Pale unampigia kura ya hapana Spika ukashangaa matakoe yanasoma 100%

Pale unampigia kura ya hapana Spika ukashangaa matakoe yanasoma 100%

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Kwanini Watanzania wa leo tunaamini kwenye inflation? Kwanini tunaamini Sana kwenye ushindi wa asilimia 100%? Kwanini tumepumbazika na cooked data? Kwanini tunawaza sana kwamba tukishinda kwa kishindo tutaleta maendeleo kwa kishindo?

Nimepokea taarifa kwamba upon uwezekano mkubwa 100% isiwe 100% lakini walioifanya isiwe 100% wanaogopa kusema siyo 100% Kwa sababu wakisema siyo 100% wataulizwa hiyo kura yako inaweza kubadili matokeo?

Tukiendelea na jamii ya aina hii na tukaendelea kuweka mafanikio yetu kwenye mizania ya 100% hata kama tupo 67% tunajiumiza Sana. Tunajidanganya kwamba tunakubalika Kwa asilimia mia Moja tunapozungumza mbele za watu lakini wakati huohuo tukikaa uchagoni tunaumizwa sana tunapojiuliza Hawa 23% walionikataa ni wakina nani?

Ukitaka kuchanga karata vizuri kwenye hii hoja jiulize JPM alizungukwa na watu wa aina gani katika macho ya nje na alipoondoka Wale wale watu walifanya Nini? Means kwenye kura za siri walikuwa awamkubali ila kwenye kura za wazi waimwonyesha wapo naye.

Jiulize Ndugai alizungukwa na watu wa aina gani? Kwamba anapata mtelezo wa ulimi then hakuna hata Mmoja kati ya marafiki zake aliyejitokeza kumwombea msamaha au hata basi kumpongeza kwa maamuzi magumu, maana yake hakuwa na marafiki ila walikuwepo marafiki wa kiti chake.

Niombe tubadilike, tukubali ukweli Ili tuweze kujua wabaya na wazuri wetu na kujipanga nao. Maisha ya apendwi mtu yanasujudiwa madaraka yake yamepitwa na wakati.

Wish you all the best wapiga kura
 
Unafiki haujanzaa kwa magufuli au kwa ndugai ni kitu kipo tu kwenye jamii yetu, sasa bunge lote limejaa maccm uliwazaje kuwe na kura ya hapana kama chama tu kilishampitisha, na wale baadhi wapo tu maana kwenye msafara wa mamba hata kenge wamo.
 
Hii homa ya 100% ndio huwa inatuharibia chaguzi kuu. CCM watafukuza mawakala wa vyama vingine, kuchapisha karatasi za kura za ziada nk ili tu wapate 100%.
 
Kila siku unaleta habari zisizo na ushahidi. Eti umepokea taarifa! Tena bila kueleza sources na authentic ya hicho unachotaka tujadili. Hivi hapa kila mtu akieleza "nimepokea taarifa" na kutaka tuijadili tutaendelea kujiita ni great thinkers? Nakushauri ujitathmini na style yako maandiko.
 
Humo kwenye ccm kama katika chama kingine cha siasa kuna makundi ya aina mbili dhahiri nayo ni : Wale walioko karibu na viongozi, hivyo kupata fursa ya kupewa madaraka. Kundi la pili ni wale ambao hawako karibu na watoa maamuzi ya chama hivyo kwa lugha nyingine tunasema hawako karibu na meza!!

Wanachama wa kundi la kwanza kwa kawaida hawakosoi mabaya yoyote yanayofanywa na viongozi kwa kuogopa kumwaga ugali wao, hata Kama wanayaona madhaifu ya Uongozi hawasemi . Kundi la pili kwa kawaida ndio wanaokosoa matendo mabaya ya viongozi wao hata kama kwa siri kwani they have nothing to lose; hawako karibu na meza!!

Hivyo tusione ajabu kuwa kuna wanachama ambao ni CHAWA simply because wanalinda ugali wao kwa kuweka maslahi yao mbele kuliko maslahi ya jamii na TAIFA kwa Jumla!!!

Hapo hapo basi, kwa vile ni lazima kuwepo na wale ambao hawako karibu ya meza ni ukweli usiopingika kuwa kwenye kura ya siri sio rahisi kupata 100% katika uchaguzi wowote; hata kama ni wa ccm!
 
Kila siku unaleta habari zisizo na ushahidi. Eti umepokea taarifa!!tena bila kueleza sources na authentic ya hicho unachotaka tujadili. Hivi hapa kila mtu akieleza "nimepokea taarifa" na kutaka tuijadili tutaendelea kujiita ni great thinkers? Nakushauri ujitathmini na style yako maandiko.
Huwa anajikuta yeye ndio Mkurugenzi wa usalama wa Taifa sijui 🤔
 
Kila siku unaleta habari zisizo na ushahidi. Eti umepokea taarifa!!tena bila kueleza sources na authentic ya hicho unachotaka tujadili. Hivi hapa kila mtu akieleza "nimepokea taarifa" na kutaka tuijadili tutaendelea kujiita ni great thinkers? Nakushauri ujitathmini na style yako maandiko.
Hiyo ndio JF mpya mkuu🤣🤣🤣
 
Ndugai hakuwepo kwenye uchaguzi Lakini kura yake ilipigwa,[emoji23]
 
Mwizi ni mwizi tu haachi asili yake, akikosa cha kuiba atanyatia kofia yake ilimradi airidhishe roho yake ya wizi, na siku zote mwizi hawezi kuendelea hata aibe mabilioni.
 
Hakuna mtu anayependwa na watu wote kwa asilimia mia. Kuna mwanasiasa mmoja aliwahi kuuliza : unataka upendwe na kula mtu wewe umekuwa pesa? Binadamu yeyote lazima achukiwe na kupendwa. Ukipendwa tu jiulize kwa nini.

Huko nyuma katika nchi za kidikteta ndio tulikuwa tunasikia kiongozi ameshinda kwa asilimia mia au tisini na tisa kwa sababu matokeo yalikuwa ya kupika. Sass picha ninayoiona chaguzi za mbele tusishangae tukitangaziwa matokeo kama haya kuanzia uchaguzi ndani ya chama hadi uchaguzi mkuu ule wa 2025.

Nb: Ukiambiwa umeshinda kwa asilimia 100 inatakiwa ujiulize maswali kadhaa.
 
Ngoja nisiumize kichwa kuhusu hili, hii akili kiduchu ngoja niielekeze kwenye mambo mengine
 
Unataka kutuambia hata Convid 19 wanaogopa kuikana 100%? Kama ni hivyo basi mambo yamebadilika sana😅😅
 
Bora Spika na siyo Spika Bora, ubunge aliupataje??
 
Hakuna mtu anayependwa na watu wote kwa asilimia mia. Kuna mwanasiasa mmoja aliwahi kuuliza : unataka upendwe na kula mtu wewe umekuwa pesa? Binadamu yeyote lazima achukiwe na kupendwa. Ukipendwa tu jiulize kwa nini...
Michezo ya chama la wana ni ya kipuuzi jamani, hakuna hata Kura iliyoharibika?

Hii yote ni katika showdown ya kuonyesha Job, alikuwa hakubaliki!

Shame! Mbatia yupo wapi?? Kesi yetu pingamizi itakuwaje?
 
Back
Top Bottom