Pale Pastor anapoteleza ulimi wenye hekima humsahihisha

Sio kweli. Halimlengi kila mtu.
Sio wote wanataka kutoka miss kuwa Mrs, wengine ni wanaume, wengine ni watoto, na hata hao wanawake wameshaolewa.

Sio kila mtu anataka kutoka kwenye usafiri wa umma. Wengine tayari wana magari yao
Sijawahi ona mwanaume akilalamika kuwa kakosa wa kuoa πŸ˜‚πŸ˜‚
Kwa kawaida lalamiko la kukosa bwana lipo kwa wanawake pekee.
 
Hawa walaghai kanuni za uandishi humu haziruhusu kuwataja majina yao moja kwa moja, orodha ni ndefu, wapo wa kimataifa na wa ndani, wanapenda kusifiwa na kutukuzwa bila aibu wakitumia mawasiliano ya kisasa. Wengine wamevuka mipaka wanajiita mungu. Hichi kizazi kisipokuwa makini kitaharibiwa akili na hawa matapeli
 
Ni wengi sana wanacheza hizi movie. Wanajua watu wenye shida huvutiwa na miujiza. Ndipo injili ya siku hizi ilipofika i.e. upande mmoja, waumini wenye matatizo wakitafuta miujuza watatue matatizo yao upande wa pili ni wachungaji wanao-fake miujiza ili wavutie waumini (fedha). Mama Rwakatare kabla hajafariki alikuwa na skandali ya kuchukuwa ''misikule'' kijiji kimoja mkoani Pwani ije itoe ushuhuda. TB Joshua naye siku moja niliona kwa macho yangu ''muumini'' mmoja akitoa ushuhuda wa kupona, akidai ametokea Tanzania wakati alikuwa anaongea pure pigeon english ya West Afrika. Ni wengi sana wanafeki.
 
Tupeane mbinu za kukabiliana nao ili tuokoe kizazi cha kesho.
 

Just imagine mtu anajiita Mungu na anapumua na kuishi. Huko Ghana Kuna wale wanajiita Angels. Kuna mmoja anaitwa angel obinim. Yani yeye ni malaika. Tunapoelekea jina Nabii au Mtume litakosa nguvu , tutaingia kwenye malaika na baadae wataanza kujiita Yesu.

Kwa kweli hichi ndio kizazi Cha nyoka .
 

Aisee. Mimi siku ile nilishangaa pale uwanja wa Mkapa usiku wa Mwamposa. Waliokuwa wanatoa ushuhuda ni wa morogoro na Geita, nikajiuliza Hawa wamekuja wenyewe au wamesafirishwa?. Na Kama wamasafirishwa , Hakuna maelekezo waliopewa ?.

Hata Tabora wengi waliotoa ushuhuda sio wa Tabora wengi ni kahama , Musoma na Tarime. Unajiuliza wamekuja wenyewe kutoa ushuhuda au wamesafirishwa kuja Tabora?.
 
Huyo sister kavamia kazi ya Yesu, ni bora tu akawe mwana mitindo hapo atafit

Kweli kabisa, ana mabodi guard hao. Akikusonta uende mbele wanakuja kwa nguvu kukutoa uende mbele ukatabiriwe. Yani anafaa kuwa muigizaji na sio mtumishi wa Mungu.
 
Tatizo kizazi Cha Leo kinawakubali Sana hao manabii wa mchongo.
 
Cha ajabu kuna wenzao wanajinasibu ni wa dini ile, nao wanawaiga hawa kwa kila wanachokifanya mpaka kunena kwa lugha japo wao wananena kwa lugha ya dini yao. Watu wanavurugwa akili hawajui wamuamini nani, waganga wa kienyeji nao 'wameboresha' mbinu zao zifanane na hawa wa dini ili nao wapate wateja. Wako wanaojitangaza ni freemason wakati hata umasoni hawaujui, wanadhani freemason ni taasisi ya kipuuzi na kichawi
 
wameona jina la nabii na mtume limezoeleka na halina mashiko wanaanza kujiita makuhani wengine wakijiita malaika mpaka kujiita mungu. Wanajua sheria za nchi haziwezi kuwaingilia wanachoamini, manabii gani wanaishi maisha ya kifahari huku wafuasi wao wakiishi kwenye umasikini mkubwa? Hawa matapeli ni washenzi, hawaachi kitu mpaka hela ya masikini wanaitaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…