Pamba, Korosho Mmeshindwa kununua sasa mnanyang'anya Watu Choroko zao

Natamani mh Bashe apite hapa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi ni mwathirika wa ushirika nitakupa matukio kadhaa kwa upande wa kahawa.
Ngazi ya chini kabisa ni vyama vya msingi. Kuna ghala, m/kiti, karani, wajumbe, mlinzi. Wakulima huleta mazao (kahawa) kwenye ghala, hupima na kupewa stakabadhi ya kilo. Ghala likijaa karani anaita gari kutoka chama kikuu. Chama kikuu kinakoboa na kuunganisha uzito na vyama vikuu vingine wanaenda kwenye soko la dunia.
Madhara ya ushirika
1. Mizani ya mawe wazee hawajui kuisoma hivyo karani anaiba kilo na kujiwejekea kwa jina lake na wenzake ila wengi wamepatwa na mabalaa
2. Mkulima utakaa na shida zako labda chama kikuu kiwahurumie kiwalipe nusu ya malipo kwa kukisia bei. Baadae mnaweza kuambiwa soko la dunia limeshuka hakuna nyongeza na huna wa kumhoji kwa sababu hakuna mkulima wa kijijini aliyewahi kuona soko la dunia.
3. Mzigo wa mazao unaweza kupigwa ghalani au ukaharibika wakulima wakalazimishwa kukatwa.
4. Gharama zote za uendeshaji wa ofisi, za kusafiri kwenda soko la dunia, n.k zinalipwa na mkulima. Sijui anayepanga viwango vya mishahara na benefits.
Sasa kwa kuwa mkulima anakuwa ameshasubiri muda mrefu, hela anayopewa anashangilia ila swala la imechotwa kiasi gani na imechotwa na nani kwa matumizi gani hayo wanajua intelijensia.
Kinachoumiza ni kwamba anaweza kuja mnunuzi toka nchi jirani anatoa bei mara mbili ya bei ya ushirika na analipa cash lkn ataitwa mhujumu uchumi.
Hapa ni upande wa kahawa ila kila zao lina sarakasi zake.
 
Wahusika ni washirika yaani wakulima na viongozi watakaowachagua, maafisa ushirika ambao ni serikali wanaowashauri na kuwaongoza viongozi, mrajisi wa mkoa ambaye ni serikali kazi yake ni kusimamia vyama vya mkoa wake na wakaguzi wa mahesabu ya vyama vya ushirika ambao ni taasisi ya serikali(coasco). Huo ndo muundo.
 
Kifupi..hivyo vyama vya Ushirika ni uridhi wa wakoloni .Vyama hivi vingi vilianzishwa baada ya ww2 malengo yakiwa kuongeza tija ya uzarishaji,kusaidia wakulima kupata masomo pamoja na elimu.Ila lilijificha ilikua ni njia ya kuwezesha wakoloni kuwanyonya wakulima kwa wakati mmoja basi usishangae mpaka sasa huu mfumo upo na ndiyo mbaya zaidi.Ukienda kwa wakulima na kuwauliza kama wakati wanalima walipata msaada kutoka kwenye chama cha ushirika? Majibu tunayo....alafu mkija mnasema kua serikali ya wanyonge...Serikali ya wajamaa...kumbe uhalisia ni ubepari na ubeberu tu.
 
Hili haikubaliki nadhani kuna makosa sehemu fulani.
serikali kuu itaingilia kati nadhani. Mwananchi hawezi kudhurumiwa na serikali.
Subiri Polepole akiishakagua utekelezaji wa ilani, wanajeshi lazima watatumwa kununua choroko virzuri kama walivyofanya kwenye korosho kule 'Ntwala'
 
Mbaazi nazo waliziuwa halafu siku ya kura CCM 💩 wanaenda na Mapolisi kuwatisha Wakulima
 
Huu ni unyonyaji
 
Mkuu mazao tu ni shida ambayo ishakuwa sugu miaka na miaka. Alafu utasikia walegeza pua tunapambana na BEBERU. Naishiaga kucheka tu
 
Halafu cha ajabu Mkuu Vyama vyenyewe havina pesa za kununulia mazao. Yaani Mfanyabiashara unatakiwa ufanye makubaliano na Chama cha Ushirika unahitaji aina na kiasi gani ya mazao kisha unawapatia fedha wakununulie mazao toka kwa Wakulima. Kwa kifupi Vyama hivi vimekuwa ni madalali wa mazao ya Wakulima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli mkuu hao ni wezi zaidi ya mkoloni
 
Nimekusoma vizuri sana, mkuu wangu 'Mbekenga', nimepata mwanzo wa somo mhimu toka kwako.

