Pale dunia inapofumbwa kwa yale yanotokea nchini Sudan

Pale dunia inapofumbwa kwa yale yanotokea nchini Sudan

Misri inasambaza silaha kwa jeshi wakati Urus inawapa silaha rapidly response squad.
I don't know how some qullible people are accusing the US in fact Us inafanya kazi kubwa ya kuziunganisha pande zinazohasimiana.

Bashir katika utawala wake alihisi uenda jeshi likaja kumpindua, akaamua kuunda kikosi(RPS) na kukipa nguvu Sawa na jeshi.

Leo bashar hayupo jeshi limeamua kuita kiongozi wa RPS ili waunde jeshi moja as nchi haiwezi kuwa na majeshi mawili but wameshindwa kukubaliana kwenye mgawanyo wa madaraka ndiyo vita imeibuka.
RPS anasema ni wakati wake wa kuongoza, jeshi nalo linatoa misimamo ile ile.
Sasa sijui habari za fulani walikutana na fulani zinatoka wapi.. Ikiwa insu ni kukutana Putin hajawai kutana na viongozi wa Us?.
SAMIA hakutani na viongozi wa Us? why msudani iwe hoja?
Wakati vita ya Ethiopia inapigana kuna wapumbavu wachambuzi wakawa wanaandika humu kuwa wanapiganishwa na US kwasababu tu wamejenga bwawa la umeme kitu ambacho US hai
halendi.
Yaani bwawa lenye thamani na ndege moja ya F15 moja ndiyo marekani ipate wivu!!
Bure kabisa
Point !! Alaumiwe Bashir ,aliyeunda dubwana na kulipa nguvu ,leo linawatesa wa sudani ,na Hilo kundi litaleta gasia hasa ,hapo watauwana mpaka Basi.
 
Jifunze kusoma uzuri mada kabla hujaunda hoja yako.

Nimeeleza masuala mengi tu na sijailaumu US kama unavyodai.

Nimegusia kwa kifupi historia ya Sudan , sababu mbalimbali zinoweza kuwa kichocheo cha mgogoro wa sasa ikiwemo sababu ya kugombea madakara baina ya majenerali wawili kutoaminiana na pia msukumo kutoka nje ya Sudan ambayo nayo yaweza kuwa kichocheo cha mgogoro huo.

NImeongelea kuibuka kwa wakimbizi na watoto wa kivita ambao sasa hivi wazagaa mitaani wakiua watu na kupora mali, hizo zote zikiwa ni athari za vita.

Sasa weye waleta mara US, mara wamtaja raisi Samia, mara Ethiopia mara ndege ya F15!

Soma mada uielewe na kisha jenga hoja usiangalie tu US kasemwa vipi.
Ndugu samahan naomba uweke sawa jambo moja,wakat w mapinduz ya sudani n jesh l selikali ndo lilifanya mapinduz au hawa rfs,au wote waliunga mkono mapinduz piya naomba unisaidie kuna ile selikali ya kiraia iliumdwa baada y mapinduzi lakin haikudumu ikapinduliwa nawasilisha mkuu
 
Umeleta mada na kuielezea ktk mazingira ambayo mada ni kubwa kuliko upeo wako wa kufikiri na kuchambua.

Ungekuwa na akili timamu, kama ungemuelewa jamaa hapo. Masuala ya US na Russia yalikuwa hayana ata chembe 1% ktk hiyo mizozo ya Sudan. Ila kwa kuwa akili ipo chini ukashindwa kupanua wigo wa akili.
Hapana jamaa kaeleza vizur sana kwanza kazungumzia internal facts alafu akaja ushawishi wa nje ambao umechochea vurugu piya,kimsingi vurugu zote zinazotokea nchi nyingi dunian kuanzia arabun mpaka africa yanakua n matokeo ya makabiliano y madola makubwa
 
Jenerali Dagalo atokea Sudan ya Kusini ambayo ilipata uhuru wake mwaka 2011 baada ya mapigano ya muda mrefu kati ya wapiganaji wa SPLA/M na majeshi ya serikali ya Khartoum.
Dagalo anatokea Darfur ambalo ni Jimbo huko magharibi mwa Sudan kaskazini linalopakana na Chad na liliokumbwa na Vita kati ya serikali na makundi ya waasi tangu mwaka 2003.
 
