Pallangyo wa CHADEMA ndio awe Mgombea jijini Arusha 2025

Makupa

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
6,822
Reaction score
4,034
Wananchi wa Arusha bado tunakumbuka miaka ya mateso wakati wa ubunge wa binamu yake Mzee Mbowe. Hatutaki kurudia yale mateso ambayo ni pamoja na fujo za mara kwa mara hadi mkoa ukakosa wageni waliokuwa wanatumia mkoa wa Arusha kama kitivo cha mikutano.

Kwa hiyo, tunawaombeni chonde chonde Pallangyo ndio awe mgombea wa CHADEMA kutokana na yafuatayo;

1. Wazazi wa Pallangyo ni wenyeji wa Arusha sio wahamiaji, hivyo watakuwa na uchungu wa maendeleo ya Mkoa

2. Binamu yake mzee Mbowe alishatamka wazi wazi kuwa ubunge kwake sio dili.
 
Acha unaa hivi kwani kijani mnajifunzia wapi🤔
 
Gambo umeanza kulialia! Lazima hicho kiti ukiteme maana hata 2020 hukushinda wewe!
 
Chadema wanatenda kinyume na wanachohubiri. Kuna haha gani ya kumsimamisha mtu mmoja kugombea ubunge miaka 20 kwa Chama kinachojiita cha demokrasia? Kwanini wasitoe nafasi kwa vijana wanaochipukia na kujitoa kwenye chama?
Nafasi haitolewi kwa kupewa nafasi inagombaniwa.
Huku sio SISIEMU Mtu akimsifia Rais anapewa nafasi ya kugombea ubunge.
 
Lema anatosha
 
Veeepe tena Chato hakukaliki?
 
Wewe mamluki nani atakuelewa ? nyie ccm si mna Mrisho gambo ?

Hebu jisome hapa

 
Jamaa unavyohangaika mara Mbowe, umegeukia kwa Lema, baadae sijui utahamia kwa Sugu au Heche..

Anyway, hiyo ndio Chadema, lazima umeze kidonge cha Panadol kila siku ukiendeleza ujuaji wako.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Gambo ni mwenyeji?
 
Chadema wanatenda kinyume na wanachohubiri. Kuna haha gani ya kumsimamisha mtu mmoja kugombea ubunge miaka 20 kwa Chama kinachojiita cha demokrasia? Kwanini wasitoe nafasi kwa vijana wanaochipukia na kujitoa kwenye chama?
Kama anakubalika sioni tatizo. CCM ndio kuna watu wamejimilikisha majimbo tena wanawaachia watoto wao.
1. Lukuvi miaka 20+
2. Lowassa 20+ Lowassa Jr.
3. Pinda 20+ Pinda Jr.
5. Kikwete 20+ Kikwete Jr.
List ni ndefu
 
Kama anakubalika sioni tatizo. CCM ndio kuna watu wamejimilikisha majimbo tena wanawaachia watoto wao.
1. Lukuvi miaka 20+
2. Lowassa 20+ Lowassa Jr.
3. Pinda 20+ Pinda Jr.
5. Kikwete 20+ Kikwete Jr.
List ni ndefu
Hata Chadema kuna watu wamegombea miaka 15+ kina Heche, Mbowe, Lema, Sugu, Mdee n.k. Half kuna haja gani ya kuipinga CCM km mnafanya mambo yanayofanana?
 
kwahiyo umeamua kuchochea joto la kisiasa kuni mbichi kiainaee🐒

binamu ana hasira anaweza kupiga mtu na kitu kizito, halafu mbaya zaidi anajua na anauhakika kabisa Arusha amechokwa hawezi toboa ng'oo 🐒
 
kwahiyo umeamua kuchochea joto la kisiasa kuni mbichi kiainaee[emoji205]

binamu ana hasira anaweza kupiga mtu na kitu kizito, halafu mbaya zaidi anajua na anauhakika kabisa Arusha amechokwa hawezi toboa ng'oo [emoji205]
Arusha wanasema hawaitaki ccm asilani,na wameonyesha hivyo kwa vitendo,tena si tu kipindi hiki cha vyama vingi, hata enzi ya chama kimoja migogoro ya ndani ya ccm yenyewe ilitosha kuonyesha kuwa Arusha kuna kitu wanakihitaji kuliko ccm,ila hakikuwepo kwa kipindi hicho,hivyo siasa za vyama vingi zilipoingia tu wana Arusha waka take chance, huijui arusha wewe,tulikuwepo,tupo,na tunajua.
 
CCM wanauhakika sifahamu kama kuna kitu, ispokua Chadema kuna fukuto, jotroo, na motroo mkali unawaka ndrani kwa ndraaaaaani ukilipuka sijui itakuaje 🐒
 

..kama mnataka kila mtu akagombee alikozaliwa basi Samia naye asigombee huku Tanganyika, arudi kwao Zanzibar.
 
Umempigia kampeni Lema bila kujua. Ndo matatizo ya kukurupuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…