti na kutafuta wauzaji au wasambazaji wa bidhaa hizo. Pia unaweza kufikiria kutumia huduma za makampuni ya usafirishaji mizigo au wasafirishaji wa kibinafsi ambao wanaweza kukusaidia kuagiza bidhaa kutoka Pakistan. Ni muhimu kuhakikisha kuwa unafanya biashara na wauzaji wa kuaminika na wanaofuata taratibu na sheria za biashara.

Maelezo yako bado hayajajitosheleza yaan unasema pakistan kuna hili na lile alf hujui hata specific way ya kununua vitu.
 
Maelezo yako bado hayajajitosheleza yaan unasema pakistan kuna hili na lile alf hujui hata specific way ya kununua vitu.
Kuna njia kadhaa ambazo unaweza kutumia kununua vitu kutoka Pakistan ikiwa upo Tanzania.

Moja ya njia hizo ni kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao. Kuna tovuti nyingi za biashara mtandaoni zinazotoa huduma ya mauzo na usafirishaji wa bidhaa kutoka Pakistan kwenda sehemu nyingine duniani, ikiwemo Tanzania. Unaweza kutumia huduma za tovuti kama Amazon, eBay, Alibaba, au Daraz.pk kununua bidhaa unazotaka na kuzisafirisha kwako.

Njia nyingine ni kutafuta wasafirishaji binafsi ambao wana nia ya kusafirisha vitu kutoka Pakistan hadi Tanzania. Unaweza kutafuta wasafirishaji kupitia tovuti za biashara mtandaoni, kama vile Alibaba, na kuwasiliana nao moja kwa moja kuhusu gharama za kusafirisha bidhaa na muda wa usafirishaji.

Ni muhimu kukumbuka kuwa kabla ya kufanya manunuzi kutoka nje ya nchi, unapaswa kujua sheria na taratibu za usafirishaji na kodi za nchi yako ili kuepuka matatizo yoyote yanayoweza kujitokeza wakati wa kusafirisha bidhaa.

Pia ujue kabisa sijawahi kuagiza vitu kutoka Pakistan, tafuta mtu aliyewahi kuagiza vitu kutoka Pakistan ndio atakupa maelezo unayotaka kuyasikia, sio mimi
 
Mtanzania anapenda kitu quality kwa bei ndogo , ukimuuzia cha bei ndogo kibovu analalamika ukimuuzia cha bei kubwa lakini quality still analalamika bei
Tungekuwa twataka quality tusingenunua vitu vya mafungu KKOO
 
Back
Top Bottom