Kama ilivyotuathiri vita vya Darfur

Wanajeshi saba wa Tanzania waliokufa Darfur waagwa rasmi.​

22 Julai, 2013

Wanajeshi wa Tanzania waliouwawa Darfur
 
Mgogoro na vita baina ya Jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF umeingia siku ya 10 huku kukiwepo na amri ya kusimamishwa mapigano kwa masaa 72.

Amri ya kusimamisha mapigano kuruhusu uokozi wa raia wa kigeni ilianza kutokea siku ya Ijumaa iliyopita ambapo watu waliruhuswa kusheherekea siku kuu ya Iddi. Lakini baadae Jumapili mapigano yakaendelea tena. Juzi kati jeshi la wanamgambo hao wa RSF wakakubali maombi ya mataifa ya kigeni kufanya uokozi wa raia wake.

Mpaka sasa nchi za Misri, Saudi Arabia, Iran, Syria, Ukraine, Hispania, Italia, Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Marekani na zingine, zimetuma ndege za kijeshi na wanajeshi maalum kufanya shughuli za uokoaji wa raia wake. Djibouti ndo pamekuwa kituo cha kufikia wageni mbalimbali kabla kusafirishwa kwenda nchi zingine.

Watu wapatao 27,000 raia wa Sudan tayari wamekimbilia nchi jirani za Mali, Chad na Misri kwa njia ya barabara ambapo magari na mabasi yamekuwa yakibeba watu kupeleka katika nchi hizo na kuwa wakimbizi. Shirika la UNHCR ambalo lina kambi nchini Chad limekuwa likiendelea kupokea wakimbizi hao ambao idadi yao huenda ikaongezeka na kuzidi 100,000.

Uingereza ambayo imekuwa nyuma ya juhudi za uokozi wa raia wake, leo imenza rasmi zoezi hilo kwa kuwaelekeza raia wake kwenda katika kituo cha kijeshi cha Weid Seidna kilichopo kakazini mwa mji mkuu wa Khartoum. Uingereza imetuma kikosi cha jeshi lake la Raf kutokea kwenye kambi yake ya kijeshi iliyopo nchini Cyprus iitwayo Akrotiri.

Lakini serikali ya Uingereza imesisitiza kuwa ni raia wenye kubeba pasi za kusafiria za nchi hiyo na familia zao tu ndo watoruhusiwa kupanda ndege hizo kuokolewa na si raia wengine ambao ni wakazi wa namna yoyote ile nchini Uingereza kwa mujibu wa serikali ya Uingereza raia wapatao 1,000 tayari walikuwa wamewasiliana na wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo.

Ujerumani imetuma ndege sita za uokozi na kuokoa raia wapatao 500, Italia raia 400, Ukraine raia 138, Marekani zaidi ya raia 3000, India 3000, na raia wengine wametumia bandari ya Sudan au Port Sudani kuvuka kwa meli kwenda nchi za Yemen na Saudi Arabia.

Lakini mapigano hayo yakiwa yaendelea khasa katikati ya Khartoum, tayari kuna taarifa za kutekwa kwa maabara ya taifa ambayo imehifadhi sampuli na dawa za chanjo za magonjwa mbalimbali kama malaria na kipindupindu. Pia kuna taarifa za kuwepo kwa watoto wadogo wabebao silaha aina za AK 47 (watoto wa vita ) au Child Soldiers ambao wamekuwa wakiranda mitaani kutafuta chakula na kuanza kupora katika maduka, majengo na majumbaya watu khasa wale raia wa kigeni wanokimbia.

Watoto hawa ambao wana umri kati ya miaka 13 na 14 ni watoto hatari sana ambao wanapigana upande wa vikosi vya RSF. Kwa kawaida jeshi huwa na komandi moja ambayo hutoa amri wakti vita iikiendelea na hivyo kuwepo nidhamu baina ya wanajeshi. Kwa upande wa wapiganaji wa RSF hali ni tofauti kwani kila mpiganaji ana maamuzi yake na anachokikuta mbele yake huwa na halali kwake na hali hiyo ndo ilopelekea nchi nyingi kutuma vikosi vya jeshi kusaidia uokozi maana tayari kuna taarifa ya kushambuliwa kwa vikosi vy uokoaji.

