Pale ambapo familia haikatai Ulevi bali inakataa sala ya mlevi!

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Ni hivi kwenye familia moja ya wagalatia huko mkoa X, kama unavyojua katika madhehebu fulani Fulani hivi usipo hudhuria ibada wakati wa Uhai wako basi wakati wa kifo chako nao hawahudhurii pia.

Basi Kaka mtu na mdogo wake wote ni walevi wa haja Tu,kama unavyojua kifo hakina taarifa mwisho wa siku kiumbe wa Mungu siku yake ikawadia na kurudisha namba Kwa mwenyewe.

Basi kwenda Kwa viongozi wa Dini wa dhehebu lake wakakataa kushiriki kwakuwa mwanakondoo hakuonekana zizini kwao Kwa muda mrefu au huenda hawakuwahi kumuona kabisa. Hivyo hawawezi kutoa huduma Kwa kondoo ambaye hawamfahamu.

Wanafamilia wakiwa katika taharuki ya majibu hayo toka kwenye mamlaka ya kidini wasijue nini cha kufanya, ndio Kaka mtu ambaye ni mlevi akasema isiwe tabu hata yeye anaweza kumwombea Sala ya maiti ndugu yake. Laa haula hapo ukatokea upinzani mkubwa Sana Kwa ndugu Yao Yule, wakamwambia tangia lini umeanza kuombea Sala ya mazishi, mlevi kama wewe utamwombeaje ndugu yako?

Kaka mtu akasisitiza kuwa hakuna Jambo la ajabu juu ya Hilo, bilashaka ulitaka kujua mwisho wake ilikuwaje, mnyetishaji wa habari ile naye hakuendelea kwani aliacha zogo bado linaendelea.

Baada ya story hii nikapatwa na tashuwishi na kujiuliza mambo kadhaa, je kama familia ingeamua kulikataa swala la Ulevi kama walivyokataa huyo mlevi kutoa sala ya mwisho ya maiti si wangeiokoa familia Ile na Ulevi?

Je, sala ya mwisho ina umuhimu gani na maana gani kama katika Maisha yako hapa duniani haukuishi katika misingi inayo mpendeza Mwenyezi Mungu?

Ewe mwanadamu tambua wewe ni mavumbi na hakika mavumbini utarejea.

Ni hayo tu!
 
Mnateseka sana na ukristo,christophobia itawamaliza.

Get a job dude.
Inahusiana nini na Ukristo na get a job dude!

Wakati mwingine ni Bora zaidi ukasoma post na kupita zako, mbona Mimi hufanya hivyo Sana Tu!
 
Inahusiana nini na Ukristo na get a job dude!

Wakati mwingine ni Bora zaidi ukasoma post na kupita zako,mbona Mimi hufanya hivyo Sana Tu!
Umeandika mambo ya uongo. Njoo utetee hoja yako useme ni imani ipi inatetea ulevi.

Nakusubiri.
 
Ebu niwasaidie kuelewa story naona wengi wetu huwa tunasoma kubishana na sio kuelewa ujumbe uliokusudiwa

Hapa kuna swala la familia kushindwa kuitengeneza familia ikawa katika maadili mema yanayo mpendeza Mwenyezi Mungu na badala yake hiyo hiyo familia inaona umuhimu wa ndugu Yao kuzikwa kimaadili ya Dini wakati huyo kijana wakati WA Uhai wake hakuishi katika misingi hiyo.

Je kwanini umuhimu huo hawaku uona mapema?

Swala la pili, ibada za mazishi huwa hazina mchango mkubwa WA kumuingiza peponi ikiwa huyo marehemu mwenyewe hakutengeneza mazingira hayo.

Kwa maana nyingine kuzika na hizo sala ni utaratibu Tu ambao ima ukifanyika au usipofanyika hauna impact yoyote kubwa katika safari ya mwisho ya marehemu.

Muwe mnasoma na kuelewa,matokeo yake tunachoshana Kwa comment ambazo hazina hata maana.
 
Mkuu hivi umeelewa story yenyewe Kwanza?
Sasa mkuu familia inakataa vipi ulevi? Au tunajuaje walishaonyana juu ya ulevi? Hapo issue ni marehemu mwenyewe maana watu wa hivyo tunao familia zote. Wewe kwenye ukoo wako wote ni washirika wazuri Kanisani?

Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Nakubaliana na wewe,huenda waliwaonya au laa! Wao ndio wanajua

Point yangu ni hivi,laiti nguvu iliyotumika kupinga mlevi kumsalia mwenzake Lau ingekuwa inatumika kuwarekebisha wanafamila basi naamini kama jamii tungefanikiwa Sana

Hiyo familia tumechukulia kama case study Tu!
 
Ebu niwasaidie kuelewa story naona wengi wetu huwa tunasoma kubishana na sio kuelewa ujumbe uliokusudiwa

Hapa kuna swala la familia kushindwa kuitengeneza familia ikawa katika maadili mema yanayo mpendeza Mwenyezi Mungu na badala yake hiyo hiyo familia inaona umuhimu wa ndugu Yao kuzikwa kimaadili ya Dini wakati huyo kijana wakati WA Uhai wake hakuishi katika misingi hiyo.

Je kwanini umuhimu huo hawaku uona mapema?

