Uchaguzi 2020 Pambazuko la kipenga cha mwisho sehemu ya pili

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Tuna chini ya siku 150 kuelekea uchaguzi mkuu.
Huu utakuwa uchaguzi mkuu tofauti kabisa na chaguzi nyingine zote zilizopita
Hakuna amsha amsha hakuna shamra shamra

Hakuna kimbiza kimbiza... Kumetulia sana na kwa sehemu kuna wasiwasi, woga na sononi kwa wananchi... Lakini pia wana tashwishwi ya kutaka kuona maajabu yakitendeka.

Muda uliobaki ni mchache sana lakini ni muhimu sana kwa kila dakika inayo tiktok.. Kuna mambo yanaendelea kimyakimya... Chinichini lakini kwa haraka na wepesi wa ajabu

The race against time...! Kama kutakuwa na huo uchaguzi (achana na neno HURU na HAKI) Tanganyika inaweza kuishangaza dunia.. Kila zama huwa na kurasa zake... Na unapofika wakati wa kufunua ukurasa husika huna budi.. huna jinsi.. Huna namna.. Huna hiari... Inabidi kuufunua...!!!

Kila jambo huwa na kikomo cha kuwa... Kikomo cha zama.. Kikomo cha nyakati... MWANADAMU ni mtumwa wa muda... Achana na maneno HURU na HAKI kuna watu walivikwa ukuu wakiwa hawapo... Kuna watu walikabidhiwa majukumu makubwa wakiwa mbali uhamishoni..

Kuna baadhi ya imani ukitaka kuoa mke si lazima uwepo eneo la tukio... Ndugu yako anaweza kukuolea kwa maneno halafu vitendo ukaja kufanya mwenyewe

Hili ni pambazuko la kipenga cha mwisho.. Kila alfajiri ipitayo haitarudi tena... Nje upepo unavuma lakini unavuma na mengi... Ni alfajiri nyingine tena...

Natambua wazi jana ulilala fofofo baada ya uchovu wa kazi na mihangaiko ya siku nzima... Juma zima... Lakini wapo ambao hawalali... Hawakulala na hawatalala mpaka kipenga cha mwisho kitakapodhihiri mwangwi wake na kupotelea kwenye kadamnasi ya hadhira yenye tashwishwi kubwa ya mabadiliko

Ni alfajiri nyingine tena.. Wanaume hawajalala ni mwendo wa kuandaa mazingira ili timu pinzani isiliguse dimba.. Kisha tutangaziane ushindi mnono wa kishindo!!

Kwenye kila andishi kuna TAMATI... Kama tamati ya andiko lako imetimia funika buku lako ulirudishe kabatini kwakuwa hakuna kurasa zaidi... Huhitaji kufanya marudio ya kurasa

Kuna kitabu kipya na wasomaji wapya.. Wape nafasi kwa upendo na bila ghiliba wasome kwa utulivu na amani kurasa zao... Nao kuna siku watafikia TAMATI... Usilazimishe makhaba kama hisia zumeshakufa

Kumbuka ni wafu pekee ndio wasiokula wala kunywa... Chumvi ikiisha ladha haifai tena kwakuwa hakuna cha kuipa ladha tena..
Ni alfajiri ya kipenga cha mwisho. Pambazuko lenye tumaini jipya. Achana na maneno HURU NA HAKI.. Uchaguzi utafanyika.. Maajabu yatatokea na dunia itashangaa

Jr[emoji769]
 
Mara nyingi tabiri zako umekuwa ukiangukia pua..!!
Tuone mara hii nafikiri utaanguka jicho kabisa..😅
Wenyewe wanakuambia chichiemu ni ileile ooh ni ileile..

Tusubiri tuone maajabu ya huyu mlozi
 
Maajabu yatatokea na dunia itashangaa
Sitegemei maajabu labda ya 100% CCM KUPORA haki za watanzania/matakwa ya watanzania. Mshana, tuliokulia kwenye enzi wa Idd Amin, tunajua hulka ya madikiteita! Ndiyo maana unaona bila aibu mtu anasema Rais, CJ na Speaker wavunje Katiba, sheria wasishitakiwe! Unategemea uchaguzi toka watu hao? Klichopo wacha watunge sheria zao, SIKU YA SIKU UNA-SISPEND KATIBA NA KUWASHITAKI CHINI YA MAHAKAMA MAALUMU!
 
