Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Ni hivi kwenye familia moja ya wagalatia huko mkoa X, kama unavyojua katika madhehebu fulani Fulani hivi usipo hudhuria ibada wakati wa Uhai wako basi wakati wa kifo chako nao hawahudhurii pia.
Basi Kaka mtu na mdogo wake wote ni walevi wa haja Tu,kama unavyojua kifo hakina taarifa mwisho wa siku kiumbe wa Mungu siku yake ikawadia na kurudisha namba Kwa mwenyewe.
Basi kwenda Kwa viongozi wa Dini wa dhehebu lake wakakataa kushiriki kwakuwa mwanakondoo hakuonekana zizini kwao Kwa muda mrefu au huenda hawakuwahi kumuona kabisa. Hivyo hawawezi kutoa huduma Kwa kondoo ambaye hawamfahamu.
Wanafamilia wakiwa katika taharuki ya majibu hayo toka kwenye mamlaka ya kidini wasijue nini cha kufanya, ndio Kaka mtu ambaye ni mlevi akasema isiwe tabu hata yeye anaweza kumwombea Sala ya maiti ndugu yake. Laa haula hapo ukatokea upinzani mkubwa Sana Kwa ndugu Yao Yule, wakamwambia tangia lini umeanza kuombea Sala ya mazishi, mlevi kama wewe utamwombeaje ndugu yako?
Kaka mtu akasisitiza kuwa hakuna Jambo la ajabu juu ya Hilo, bilashaka ulitaka kujua mwisho wake ilikuwaje, mnyetishaji wa habari ile naye hakuendelea kwani aliacha zogo bado linaendelea.
Baada ya story hii nikapatwa na tashuwishi na kujiuliza mambo kadhaa, je kama familia ingeamua kulikataa swala la Ulevi kama walivyokataa huyo mlevi kutoa sala ya mwisho ya maiti si wangeiokoa familia Ile na Ulevi?
Je, sala ya mwisho ina umuhimu gani na maana gani kama katika Maisha yako hapa duniani haukuishi katika misingi inayo mpendeza Mwenyezi Mungu?
Ewe mwanadamu tambua wewe ni mavumbi na hakika mavumbini utarejea.
Ni hayo tu!