Swala la pili, ibada za mazishi huwa hazina mchango mkubwa WA kumuingiza peponi ikiwa huyo marehemu mwenyewe hakutengeneza mazingira hayo.

Kwa maana nyingine kuzika na hizo sala ni utaratibu Tu ambao ima ukifanyika au usipofanyika hauna impact yoyote kubwa katika safari ya mwisho ya marehemu.

Muwe mnasoma na kuelewa,matokeo yake tunachoshana Kwa comment ambazo hazina hata maana.
Mkuu umeelewaka ila naona unaionea tu familia labda kama hiyo familia inalalamika mtu wao kutozikwa kidini. Watu wa hivyo tunao wengi tu, wengine wakifa Kanisa linashiriki kwa heshima za wake zao tu.

Kama huna time na mambo ya dini na mwisho wako utakuwa jinsi hivyo hivyo. Mwanajeshi akifa katika maadili ya kijeshi atazikwa kijeshi, akikiuka miiko ya kijeshi anazikwa kiraia tu na hakuna kulalamika.
 
Mkuu umeelewaka ila naona unaionea tu familia labda kama hiyo familia inalalamika mtu wao kutozikwa kidini. Watu wa hivyo tunao wengi tu, wengine Kanisa linashiriki kwa heshima za wake zao tu.

Kama huna time na mambo ya dini na mwisho wako utakuwa jinsi hivyo hivyo. Mwanajeshi akifa katika maadili ya kijeshi atazikwa kijeshi, akikiuka miiko ya kijeshi anazikwa kiraia tu na hakuna kulalamika.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Tuko pamoja mkuu naona tumeelewana
 
Tuko pamoja mkuu naona tumeelewana
Nimekupata vizuri. Imani ni too personal, unakuta familia baba na mama ni wachungaji, lakini watoto wakikua wanaishi kipagani! Mimi hulaumu familia kwenye malezi ya watoto lakini kwenye utu uzima tunajua jema na baya! Hapo utabeba msalaba wako na wazazi wako au familia haitaulizwa mbinguni!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Nimekupata vizuri. Imani ni too personal, unakuta familia baba na mama ni wachungaji, lakini watoto wakikua wanaishi kipagani! Mimi hulaumu familia kwenye malezi ya watoto lakini kwenye utu uzima tunajua jema na baya! Hapo utabeba msalaba wako na wazazi wako au familia haitaulizwa mbinguni!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Kweli kabisa mkuu kama mazazi ukajitahidi vizuri kufanya wajibu wako WA kuwalea vijana kiimani na malezi mema kwakweli hata huko ukubwani wakikengeuka hata Kwa Mwenyezi Mungu hauna makosa kabisa,kwasababu hata yeye ameona juhudi yako na malezi yako.

Ndio maana hata kijana wa Nabii Nuhu pamoja na Baba yake kuwa Nabii lakini Kwa ukaidi wake akakataa kupanda jahazi na kufikri akipanda mlimani atakuwa salama,kwahiyo alikuwa responsible Kwa matendo yake.
 
Ni hivi kwenye familia moja ya wagalatia huko mkoa X, kama unavyojua katika madhehebu fulani Fulani hivi usipo hudhuria ibada wakati wa Uhai wako basi wakati wa kifo chako nao hawahudhurii pia.

Basi Kaka mtu na mdogo wake wote ni walevi wa haja Tu,kama unavyojua kifo hakina taarifa mwisho wa siku kiumbe wa Mungu siku yake ikawadia na kurudisha namba Kwa mwenyewe.

Basi kwenda Kwa viongozi wa Dini wa dhehebu lake wakakataa kushiriki kwakuwa mwanakondoo hakuonekana zizini kwao Kwa muda mrefu au huenda hawakuwahi kumuona kabisa. Hivyo hawawezi kutoa huduma Kwa kondoo ambaye hawamfahamu.

Wanafamilia wakiwa katika taharuki ya majibu hayo toka kwenye mamlaka ya kidini wasijue nini cha kufanya, ndio Kaka mtu ambaye ni mlevi akasema isiwe tabu hata yeye anaweza kumwombea Sala ya maiti ndugu yake. Laa haula hapo ukatokea upinzani mkubwa Sana Kwa ndugu Yao Yule, wakamwambia tangia lini umeanza kuombea Sala ya mazishi, mlevi kama wewe utamwombeaje ndugu yako?

Kaka mtu akasisitiza kuwa hakuna Jambo la ajabu juu ya Hilo, bilashaka ulitaka kujua mwisho wake ilikuwaje, mnyetishaji wa habari ile naye hakuendelea kwani aliacha zogo bado linaendelea.

Baada ya story hii nikapatwa na tashuwishi na kujiuliza mambo kadhaa, je kama familia ingeamua kulikataa swala la Ulevi kama walivyokataa huyo mlevi kutoa sala ya mwisho ya maiti si wangeiokoa familia Ile na Ulevi?

Je, sala ya mwisho ina umuhimu gani na maana gani kama katika Maisha yako hapa duniani haukuishi katika misingi inayo mpendeza Mwenyezi Mungu?

Ewe mwanadamu tambua wewe ni mavumbi na hakika mavumbini utarejea.

Ni hayo tu!
Mwandishi hujalewa kweli
 
Back
Top Bottom