Lakini yote haya yameanzaje na nini ni chanzo na pengine mwisho wake utakuwaje?

Mazingira khasa ya kuibuka kwa mapagano yaelezwa tofauti na vyombo vingi vya habari vikisema kuwa ni mvutano baina ya majenerali wawili Abdel Fattah-al Burhan na Dagalo au kama alijulikanavyo kama Hemedti. Taarifa zingine zadai kuwa majenerali Al Burhan na Dagalo ni majasusi wa nchi za magharibi na Russia. Zipo taarifa kadha wa kadha kuhusu majenerali hawa na ziara zao nchini Marekani na kule Kremlin.

Jenerali Al Burhan amekuwa akifanya ziara nyingi jijini Washington na ipo ziara ambayo alikutana na waziri wa nchi wa Marekani bwana Pompei mwaka 2020 na waziri wa ujasusi wa Israeli Eli Cohen mwaka 2022.

Lakini kinotokea sasa nchini humo ni kugombania madaraka au "power struggle" ambapo kila upande unashutumu mwenzie kutaka kupindua. Kwa muda mrefu tangia wanamgambo wa RSF ambao kiini chake ni wagamgambo wa Janjaweed washirikiane na jeshi kuongoza Sudan, bado uhusiano baina ya majenerali Burhan na Dagalo umekuwa ni wa kutiliana mashaka.

Jenerali Dagalo atokea Sudan ya Kusini ambayo ilipata uhuru wake mwaka 2011 baada ya mapigano ya muda mrefu kati ya wapiganaji wa SPLA/M na majeshi ya serikali ya Khartoum. Sudan ilitawaliwa na Uingereza na katika utawala wake Uingereza iliigawa Sudan katika maeneo mawili ya Kaskazini kwenye waarabu ambako walijenga mashule, mahospitali na miundombinu mingine kama barabara , madaraja na huduma zingine za msingi kama makanisa na misikiti.

Lakini wakoloni hao wa Uingereza walisahau kabisa Sudan ya Kusini ambayo ina waafrika weusi na kuiacha kama ilivyo huku mji yake mkubwa ya Juba ukiwa ndani ya vumbi la jangwa. Hali hiyo ilifanya Sudan Kusini kuendesha kampeni ya vita na serikali ya Khartoum ambayo iliendelea kuwaadhibu wasudani weusi na baadae kuwapelekea kundi la Janjaweed ili kumaliza tatizo la wahamiaji waloitwa haramu ambao walikuwa wakitafuta maisha bira kutoka kaskazini.

Tangu ipate uhuru mwaka 2011 na kujiunga na umoja wa Afrika kuwa nchi ya 54 barani humo, Sudan ya Kusini ni nchi huru na inojitegemea. Sudan ya Kusini ina majimbo 10 ambayo wananchi wake wamekuwa kila mara walipigana kwa kuona hakuna maendeleo ya haraka yanofanywa na serikali ya Sudan ya Kusini.

Lakini ni kitendo cha jenerali Burhan kukubali kuwaleta Khartoum wanamgambo wa RSF kusaidia shughuli mbalimbali za kijeshi na pia kuanza mazungumzo ya kuwarasimisha wanamgambo hao wa RSF kuwa sehemu ya jeshi la Sudan ndicho kilicholeta zogo na vurugu na sasa mapigano makali.

Lakini wadadisi na wachambuzi wengi wanaamini kuwa mapigano ya sasa kati ya majenerali hao wawili Burhan na Dagalo yametokana na majenerali hao (Jenerali Burhan) kuunga mkono nchi za Marekani na NATO ambazo bado zasaidia nchi ya Ukraine ambayo iko kwenye vita na Russia, na Jenerali Dagalo kuwa upande wa Russia ambayo ina vikosi vyake Sudan ya Kusini.

Al Burhani pia asaidiwa na Misri kwa misaada ya vifaa vya kijeshi kutoka kwa raisi Abdel Fattah El- Sisi. Jenerali Dagalo ambae ni tajiri mkubwa wa dhahbu kutoka Sudan ya Kusini anasaidiwa pia na nchi za Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu UAE ambako amewahi kupeleka vikosi vya RSF kusaidia vita vya Yemen.