Da Mshana Jr kw hyo unatuambia team pinzani itangusha mbuyu uliyojichimbia miziz iliyojaa nge,Nyoka,miziz ambayo ikitumika kuloga huua kwl,miziz iliyojaa jaa miiba ambayo ikikuchoma huua kabsa na ikameza ndg waskuzke, miziz iliyojaa giliba na fitina isiiomithirika! Yetu Macho juu ya dimba lileeee!!!
 
Mshana Jr, Mimi naipenda Sana CCM.
Mwenyekiti wa CCM ndiye aliyemteua Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi.
Mwenyekiti wa CCM ndiye anayeteua Wagurugenzi wa Halmashauri. Wagurugenzi ndio watangazaji wa matokeo ya uchaguzi.
Mwenyekiti wa CCM alishawahi kutoa onyo hadharani kwa Wagurugenzi wa Halmashauri akiwaonya kwamba gari wamepewa na CCM, mshahara wanalipwa na CCM, nyumba wanalipwa na CCM, Sasa ole wake Mkurugenzi atakaye mtangaza mgombea wa upinzani kuwa mshindi.
Naomba mwenye uwezo wa kuipata hiyo video clip aiweke hapa.
Kwenye mazingira hayo ushindani huru na wa haki unatokea wapi?
Polisi ni Mali ya CCM, TISS, Jeshi, Mahakma na Magereza vyote Mali ya CCM kudidimiza upinzani.
Sioni haja ya kuingia kwenye uchaguzi wa kibabe namna hii.
 
Mara nyingi tabiri zako umekuwa ukiangukia pua..!!
Tuone mara hii nafikiri utaanguka jicho kabisa..[emoji28]
Wenyewe wanakuambia chichiemu ni ileile ooh ni ileile..

Tusubiri tuone maajabu ya huyu mlozi
Tusubiri tuone maajabu ya huyu mlozi

Jr[emoji769]
 
Kama Chadema wanaitaji ushindi katika uchaguzi huu hawana budi kufanyia Kazi eneo la ushirikiano wa Kimataifa. Lazima wajikite katika kutafuta both external na internal support. Hao CCM wanaopambana nao wanaushirikiano mkubwa na vyama vya China na Vietnam pamoja na vyama vya nchi za Afrika. Hakuna budi katika kipindi hiki cha muda mfupi nao cha sema wakatafuta vyama na Serikali za kuziunga mkono nchi za ulaya, Asia na hata nchi zinazotuzunguka

TANU bila support ya nchi nyingine isingefanikiwa kuiletea Tanganyika uhuru.

Kazi kwenu!
 
Da Mshana Jr kw hyo unatuambia team pinzani itangusha mbuyu uliyojichimbia miziz iliyojaa nge,Nyoka,miziz ambayo ikitumika kuloga huua kwl,miziz iliyojaa jaa miiba ambayo ikikuchoma huua kabsa na ikameza ndg waskuzke, miziz iliyojaa giliba na fitina isiiomithirika! Yetu Macho juu ya dimba lileeee!!!
Inawezekana kabisa,hatuwezi kuvumilia uonevu zaidi,tulipotafuta Uhuru siyo wa watu wachache kufaidi matunda yake huku wengine wakiteswa waziwazi kimfumo.
Ukifika wakati wa uchaguzi mnajiamulia hadi asilimia za ushindi kabla ya upigaji kura.
Hebu tuache kuigiza na kuanza kufanya uchaguzi halali,tuheshimu matokeo yake na kujikita katika kuijenga nchi yetu.Nchi yenye umri wa 60 years bado tegemezi?
 
