Vyama vya ushirika kwa mujibu wa Sheria ya vyama vya ushirika ya mwaka 2013 vimeundwa katika 3 tier system.
1 chini kuna kuwa na vyama vya msingi au PCS ambavyo vinaundwa na wakulima wenyewe.
2 Kati kuna chama kikuu ambacho majukumu au Union ambacho wanachama wake ni hao PCS.
3 Mwisho ni Federation ambayo wanachama wake ni vyama vikuu japo PCS pia wanaweza kuwa wanachama wa shirikisho.
Hii ndiyo structure iliyopo kwe Agricultural Marketing Corperative Socities (AMCOSs)
Sasa ili serikali uweze kumonitor ushirika sheria imeanzisha chombo kinachoutwa REGISTRAR wa vyama vya ushirika ambaye ana watu wake mpaka huko wilayani ambao wengi ni mchwa wa kutafuna pesa za ushirika kwa kushirikiana na viongozi wa ushirika hasa vyama vikuu na vyama vya msingi.
Sheria ya mwaka 2003 ilikuwa na 4 tier structure ambapo kulikuwa na chama kilele au APEX ambacho kiliondolewa baada ya kuwa chanzo cha migogoro na upigaji tu.
Sasa kuhusu changamoto zilizochangia kulala kwa vyama vya ushirika na uwezo wake wa sasa kuhudumia wakulima hii ni mada ndefu kwa sababu umeomba muundo niishie hapa kwanza.
Sent using
Jamii Forums mobile app