Pale dunia inapofumbwa kwa yale yanotokea nchini Sudan

Point !! Alaumiwe Bashir ,aliyeunda dubwana na kulipa nguvu ,leo linawatesa wa sudani ,na Hilo kundi litaleta gasia hasa ,hapo watauwana mpaka Basi.
 
Ndugu samahan naomba uweke sawa jambo moja,wakat w mapinduz ya sudani n jesh l selikali ndo lilifanya mapinduz au hawa rfs,au wote waliunga mkono mapinduz piya naomba unisaidie kuna ile selikali ya kiraia iliumdwa baada y mapinduzi lakin haikudumu ikapinduliwa nawasilisha mkuu
 
Hapana jamaa kaeleza vizur sana kwanza kazungumzia internal facts alafu akaja ushawishi wa nje ambao umechochea vurugu piya,kimsingi vurugu zote zinazotokea nchi nyingi dunian kuanzia arabun mpaka africa yanakua n matokeo ya makabiliano y madola makubwa
 
Jenerali Dagalo atokea Sudan ya Kusini ambayo ilipata uhuru wake mwaka 2011 baada ya mapigano ya muda mrefu kati ya wapiganaji wa SPLA/M na majeshi ya serikali ya Khartoum.
Dagalo anatokea Darfur ambalo ni Jimbo huko magharibi mwa Sudan kaskazini linalopakana na Chad na liliokumbwa na Vita kati ya serikali na makundi ya waasi tangu mwaka 2003.
 
Asante kwa makala nzuri.
 
Ndugu, Sudan ilitawaliwa na sheria za jamhuri ya kiislam yaani kama vile Iran hivyo Al Bashir alikuwa ni kiongozi wa taifa la kiislam.

Mwaka 2019 makamu wake Ahmed Awad Ibn Anuf akishirikiana na jenerali Burhan wakampindua Al bashir na wakaunda serikali ya mpito ya kijeshi. Hivyo Sudan imekuwa chini ya baraza la kijeshi (Military Council) tangu 2019.

Kwa maana hiyo kama kawaida ya jeshi likichukua nchi hakuna bunge, wala serikali na kila kitu ni chini ya baraza la kijeshi.

Baadae mwaka huohuo wa 2019 baraza la kijeshi likakubaliana na viongozi wa kiraia walotaka serikali ya kiraia chini ya waziri mkuu na ndo bwana Abdallah Hamdok akawa waziri mkuu lakini wakati huo Sudan ilikuwa imefukuzwa uanachama wa Umoja wa Afrika (mwezi June 2019)

Nikirudi kwenye suali lako kwamba RSF waliunga mkono mapinduzi ya kumuondoa Al Bashir na Hamdok kwani lilipoundwa baraza la kijeshi jenerali Burhan akawa mwenyekiti wa baraza na jenerali Dagalo akawa makamu wake hivyo kuanzisha mchakato wa kuwaingiza jeshini wanamgambo wa RFS.

Kwahiyo hawa majenerali ndo walimwondoa Al Bashir mwaka 2019 na pia ndo walimwondoa waziri mkuu wa kiraia bwana Hamdok mwaka 2021. Hamdok hakukaa sana madarakani kwani kulikuwepo maandamano ya kulishikinikiza baraza la kijeshi kumuondoa Hamdok.

Kwahiyo ni kama nilivyosema katika mada yangu kwamba Sudan ndnai kuna vita inohusu makundi zaidi ya mawili yaani kundi la kijeshi kwa maana ya lilochini ya jenerali Burhan, RSF lilo chini ya jenerali Dagalo na kundi kubwa la watu mchanganyiko akiwemo Abdallah Hamdok ambalo ndo lenye kushikiniza kuwepo serikali ya kiraia, kundi la ambao bado wanaomuunga Al Bashir pamoja na baadhi ya wanajeshi na makundi mengine ya ndani na nje ya Sudan.

Tatizo la Hamdok ni kwamba aonekana ni mtu wa nje kwani amefanya kazi IMF na ni mchumi kitaaluma. Pia IMF na WB waliamua kumpatia fedha ili alete mabadiliko ya kiuchumi ambayo yalianza kusababisha vyuma kubana na wananchi wakaamua huyu hafai.