Kiasi kikubwa cha dhahabu inochimbwa Sudan ya Kusini yapelekwa nchini Russia kupitia UAE na vikosi vya jeshi la kukodi la Wagner vya Russia vipo Sudani Kusini vikilinda migodi ya dhahabu na visima vya mafuta. Russia imekuwa katika mazungumzo na jenerali Dagalo kuhusu kutaka kujenga kituo cha kijeshi katika bandari ya Sudan au Port Sudani kwenye bahari nyekundu.

Itakumbukwa baada ya Russia kuanzisha operesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine umoja wa mataifa uliweka azimio la kulaumu kitendo hicho cha Russia lakini Sudan haikushiriki kupiga kura kuunga mkono azimio hilo. Tangu wakati huo Marekani na washirika wake wamekuwa wakihangaka kuhaikisha Sudani inapata shida kwanza kwa kuondoa misaada ya fedha kutoka IMF na Benki ya Dunia, kuharibu mahusiano ya Sudan na Iran ambayo yaiuzia Sudan vifaa vya kijeshi, Russia na China.

Pia Marekani yaitaka Sudan kufunga mazungumzo na mijadala ya Russia kuweka kituo cha jeshi la majini kwenye bandari ya Sudan, kuimarisha uhasama na Iran na kuharibu uhusiano wa kijeshi kati ya Sudan na Iran na Russia na kuchagiza machakato wa kurudisha serikali ya kiraia chini ya waziri mkuu Abdallah Hamdok ambayo itapunguza usafirishaji wa dhahabu kwenda Russia ambapo yaaminika jambo hilo laisaidia sana Russia kukwepa vikwazo vya kiuchumi vilowekwa na Marekani na washirika wake.

Marekani imekuwa yaishutumu Russia kuwa nyuma ya mapinduzi yalomwondoa madarakani bwana Hamdok ambae kitaaluma ni mchumi na amesoma nchini Uingereza.

Mgogoro wa sasa zaidi umechochewa na majenerali hao wawili Burhan na Dagalo kutokukubaliana kwenye suala la kugawana madaraka na kwa vikosi vya RSF kuingizwa rasmi kwenye jeshi la Sudan. Jenerali Burhan binafsi hakubalini na suala hili lakini baadhi ya wanajeshi ndani ya jeshi wanaamini kuwa kuwaingiza RSF ndani ya jeshi kutapunguza na kuondoa hasira ya vijana wa RSF na pia maandamano yasokwisha mitaani kutoka kwa wananchi ambao wengi hawaungi mkono suala la RSF kuingizwa jeshini.

Jenerali Dagalo hakubaliani na suala la vikosi vya RSF kuingizwa jeshini hadi hapo serikali ya kiraia itapokuwa madarakani na pia anadai kuondolewa kwenye nafasi za kuu za serikali kwa wale viongozi wote wenye ukaribu na aliekuwa raisi Al Bashir ambae alipinduliwa mwaka 2019. Msimamo huu umemfanya jenerali dagalo kuungwa mkono na watu wengi wakiwemo wasomi vikundi mbalimbali vya kijamii ambavyo vimekuwemo katika mazungumzo ya kurudisha serikali ya ya kiraia.

Jumuiya ya kimataifa imekuwa ikionyesha wasiwasi wa kuwaingiza RSF jeshini na imekuwa ikisisitiza kuharakisha harakati za kuirudisha serikali ya kiraia chini ya Hamdok ambayo majenerali Burhan na Dagalo nao wana wasiwasi wa kukamatawa na kuwekwa jela kwa makosa mbalimbali ya uhalifu wa kivita.

Hadi sasa hakuna anaefahamu mgogoro huu utaisha vipi khasa baada ya jenerali Dagalo na vikosi vyake kuahidi kuendeleza mapigano. Hii ni aina ingine ya mifano hai kuwa bara la Afrika kwa sasa lipo katika kugombaniwa na mataifa makubwa. Sudan ya Kusini ina asilimia 75 ya utajiri wa maliasili ya visima vya mafuta, pia Sudan kaskazini ina dhahabu pamoja na madini mengine mbalimbali.

