Pambano la Cheka Na Mserbia

Aisee hata mimi jana nimeshangaa sana...cheka mwenyewe hajaamini kma kashinda maana kapewa...cheka kapigwa mwanzo mwisho halafu wanasema kashinda
 
Mzungu alikuwa anapiga ngumi kwa akili sana na alikuwa anapiga kwenye point tu.....cheka ndiyo alikuwa hajiamini muoga anakimbia ngumi zake hazifiki kwa mpinzani hata ikifika inaishia kwenye gadi na haina nguvu.....unazi haufai cheka kapigwa round zote.
 
Watanzania tuwe na kasumba ya kukubali matokeo, maana Jana baada ya Francis Cheka kutangazwa mshindi WBF wengi walianza kuponda kwa kusema amebebwa. Tuwe na Uzalendo
 
Nakushukuru sana mtoa mada kwa kulileta hili hapa jukwaani.
Binafsi nimelala saa 9 usiku leo na hadi sasa kichwa kinauma nikifikiria lile pambano.
Cheka alizidiwa,yule Mserbia alikuwa anarusha ngumi kimahesabu zaidi.
Ila kilichomnyima ushindi mzungu yule ni mchezo wa kujilinda zaidi ambao kitaalamu hupunguza points.

Hata hivyo hadi mwisho wa pambano niliamini mzungu kashinda,na hata Cheka mwenyewe alikuwa ameshaamini hivyo maana alikuwa hajiamini hata kunyanyua mkono (kabla ya kutangazwa mshindi alijilazimisha).
Wakati wa kutangaza mshindi Mserbia yule alitoka mbele kujiandaa kushangilia lakini matokeo yalituacha tulio wengi midomo wazi hata kushindwa kushangilia maana hatukuamini.

Cheka wa sasa sio Cheka yule kabla ya kwenda gerezani,hili limemuathiri sana kisaikolojia kwani amekuwa muoga hadi aibu!
Hana ile ari ya kimchezo tena.
Nachelea kusema kwa mchezo wake ule wa jana angepanda ulingoni na yule mdogo wake Cosmas aliyeshinda kwenye pambano la awali dhidi ya Dotto basi Francis angepigwa na mdogo wake Live!

Mwalimu wake aangalie hili upya,Cheka amekwisha kabisa!
 
Kuna mtu alianzisha thread hapa, kwamba Cheka alikuwa akila kichapo cha aibu. Kumbe ilikuwa chuki binafsi.
 
Uzito waliokubaliana ni Kg 72.2 Sasa juzi wakati wanapimwa Cheka akawa na Kg 74.6 akawa amezidi 2.4Kg.

Unajua kinachofanyika ukizidi uzito kuna option mbili moja nikuwithdraw pambano chapili ni kupungua ndani ya muda huo.

Ikabidi Cheka aanzie toilet akajiminye baada ya hapo unafanya mazoezi ya kukimbia na kuruka ruka ili kukata kilo.

Kwa masaa 5 akafikisha 72.6 akawa analalamika kuwa amechoka mpaka wanapigana Jana inamaana alikata kilo mbili ndani ya masaa machache.

Wataalam wa ngumi wanasema kupunguza 2Kg kwa siku moja huwa ni ngumu sana na ukifanikiwa kesho yake unaweza kupiga punch Ila haziwi heavy zinakuwa light punch unless mpinzani awe dhaifu sana.

Kwa hayo nilijua atachapwa tu lakini ndio hivyo jaji Lubuva na Jecha waliingilia mpambano.
 
Siasa kila mahali mengine tutakuja kumzika mtu huku ndiye mshindi.
Ni Mtanzania na mwenyeji wa Morogoro,hatari zaidi ktk dimba nilikuwepo...narudia tuweke siasa ktk mengine ila si Ngumi,itakuja kutokea Tz Pekee Mshindi ndiye Marehemu kwa style hii.
 