Kwa kifupi tatizo la Sudan ambayo ni nchi ya tatu kwa ukubwa barani Afrika ni kama la Libya chini ya Muamar Gaddafi.

Yaani kwa maana kwamba akiondolewa kiongozi kama huyu huacha mizizi na pia kumuondoa kwa nguvu huleta vita vya wenyewe kwa wenyewe au kusababisha nchi isitawalike.

Nafikiri nimekujibu.
 
ww ni mpumbavu hata ujui unacho kiongolea, kaa pembeni mrusi uache wenye akili wachambue hili ok
Kutukana umeenda mbali sana halafu mimi si mrusi ila nimefika Moscow wakti wa kombe la dunia.

Jitahidi uondoe hasira maana ukiwa nazo huondoa furaha moyoni na huleta HBP.
 

Andiko maridhawa, lakini lenye mapungufu kidogo ya kisarufi:
1. Adhira[emoji735], Hadhira[emoji3514]
2. Ujaongelea[emoji735], Hujaongelea[emoji3514]
3. Kweri kweri[emoji735], Kweli kweli[emoji3514]
4. Let the caged bird sings[emoji735], Let the caged bird sing[emoji3514] (Kama statement ingekuwa the caged bird sings, ulikuwa sahihi maana inakuwa third person singular na verb sing inakuwa sings, lakini ulipoweka neno let inakuwa siyo sahihi kuweka suffix S kwenye verb sing).
 
Kwingine utakuwa SAWA, ila kwenye KWERI KWERI nimeandika kwa kummrejea kiongozi wa malaika.
KWERI KWERI!! AU NASEMA UWONGO NDUGU ZANGU?.🤣🤣
 
Dagalo anatokea Darfur ambalo ni Jimbo huko magharibi mwa Sudan kaskazini linalopakana na Chad na liliokumbwa na Vita kati ya serikali na makundi ya waasi tangu mwaka 2003.
Jamaa ni tajiri mkubwa na aogopewa sana hata na wale wa nje ya Sudan.

Ana connections UAE, Moscow , Saudi Arabia, na yeye sasa hivi kalenga Khartoum.

Jenerali Burhan ana kazi kubwa na kumdhibiti jenerali Dagalo.

Kumbuka jenerali Dagalo ni kijana mdogo sana yasemwa kazaliwa 1974 au 1975 hakuna taarifa rasmi ya mwaka halisi.
 
Huu mzimu ulitengenezwa na Bashir mwaka 2013 baada ya kazi chafu alizofanya huko Darfur kupitia wanamgambo wa kiarabu (Janjaweed) na ukaletwa Khartoum ili ilinde utawala wa yule dikteta, sasa umegeuka jinamizi kwa Sudan.

Majenerali wote wawili Burhan na Dagalo walihusika na Vita vya Darfur hivyo hakuna mwema hapo.
 
Wote Burhan, Dagalo, Ibn Ouf na Al Bashir wote ni wahalifu wa kivita.

Hawa waogopa sana ikija serikali ya kiraia kwani itabidi wote wakamatwe na hilo ni jambo ambalo halitawezekana kwani serikali ikijaribu hilo itapunduliwa.

Ni jeshi ndilo limemwokoa Al Bashiri kutoka gerezani na kumhamishia sehemu ingine.

Jeshi laona ni lazima wamlinde.
 
Asante sana ndugu nimekupata vizur
 
Kwa jinsi ulivyo andika hapa it shows you know nothing about MKIRU militias and what kind of fire arms they possessed that time. Hapa naandika nikiwa maeneo ambayo baadhi yao walikuwa wametokea na walikuja kufurumushwa na vyombo vetu vya ulinzi na usalama.
Na kwa hakika hujui PSY-OPS na watu wa magharibi wanazitumiaje kuchochea vurugu kama za Libya, Sudan , Syria na Misri. Wewe ni victim tu wa MSM zenye kulenga kuimarisha western hegemony.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…