Hakika yanotokea Sudan yatupa funzo kubwa sana sisi waafrika na mstakabali wetu hapa duniani maana waafrika wenye ngozi nyeusi wamekalia maliasili yenye thamani ya mamilioni ya dola lakini ni raia kutoka nchi zingine ambao ndo wenye uwezo wa kuamua hatima ya mwafrika mweusi.
Asante kwa makala nzuri.
 
Ndugu samahan naomba uweke sawa jambo moja,wakat w mapinduz ya sudani n jesh l selikali ndo lilifanya mapinduz au hawa rfs,au wote waliunga mkono mapinduz piya naomba unisaidie kuna ile selikali ya kiraia iliumdwa baada y mapinduzi lakin haikudumu ikapinduliwa nawasilisha mkuu
Ndugu, Sudan ilitawaliwa na sheria za jamhuri ya kiislam yaani kama vile Iran hivyo Al Bashir alikuwa ni kiongozi wa taifa la kiislam.

Mwaka 2019 makamu wake Ahmed Awad Ibn Anuf akishirikiana na jenerali Burhan wakampindua Al bashir na wakaunda serikali ya mpito ya kijeshi. Hivyo Sudan imekuwa chini ya baraza la kijeshi (Military Council) tangu 2019.

Kwa maana hiyo kama kawaida ya jeshi likichukua nchi hakuna bunge, wala serikali na kila kitu ni chini ya baraza la kijeshi.

Baadae mwaka huohuo wa 2019 baraza la kijeshi likakubaliana na viongozi wa kiraia walotaka serikali ya kiraia chini ya waziri mkuu na ndo bwana Abdallah Hamdok akawa waziri mkuu lakini wakati huo Sudan ilikuwa imefukuzwa uanachama wa Umoja wa Afrika (mwezi June 2019)

Nikirudi kwenye suali lako kwamba RSF waliunga mkono mapinduzi ya kumuondoa Al Bashir na Hamdok kwani lilipoundwa baraza la kijeshi jenerali Burhan akawa mwenyekiti wa baraza na jenerali Dagalo akawa makamu wake hivyo kuanzisha mchakato wa kuwaingiza jeshini wanamgambo wa RFS.

Kwahiyo hawa majenerali ndo walimwondoa Al Bashir mwaka 2019 na pia ndo walimwondoa waziri mkuu wa kiraia bwana Hamdok mwaka 2021. Hamdok hakukaa sana madarakani kwani kulikuwepo maandamano ya kulishikinikiza baraza la kijeshi kumuondoa Hamdok.

Kwahiyo ni kama nilivyosema katika mada yangu kwamba Sudan ndnai kuna vita inohusu makundi zaidi ya mawili yaani kundi la kijeshi kwa maana ya lilochini ya jenerali Burhan, RSF lilo chini ya jenerali Dagalo na kundi kubwa la watu mchanganyiko akiwemo Abdallah Hamdok ambalo ndo lenye kushikiniza kuwepo serikali ya kiraia, kundi la ambao bado wanaomuunga Al Bashir pamoja na baadhi ya wanajeshi na makundi mengine ya ndani na nje ya Sudan.

Tatizo la Hamdok ni kwamba aonekana ni mtu wa nje kwani amefanya kazi IMF na ni mchumi kitaaluma. Pia IMF na WB waliamua kumpatia fedha ili alete mabadiliko ya kiuchumi ambayo yalianza kusababisha vyuma kubana na wananchi wakaamua huyu hafai.

Kwa kifupi tatizo la Sudan ambayo ni nchi ya tatu kwa ukubwa barani Afrika ni kama la Libya chini ya Muamar Gaddafi.

Yaani kwa maana kwamba akiondolewa kiongozi kama huyu huacha mizizi na pia kumuondoa kwa nguvu huleta vita vya wenyewe kwa wenyewe au kusababisha nchi isitawalike.

Nafikiri nimekujibu.
 
ww ni mpumbavu hata ujui unacho kiongolea, kaa pembeni mrusi uache wenye akili wachambue hili ok
Kutukana umeenda mbali sana halafu mimi si mrusi ila nimefika Moscow wakti wa kombe la dunia.

Jitahidi uondoe hasira maana ukiwa nazo huondoa furaha moyoni na huleta HBP.
 
