Pale Bungeni simuoni Mbunge wa kuichambua ripoti ya CAG baada ya kukosekana Zitto Kabwe na wabunge wa CHADEMA

Pale Bungeni simuoni Mbunge wa kuichambua ripoti ya CAG baada ya kukosekana Zitto Kabwe na wabunge wa CHADEMA

Bajeti inakwenda kutekeleza ilani sasa ulitaka watukane au? Hizi stress za maisha na kukosa nafasi za uongozi katika chama na serikali zinatupeleka kubaya.
Hapa tunazungumzia ripoti ya CAG!

Mambo ya ilani watajadili Bawacha na UWT!
 
Hizi dharau ni kubwa sana na kulikosea heshima Bunge zima kuwa hakuna watu wenye weledi wa kuchambua mambo. ila sikushangai maana mmerithishwa na Mbelgiji mmoja ambaye anajiona katika nchii hii yeye ndo mtaalamu wa Sheria zote
Aliyeleta Thread ni MwanaCCM mwenye heshima zake sio kama wewe Chawa.
 
Hawa wametumia sehemu ya muda wao katika maisha yao kujielimisha ili kuwa uwezo wa kupambanua na kuchambua hoja,
Sasa Msukuma na Mwana FA wataleta stori za vijiweni kwenye bunge na hii ndio alikuwa jiwe anataka ili kuwatoa kwenye kuhoji vitu muhimu.
Msimponde Msukuma maana alipowaponda wasomi hamkumwambia siyo sawa. mliliridhika; na wasomi wanajiangusha wenyewe kwa kundekeza siasa na kutelekeza utaalamu wao.
Pia katiba iansema haya:
67 (1) (a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa

miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na

kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
Hao ndiyo wanatakiwa kuichambua ripoti na si hilo tu la kuchambua, kujadili bali pia na kupitisha sheria mbalimbali zinazoletwa bungeni (tena sheria nyingine ziko kwa kiingereza!)
 
Dr. Kimei umemfananisha na Msukuma etiii. Mtake radhi PHD kimei bingwa wa uchumi na maswala ya Fedha.
 
Tusitegemee bunge zuri awamu kama kila alye ndani Mle alikuwa yes boss!
Waliplan kutupiga pakubwa Hawa jamaa
Ukipanga na mungu anapanga
 
Tukiweka itikadi pembeni, kiukweli pale bungeni simuoni mtu mwenye uwezo wa kuichambua ripoti ya CAG kama walivyokuwa Zitto Kabwe, J J Mnyika, James Mbatia na Tundu Lissu.

Kuwa mwanasiasa mzuri ni jambo moja lakini kuwa mwanasiasa " mahiri" ni jambo lingine kabisa.

Hao niliowataja unapofika wakati wa uchambuzi wa maswala ya kitaalamu iwe uchumi, sheria au fedha huwa na udadisi wa kitaaluma siyo kishabiki.

Ripoti ya CAG iliyowasilishwa kwa mh Rais Samia leo inahitaji hoja nyingi za kibobezi/ kidadisi lakini sidhani kama akina Babu Tale na Nusrat Henje wana viwango hivyo.

Itoshe tu kusema wabunge wengi wa sasa wana uwezo mdogo na ujasiri hafifu wa kujenga hoja.
Marehemu Jiwe alijua umahiri wa Wabunge wa Upinzani katika kudadavua reports za CAG na michango yao kwa Bajeti za Serikali ndo maana aliamua kuwadhibiti Wabunge hao kiaina aina......!!!
Ni aibu sana kwa utawala huu USIOTAKA KUKOSOLEWA ambao umemalizika 26.03.21!! God bless Tanzania,!!!
 
Back
Top Bottom