Siasa kila mahali mengine tutakuja kumzika mtu huku ndiye mshindi.
Ni Mtanzania na mwenyeji wa Morogoro,hatari zaidi ktk dimba nilikuwepo...narudia tuweke siasa ktk mengine ila si Ngumi,itakuja kutokea Tz Pekee Mshindi ndiye Marehemu kwa style hii.
Yaelekea unaujua mchezo wa ndondi kuliko majaji!!
 
Watanzania tuwe na kasumba ya kukubali matokeo, maana Jana baada ya Francis Cheka kutangazwa mshindi WBF wengi walianza kuponda kwa kusema amebebwa. Tuwe na Uzalendo
Uzalendo wa kipumbavu hatuutaki.
Tutaonekana wajinga mbele ya jamii ya kimataifa.
TUNASEMA CHEKA KAPIGWA NA JANA KABEBWA. MSERBIA KASHINDA BILA CHENGA ILA USHINDI WAKE UMEPORWA NA MAJAJI WASIOJUA NDONDI BALI UPUUZI WA KUBEBANA.
CHEKA KAPIGWA FRESH KABISA, tusiaminishane ujinga. Kala za kutosha jana.
Mserbia oyeeeeeeeeeeeee!
 
Mimi si mtaraamu wa Masumbwi ila jana ilikuwa Surprising ya Wikiend.. ila kwa style hii kushinda nje ya nchi itakuwa ngumu
"Hongera Cheka"
 
Ameshinda nyumbani, Jambo zuri, nyi mlikua mnatakaje? Ashindwe mpate cha kuongea, Viva cheka, mcheza kwao utunzwa! Kashindwa Pacquiao na ngumi nyingi! Watu wanaesabu zilizofika sio nyingi za kujilinda!
 
Kwenye ngumi kuna umafia sana , ushindi huwa unapangwa kabisa.
Ushindi wa halali huwa ni KO peke yake.
 
Hata Mao Pacquao kwa macho ya kawaida kabisa alimpiga Mayweather,lakini mwisho wa sikuuuuuuuu mmarekani alibebwa kwa mbeleko ya nyumbani
 
Kama nyuma ya pazia mambo yalikuwa hivi basi Cheka alijitahidi sana.
Naanza kuondoa mashaka makubwa niliyoyapata juu yake maana jana hadi nilikuwa siamini ninachokiona.
Mwanzoni nilipanga nisiangalie mpambano wote ila nilijikuta usingizi unakata nikaangalia hadi mwisho.
Ila bado Cheka anatakiwa kubadilika arudi kwenye ubora wake.
 
Tafuteni calculation za Majaji tuone ndo tuukumu. Kiufupi Cheka amepiga ngumi nyingi na za kiufundi kwenda kwa mpinzani wake! (May weather style). Mserbia amenyang'anywa point Mara mbili kwa kucheza faulo za kumkaba Cheka na anajua refa alimwambia! Someni ukumu kutoka kwa majaji sio hisia zenu!. Kama kushangilia kwa Cheka ata May weather hakushàngilia kwa kuwa hakujua kuna nini kwa majaji, dhidi ya Pacquiao, Ushindi wa points una mambo mengi, kama faulo, ngumi nyingi za kupapasa, kupiga kwenye groups,na kadhalika ambazo wewe Unaweza esabu lakini majaji hawaziesabu.SI KILA MWENYE MBIO USHINDA MCHEZONI, ILA NI BAHATI ,TAIMING NA WAKATI!.(Biblia Mhubiri)soma.
 
Ameshinda nyumbani, Jambo zuri, nyi mlikua mnatakaje? Ashindwe mpate cha kuongea, Viva cheka, mcheza kwao utunzwa! Kashindwa Pacquiao na ngumi nyingi! Watu wanaesabu zilizofika sio nyingi za kujilinda!
Mkuu binafsi nashauri uangalie tena hilo pambano halafu baada ya hapo ulete mrejesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…