Misri inasambaza silaha kwa jeshi wakati Urus inawapa silaha rapidly response squad.
I don't know how some qullible people are accusing the US in fact Us inafanya kazi kubwa ya kuziunganisha pande zinazohasimiana.

Bashir katika utawala wake alihisi uenda jeshi likaja kumpindua, akaamua kuunda kikosi(RPS) na kukipa nguvu Sawa na jeshi.

Leo bashar hayupo jeshi limeamua kuita kiongozi wa RPS ili waunde jeshi moja as nchi haiwezi kuwa na majeshi mawili but wameshindwa kukubaliana kwenye mgawanyo wa madaraka ndiyo vita imeibuka.
RPS anasema ni wakati wake wa kuongoza, jeshi nalo linatoa misimamo ile ile.
Sasa sijui habari za fulani walikutana na fulani zinatoka wapi.. Ikiwa insu ni kukutana Putin hajawai kutana na viongozi wa Us?.
SAMIA hakutani na viongozi wa Us? why msudani iwe hoja?
Wakati vita ya Ethiopia inapigana kuna wapumbavu wachambuzi wakawa wanaandika humu kuwa wanapiganishwa na US kwasababu tu wamejenga bwawa la umeme kitu ambacho US hai
halendi.
Yaani bwawa lenye thamani na ndege moja ya F15 moja ndiyo marekani ipate wivu!!
Bure kabisa

Andiko maridhawa, lakini lenye mapungufu kidogo ya kisarufi:
1. Adhira[emoji735], Hadhira[emoji3514]
2. Ujaongelea[emoji735], Hujaongelea[emoji3514]
3. Kweri kweri[emoji735], Kweli kweli[emoji3514]
4. Let the caged bird sings[emoji735], Let the caged bird sing[emoji3514] (Kama statement ingekuwa the caged bird sings, ulikuwa sahihi maana inakuwa third person singular na verb sing inakuwa sings, lakini ulipoweka neno let inakuwa siyo sahihi kuweka suffix S kwenye verb sing).
 
Kwingine utakuwa SAWA, ila kwenye KWERI KWERI nimeandika kwa kummrejea kiongozi wa malaika.
KWERI KWERI!! AU NASEMA UWONGO NDUGU ZANGU?.🤣🤣
 
Dagalo anatokea Darfur ambalo ni Jimbo huko magharibi mwa Sudan kaskazini linalopakana na Chad na liliokumbwa na Vita kati ya serikali na makundi ya waasi tangu mwaka 2003.
Jamaa ni tajiri mkubwa na aogopewa sana hata na wale wa nje ya Sudan.

Ana connections UAE, Moscow , Saudi Arabia, na yeye sasa hivi kalenga Khartoum.

Jenerali Burhan ana kazi kubwa na kumdhibiti jenerali Dagalo.

Kumbuka jenerali Dagalo ni kijana mdogo sana yasemwa kazaliwa 1974 au 1975 hakuna taarifa rasmi ya mwaka halisi.
 
Huu mzimu ulitengenezwa na Bashir mwaka 2013 baada ya kazi chafu alizofanya huko Darfur kupitia wanamgambo wa kiarabu (Janjaweed) na ukaletwa Khartoum ili ilinde utawala wa yule dikteta, sasa umegeuka jinamizi kwa Sudan.

Majenerali wote wawili Burhan na Dagalo walihusika na Vita vya Darfur hivyo hakuna mwema hapo.
 
Wote Burhan, Dagalo, Ibn Ouf na Al Bashir wote ni wahalifu wa kivita.

Hawa waogopa sana ikija serikali ya kiraia kwani itabidi wote wakamatwe na hilo ni jambo ambalo halitawezekana kwani serikali ikijaribu hilo itapunduliwa.

Ni jeshi ndilo limemwokoa Al Bashiri kutoka gerezani na kumhamishia sehemu ingine.

Jeshi laona ni lazima wamlinde.
 
Ndugu, Sudan ilitawaliwa na sheria za jamhuri ya kiislam yaani kama vile Iran hivyo Al Bashir alikuwa ni kiongozi wa taifa la kiislam.

