Kwenye mada kama hii, ndipo umma wa JF unapokosa fursa nzuri kabisa, ya kuwa chanzo cha elimu kwa wengi wetu.
Kwa mfano: mimi ningependa kujua muundo wa hivi vyama vya ushirika ukoje na sababu zinazofanya visiwe na ufanisi katika utendaji wake.
Hivi vyama vinaundwa na serikali, au wananchi wenyewe?
Wananchi wanayo mamlaka yoyote juu ya vyama hivi?
Ni nini wajibu wa serikali katika usimamizi wa hivi vyama.
Hizi taarifa za kuvuruga juhudi za wananchi ndizo zitakazoendelea kutufanya taifa zima kubaki maskini
Kwa nini hatuwezi kukopi tu walichofanya nchi zingine na kurekebisha kidogo kulingana na mazingira yetu, ili na sisi tupate mafanikio?
Ununuzi wa mazao ya mkulima, mbona linakuwa tatizo sugu kiasi hiki?
Miaka yote hii, tokea tupate uhuru wetu, tunashindwa nini kulishughulikia tatizo na kuliondoa kabisa?
Mi ni mwathirika wa ushirika nitakupa matukio kadhaa kwa upande wa kahawa.
Ngazi ya chini kabisa ni vyama vya msingi. Kuna ghala, m/kiti, karani, wajumbe, mlinzi. Wakulima huleta mazao (kahawa) kwenye ghala, hupima na kupewa stakabadhi ya kilo. Ghala likijaa karani anaita gari kutoka chama kikuu. Chama kikuu kinakoboa na kuunganisha uzito na vyama vikuu vingine wanaenda kwenye soko la dunia.
Madhara ya ushirika
1. Mizani ya mawe wazee hawajui kuisoma hivyo karani anaiba kilo na kujiwejekea kwa jina lake na wenzake ila wengi wamepatwa na mabalaa
2. Mkulima utakaa na shida zako labda chama kikuu kiwahurumie kiwalipe nusu ya malipo kwa kukisia bei. Baadae mnaweza kuambiwa soko la dunia limeshuka hakuna nyongeza na huna wa kumhoji kwa sababu hakuna mkulima wa kijijini aliyewahi kuona soko la dunia.
3. Mzigo wa mazao unaweza kupigwa ghalani au ukaharibika wakulima wakalazimishwa kukatwa.
4. Gharama zote za uendeshaji wa ofisi, za kusafiri kwenda soko la dunia, n.k zinalipwa na mkulima. Sijui anayepanga viwango vya mishahara na benefits.
Sasa kwa kuwa mkulima anakuwa ameshasubiri muda mrefu, hela anayopewa anashangilia ila swala la imechotwa kiasi gani na imechotwa na nani kwa matumizi gani hayo wanajua intelijensia.
Kinachoumiza ni kwamba anaweza kuja mnunuzi toka nchi jirani anatoa bei mara mbili ya bei ya ushirika na analipa cash lkn ataitwa mhujumu uchumi.
Hapa ni upande wa kahawa ila kila zao lina sarakasi zake.