Pale mke anapofungwa miaka 30 jela na hurusiwi kuongeza mke, hii hali inatatuliwa vipi?

Nimekuelewa vema na sidhani kama umenipinga bali umeeleza kwa protocol zaidi na duongeza mambo mengine nisiyoyajua. Huwenda mwenzangu ni mkatoliki muhusika zaidi(padre , katekista,mleyi,askofu,mzee wa kanisa au shemasi) kuliko mimi. Ingawa hata mimi sikuzungumzia talaka kwa maana ya karatasi kama wanayotumia waislamu ila nilimanisha sababu moja wapo inayotosha kuachanisha watu. Nadhani kutumia neno kuachanisha ndio palipoleta shida ulipenda nisitumie neno hilo kwakuaa ndo inavunjwa na kiwa kama haikiwepo .
Ila ahsante kwa ufafanuzi wa kiteolojia.
 
Inamaana ile mpk kifo,
Kinakua Ni kiapo batili au[emoji848]
Mkuu sana deep pond . Ndoa za kikatoloki zina vinisheria ambavyo hata kwenye biblia hazipo. Mfano biblia inasema unaruhusiwa kumwacha meanamke kwa kosa la "uzinzi" kufanya tendo la ngono na mtu mwingine asiye mwandoa wake. Lakini kiuhalisia sababu hiyo haijafanikiwa kuwatebganisha wanandoa wa kikatoliki .
Karibu Ng'wanamalundi kwa ufafanuzi
 
Daaaah aiseee.
 
Mkuu, ni kweli sikuwa nakupinga. Nilijikita katika kufafanua mambo zaidi kwa kutumia uzi wako ulioanzisha hoja hiyo. Hoja zako ni sawasawa na zangu. Lakini niliona niende mbele kwa kuelezea mengi zaidi ya uliyoyasema.
Kwamba mwenzio ni Mkatoliki mhusika zaidi kuliko wewe, hilo siyo kweli. Nilibatizwa katika dini ya Katoliki, nikapata Komunio ya Kwanza na Kipaimara, na baadaye nikafunga ndoa, yote hayo chini ya Kanisa Katoliki. Sina cha ziada ya hapo.
 
Mkuu, unayoyasema yalijibiwa na Yesu mwenyewe; angalia Mateo 19: 3-8.
'Some Pharises came to him and tried to trap him by asking, "Does our Law allow a man to divorce his wife for whatever reason he wishes?" Jesus answered, "Haven't you read the scripture that says that in the beginning the Creator made people male and female? And God said 'For this reason a man will leave his father and mother and unite with his wife, and the two will become one'. So they are no longer two, but one. No human being must separate, then, what God has joined together." The Pharisees asked him, "Why , then, did Moses give the law for a man to hand his wife a divorce notice and send her away?" Jesus answered, "Moses gave you permission to divorce your wives because you are so hard to teach. But it was not like that at the time of creation".
 
Dini iliweka wazi pia tuoe ili kuondokana na uzinzi, sasa katika hii hali mwanaume anaweza kukaa miaka 30 bila kupata unyumba ?
Ngumu sana. Nimefikiria hivi tuko tunaishi na wake zetu na bado haturidhiki tunachepuka, sasa uambiwe miaka 30? Achana na hilo, hata mwaka mmoja ni ngumu sana kuvumilia sema mwanamke akifungwa mwaka akitoka lazima atajua tu jamaa alikuwa anachepuka. ila atavumilia
 
Hakuna cha vatican wala cha marekani, sheria za ukristo ni kwamba huwezi kuongeza mke na kitu pekee cha kuwatenganisha ni kifo
Yapo mazingira ndoa hutenganishwa, mfano uzinzi lipo wazi.

Na hili pia nadhani wanatenganisha.
 
Hapa ndugu unapotosha.

Ushauri wako wa kusema aende kuomba ushauri hapo ndio umekaa sawa, naamini kabisa katika hili ndoa inavunjwa tena na askofu wala si kwa papa.
 
Hakuna cha vatican wala cha marekani, sheria za ukristo ni kwamba huwezi kuongeza mke na kitu pekee cha kuwatenganisha ni kifo
Kwa hiyo mkristo mke wake akifungwa miaka 30 haoi tena wala kufanya ngono?tuache kujidanganya
 
Haina mjadala unaoa tu mwngne, wakati mwngne tujue kuwa hiz din n sheria na sheria zmewekwa ili zvunjwe teh teh teh!
Bora kuoa mwngne kuliko kuanza kudanga huku na kule, oa akitoka jela uje kuomba ushaur tena.
Watu wanafungwa miaka mitano tu wakitoka wanakuta mke kashaolewa au mume kaoa ndo iwe 30!!?unaoa tu
 
Siku hizi Maaskofu wa Majimbo wamepewa mamlaka ya kutengua ndoa. Haichukui tena muda mrefu kama kuna sababu ya msingi.

Nafahamu mifano miwili ya ndoa ambazo utenguzi haukuchukua zaidi ya mwaka mmoja.
Hakuna mamlaka zaidi ya mahakama kwenye kutengua ndoa
The rest ni ndoto za abunuasi
Hao maaskofu hawana locus stand
Pia hawa toi divorce certificate mkuu
 
Ni kuoa mke mwingine tu hakuna namna..mambo Kama hayo Mungu husamehe Jamani..
 
Cha kuongezea,
Ndoa haitakiwa kufungwa kama kuna Chembe Chembe za Uongo,
Kwa maan hyo wew unaetak kufunga Ndoa wakati unajua ni hanithi inadhihilisha wazi kabisa kwamba ulikuwa Muongo Kwa Mwenzio
 
Kitu Ambacho kanisa limekaa kimya ni kuhusu Baadhi ya Watu kunyimwa Baadhi ya Sakrament za Either Ndoa au Update,
Mfano,
Mahanithi (either wa kusababishwa au wa kuzaliwa),watu wenye Jinsia mbili nk
 
Cha msingi wakat wa harusi mnakubaliana kipengele cha kula kiapo kisiwepo
 
Hakuna cha vatican wala cha marekani, sheria za ukristo ni kwamba huwezi kuongeza mke na kitu pekee cha kuwatenganisha ni kifo
Je technically unaweza kumuua, ukatubu halafu ukaoa mwingine ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…