Mwaka 2019 makamu wake Ahmed Awad Ibn Anuf akishirikiana na jenerali Burhan wakampindua Al bashir na wakaunda serikali ya mpito ya kijeshi. Hivyo Sudan imekuwa chini ya baraza la kijeshi (Military Council) tangu 2019.

Kwa maana hiyo kama kawaida ya jeshi likichukua nchi hakuna bunge, wala serikali na kila kitu ni chini ya baraza la kijeshi.

Baadae mwaka huohuo wa 2019 baraza la kijeshi likakubaliana na viongozi wa kiraia walotaka serikali ya kiraia chini ya waziri mkuu na ndo bwana Abdallah Hamdok akawa waziri mkuu lakini wakati huo Sudan ilikuwa imefukuzwa uanachama wa Umoja wa Afrika (mwezi June 2019)

Nikirudi kwenye suali lako kwamba RSF waliunga mkono mapinduzi ya kumuondoa Al bashir na Hamdok kwani lilipoundwa baraza la kijeshi jenerali Burhan akawa mwenyekiti wa baraza na jenerali Dagalo akawa makamu wake hivyo kuanzisha mchakato wa kuwaingiza jeshini wanamgambo wa RFS.

Kwahiyo hawa majenerali ndo walimwondoa Al Bashir mwaka 2019 na pia ndo walimwondoa waziri mkuu wa kiraia bwana Hamdok mwaka 2021. Hamdok hakukaa sana madarakani kwai kulikuwepo maandamano ya kulishikinikiza baraza la kijeshi kumuondoa Hamdok.

Kwahiyo ni kama nilivyosema katika mada yangu kwamba Sudan ndnai kuna vita inohusu makundi zaidi ya mawili yaani kundi la kijeshi kwa maana ya lilochini ya jenerali Burhan, RSF lilo chini ya jenerali Dagalo na kundi kubwa la watu mchanganyiko akiwemo Abdallah Hamdok ambalo ndo lenye kushikiniza kuwepo serikali ya kiraia, kundi la ambao bado wanaomuunga Al Bashir pamoja na baadhi ya wanajeshi na makundi mengine ya ndani na nje ya Sudan.

Tatizo la Hamdok ni kwamba aonekana ni mtu wa nje kwani amefanya kazi IMF na ni mchumi kitaaluma. Pia IMF na WB waliamua kumpatia fedha ili alete mabadiliko ya kiuchumi ambayo yalianza kusababisha vyuma kubana na wananchi wakaamua huyu hafai.

Kwa kifupi tatizo la Sudan ambayo ni nchi ya tatu kwa ukubwa barani Afrika ni kama la Libya chini ya Muamar Gaddafi.

Yaani kwa maana kwamba akiondolewa kiongozi kama huyu huacha mizizi na pia kumuondoa kwa nguvu huleta vita vya wenyewe kwa wenyewe au kusababisha nchi isitawalike.

Nafikiri nimekujibu.
Asante sana ndugu nimekupata vizur
 
Wakati wa wale wahuni Amboni na Mukuranga kuna watu (magreat thinker wa Jf) wakawa wanaasema wanafadhiliwa na marekani.. et kwasababu kuna mikataba Tanzania imesain na China hivyo Marekani imeamua kutengeneza waasi Tanzania kupitia Dini.
Watu wanaosemwa kufadhiliwa na US, Maskini wa Mungu!!!! wengine Yebo Yebo zimeisha, kanzu chafu na chakavu na walikuwa wanatembea na viroba vya unga na dagaa silaha zao nyingi ni Mapanga na shoka ila wasomi waa Jf wakawa wanasisitza humu kuwa hao jamaa ni kazi ya Marekani na ukiwapinga unaambiwa ujui chochote kuhusu Geopolitical.
Kwa jinsi ulivyo andika hapa it shows you know nothing about MKIRU militias and what kind of fire arms they possessed that time. Hapa naandika nikiwa maeneo ambayo baadhi yao walikuwa wametokea na walikuja kufurumushwa na vyombo vetu vya ulinzi na usalama.
Na kwa hakika hujui PSY-OPS na watu wa magharibi wanazitumiaje kuchochea vurugu kama za Libya, Sudan , Syria na Misri. Wewe ni victim tu wa MSM zenye kulenga kuimarisha western hegemony.
 
Back
Top Bottom