Pamba, Korosho Mmeshindwa kununua sasa mnanyang'anya Watu Choroko zao

Title ya thread ni ya kishabiki, inaonyesha thread hii siyo objective. Badala ya kuandika "Serikali imeshindwa..." iimeandikwa kwa maana kuwa sisi tutaosoma thread ndiyo tumeshindwa. Ninajua mwandishi alikuwa na maana gani lakini matumizi ya hiyo lugha ya kejeli ndiyo inakoseasha thamani thread nzima.
 
Vyama vyote vilishakufa na vina madeni yasiyolipika leo nani Aende kufanya biashara na bankrupt entities?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanda pendwa ni hisia tu, tingatinga halijabakiza sehemu yoyote. Kila mtu anakula jeuri ya chama kwa namna yake!
Huyu Mzee analazimisha vitu vya kipumbavu sana, yule mfanyabiashara kasema.kabisa kwamba amelipa ushuru kwa mtendaji wa Kata na risiti anazo za serikali lakini mkuu wa wilaya anatumia mabavu kunyang'anya mzigo! Nitamkumbuka sana Mzee Mwamwindi!
 
akimaliza kwetu atakuja na kwenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali inahofia madalali kutumia huo mwanya kuwakandamiza wakulima.
Mkuu nikuulize swali la kizushi, kwa mfano hapa kuna wanunuzi wawili: mnunuzi wa kwanza ananunua kwa cash lakini pungufu ya shilngi 200 ya mnunuzi wa pili ambaye ananunua kwa mkopo ambaye hajulikani atalipa lini. Mkuu utaenda kwa mnunuzi yupi?
 
Vyama vya ushirika kwa mujibu wa Sheria ya vyama vya ushirika ya mwaka 2013 vimeundwa katika 3 tier system.

1 chini kuna kuwa na vyama vya msingi au PCS ambavyo vinaundwa na wakulima wenyewe.

2 Kati kuna chama kikuu ambacho majukumu au Union ambacho wanachama wake ni hao PCS.

3 Mwisho ni Federation ambayo wanachama wake ni vyama vikuu japo PCS pia wanaweza kuwa wanachama wa shirikisho.

Hii ndiyo structure iliyopo kwe Agricultural Marketing Corperative Socities (AMCOSs)

Sasa ili serikali uweze kumonitor ushirika sheria imeanzisha chombo kinachoutwa REGISTRAR wa vyama vya ushirika ambaye ana watu wake mpaka huko wilayani ambao wengi ni mchwa wa kutafuna pesa za ushirika kwa kushirikiana na viongozi wa ushirika hasa vyama vikuu na vyama vya msingi.

Sheria ya mwaka 2003 ilikuwa na 4 tier structure ambapo kulikuwa na chama kilele au APEX ambacho kiliondolewa baada ya kuwa chanzo cha migogoro na upigaji tu.


Sasa kuhusu changamoto zilizochangia kulala kwa vyama vya ushirika na uwezo wake wa sasa kuhudumia wakulima hii ni mada ndefu kwa sababu umeomba muundo niishie hapa kwanza.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali inahofia madalali kutumia huo mwanya kuwakandamiza wakulima.
Wazo swafi kabisa na tunaliunga mkono 100%. Lakini, kuwakopa wakulima halafu uyachukue mazao yao ndio ukatembeze kutafuta soko. Hivi hilo ndo wazo safi??
Mkulima amewekeza kwenye jembe lake, akisali kila siku kuwa mvua inyeshe ya kiasi isijezidi mazao yakazolewa na maji kwa sababu ya miundo mbinu hovyo.
Sasa kavuna, unasema kumlinda ni kungoja aje mnunuzi aliyelipa cash akamuokoa huyu mkulima weye umnyang'anye bila hata kumrudishia kile alichotoa. Useme; Sitaifishi gari kwa kuwa lilikodishwa kuubeba mzigo tu. Aliyenunua mzigo unamwambia; Kimbia tena usiangalie nyuma au nikufunge kwa uhujumu uchumi.
We waona; Hallal?? Nadhani we au miye mmojapo ni chizi. Onesha muunganiko wa utaifishaji wa kilichonunuliwa bila refund na ukandamizaji wa madalali kwa mkulima.
 
Mkuu 'PTER', ahsante kwa somo zuri.

Kumbe 'gut feeling' yangu tokea mwanzo ilikuwa ni sahihi.

Tatizo ni bayana kabisa, lipo serikalini.

Sheria zilizopo kusimamia ushirika hazitekelezwi ipasavyo, na watendaji katika ngazi zote za ushirika hawawajibishwi kusimamia kazi zao ipasavyo.

Tatizo la wakulima ni serikali.
 
Yule mfanyabiashara ni kama anaonewa, kwanin asipewe mlolongo wa kufuata ili arejeshewe mali yake. Nimejikuta namuonea huruma kwa jinsi alivyojitetea, sasa endapo kakopa Benki ndio baaasi mnada wa nyumba yake unamhusu. Hurumaaa
Toka lini wakawa na huruma hawa,we check bandarini tu wanavopiga minada gari za watu bila huruma hawana uwezo wa kufikiri zaidi ya kukariri kumbe zipo njia mbadala tu wangetumia wakapata kodi zao bila kumpora MTU gari lake
 
Serikali inahofia madalali kutumia huo mwanya kuwakandamiza wakulima.
Wakulima sio malofa kama unavyofikiri, eti kuwakandamiza, sijui nini kwanini serikali inapenda kuingilia biashara na wakulima, usikute huyo DC mkulima akikosa kulipwa kwenye ushirika hajui hata namna ya kumsaidia, ni rahisi tu kufanya uhalifu wa kutaifisha mali za watu ili mkubwa aone anafanya kazi!
 
What? Mpunga wangu nikauzie wapi? Mpunga si pamba, nitautunza ndani nile na familia yangu kidogo kidogo hata kwa miaka 4 hadi uishe. Sipend
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…