Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Sabaya analaumiwa na wananchi namna alivyokuwa akitumia mbinu za kubambikizia watu makosa ya uongo ili apate anachokitaka.
Wakati mwingine alikuwa tayari hata kublackmail watu kwa kuwapandikizia madawa ya kulevya ili awatoze pesa.
Samia alivyoingia madarakani, tulimuona kama Mtenda haki aliyeamua kumnyoosha yule kijana kutokana na udhalimu wake
Lakini tunasikitika, haijapita hata miezi mitatu tangu Sabaya akamatwe, Samia anatumia mbinu hizohizo za Sabaya ili kunyamazisha mpinzani wake Mkuu.
Leo Mbowe anakwenda kuunganishwa katika kesi ya walinzi waliokuwa wanamlinda mwaka jana, walinzi ambao kukamatwa kwao kunatokana na Mipango ovu ya Sabaya ya kuhakikisha Mbowe hana walinzi anaowaamini wa kumlinda.
Yaani Samia anakwenda kumuunganisha Mbowe katika kesi iliyotengenezwa na Sabaya, halafu wakati huo kamuweka ndani Sabaya!
Kwa kweli sikutegemea hata kidogo kama ni Mkubwa anaweza akageuka namna hii, kutoka kwenye kuhubiri kutobambikizia watu kesi na yeye maenyewe kwrnda kufanya hayohayo.
Mashitaka dhidi ya Mbowe ni ya uongo, hayana mashiko na ni uonevu mtupu!
Haifai kwa mtu mwenye cheo cha Ukuu wa nchi, aliyekula kiapo cha kutenda haki kuanza Kuonea watu na kutenda Dhulma.