Kwa maoni yangu ya harakaharaka kuhusu haya uliyoandika hapa, lawama nawatupia serikali moja kwa moja kwa kushindwa kusimamia vyema utendaji wa vyama hivi katika ngazi zote.

Lakini si hivyo tu, serikali inao wajibu, na uwezo inao wa kujua mwelekeo wa mazao mbalimbali katika soko la dunia kwa uhakika zaidi.

Teknolojia iliyopo leo, kwa nini tusiweze kuitumia ili kuondoa hizi sintofahamu zisizokuwa za lazima?

Kwa nini serikali isiwe na kitengo maalum, cha kufuatilia bei za mazao mbalimbali katika soko la dunia?

Kitengo ambacho kinao uwezo hata wa ku'forecast' bei za mazao yetu miaka michache mbele kutokana na uzalishaji sehemu mbalimbali duniani?
Hapa kuna ugumu gani?

Inasikitisha, kama hadi hii leo, miaka karibu 60 tokea tupate uhuru wetu, bado pawe na watu ambao wanavungwa tu na mpuuzi fulani na kuwaibia jasho lao kupitia kwenye vipimo. Inasikitisha sana.
Kuna idara nzima ya vipimo wizara ya biashara inayotakiwa kuhakikisha mizani yote inayotumika nchini inakidhi viwango..., lakini, bado hili nalo ni tatizo. Sisi sasa tutaweza kitu gani?

Mshutumiwa wa kwanza kabisa katika kufifisha juhudi za wakulima ni serikali yenyewe.

Hii habari ya "walanguzi" ni kisingizio tu cha kujitoa lawama.
 
Serikali ya CCM ... Alafu MTU mmoja utasikia anasema... serikali ya wanyonge

"What is yours will always be yours no matter what "
 
Ahsante sana mkuu, kwa ufafanuzi huu.

Kufikia hapa, naona serikali yenyewe ndio tatizo kwa wakulima.

Hawa watumishi wake wote hawafanyi kazi ipasavyo.

Hadi hapo serikali itakapokuwa na nia dhati ya kuvifanya hivi vyombo vifanye kazi yake ipasavyo, ni kazi bure kuwalaumu 'walanguzi' ambao kiuhakika wanajaza ombwe lililosababishwa na hawa watendaji wa serikali.

Kwani kuna ugumu gani kwa serikali ikitaka hivi vyama vya ushirika viwahudumie wakulima kwa weledi? Serikali inashindwa wapi katika hili!
 
Hali ni MBAYA SANA kila mahali na kwa kila zao la biashara. Ushirika kumejaa urasimu na WIZI, WIZI, WIZI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usichokijua ni kwamba maafisa ushirika wa serikali walishiriki kuibia wakulima katika vyama vya ushirika vya tumbaku Tabora.

Mpaka sasa hakuna chama hai Tabora tena vingine vina mademu hadi ya billioni Tatu ambayo hayana hata maelezo.

Ni ngumu sana kujua namna gani imeshiriki kuua zao la tumbaku kizembe na kuchochea umaskini mkubwa kwa watu wa Tabora ambao ndiyo lilikuwa tegemeo kubwa la kuingiza pesa nyingi sana kwa wakulima.

Basi kwa sababu bado tuko chini ya serikali ya ccm wakulima wataendelea kuwa GUINEA PIGS wa sera ovu za ccm.
Hili haikubaliki nadhani kuna makosa sehemu fulani.
serikali kuu itaingilia kati nadhani. Mwananchi hawezi kudhurumiwa na serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…