Mbio za sakafuni huishia ukingoni, nyumba iliyojengwa juu ya msingi wa uongo na ulaghai haitodumu milele. Kwaheri Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Mshana Jr, Mimi naipenda Sana CCM.
Mwenyekiti wa CCM ndiye aliyemteua Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi.
Mwenyekiti wa CCM ndiye anayeteua Wagurugenzi wa Halmashauri. Wagurugenzi ndio watangazaji wa matokeo ya uchaguzi.
Mwenyekiti wa CCM alishawahi kutoa onyo hadharani kwa Wagurugenzi wa Halmashauri akiwaonya kwamba gari wamepewa na CCM, mshahara wanalipwa na CCM, nyumba wanalipwa na CCM, Sasa ole wake Mkurugenzi atakaye mtangaza mgombea wa upinzani kuwa mshindi.
Naomba mwenye uwezo wa kuipata hiyo video clip aiweke hapa.
Kwenye mazingira hayo ushindani huru na wa haki unatokea wapi?
Polisi ni Mali ya CCM, TISS, Jeshi, Mahakma na Magereza vyote Mali ya CCM kudidimiza upinzani.
Sioni haja ya kuingia kwenye uchaguzi wa kibabe namna hii.
Uchaguzi upo Ila ni wa kiini macho
 
Kurasa za kitabu zinapofikia tamati hakuna namna hata utumie sungusungu wa mmea janja... Kwahiyo huu si utabiri bali ni kuhusu kufunga kitabu kama kurasa zimeisha

Jr[emoji769]
Umekula lakini..?😂
 
Vipo vingi vya kuliwa... Kipi kimojawapo unamaanisha[emoji848]

Jr[emoji769]
😂😂 Wacha mambo yako
Chakula kama chakula ndo nachomaanisha...
Unazeeka vibaya ndugu😜

Umefanya nikumbuke tukio lile la ugombanizi nashukuru nilikushinda.. usipokumbuka jua ushazeeka..😅
 
[emoji23][emoji23] Wacha mambo yako
Chakula kama chakula ndo nachomaanisha...
Unazeeka vibaya ndugu[emoji12]

Umefanya nikumbuke tukio lile la ugombanizi nashukuru nilikushinda.. usipokumbuka jua ushazeeka..[emoji28]
[emoji23][emoji23][emoji23]hata kwio INALIWA ujue... Usipolifahamu hili basi hujakua... Halafu kuna kitu kinaitwa sefuli nacho wanasema ati ni chakula kitamu sana... Kwahiyo vya kuliwa ni vingi
BTW hilo tukio halipo kwenye memory card yangu labda unikumbushe kama hutojali[emoji848][emoji144][emoji419]

Jr[emoji769]
 
Sitegemei maajabu labda ya 100% CCM KUPORA haki za watanzania/matakwa ya watanzania. Mshana, tuliokulia kwenye enzi wa Idd Amin, tunajua hulka ya madikiteita! Ndiyo maana unaona bila aibu mtu anasema Rais, CJ na Speaker wavunje Katiba, sheria wasishitakiwe! Unategemea uchaguzi toka watu hao? Klichopo wacha watunge sheria zao, SIKU YA SIKU UNA-SISPEND KATIBA NA KUWASHITAKI CHINI YA MAHAKAMA MAALUMU!
Wamesahau cheo cha RC wa Dar katika hiyo safu ya immunity
 
[emoji23][emoji23][emoji23]hata kwio INALIWA ujue... Usipolifahamu hili basi hujakua... Halafu kuna kitu kinaitwa sefuli nacho wanasema ati ni chakula kitamu sana... Kwahiyo vya kuliwa ni vingi
BTW hilo tukio halipo kwenye memory card yangu labda unikumbushe kama hutojali[emoji848][emoji144][emoji419]

Jr[emoji769]
Hata mi nimelisahau..
Ndo nipo naelekea milembe kabla hawajaniijia wahusika..😅

Sikuhizi umekuwa wa misemo hii pia inaashiria umekuwa wa mtaani sasa hongera😎😂😅
 
Tuna chini ya siku 150 kuelekea uchaguzi mkuu...
Huu utakuwa uchaguzi mkuu tofauti kabisa na chaguzi nyingine zote zilizopita
Hakuna amsha amsha hakuna shamra shamra
Hakuna kimbiza kimbiza... Kumetulia sana na kwa sehemu kuna wasiwasi, woga na sononi kwa wananchi... Lakini pia wana tashwishwi ya kutaka kuona maajabu yakitendeka...

Muda uliobaki ni mchache sana lakini ni muhimu sana kwa kila dakika inayo tiktok.. Kuna mambo yanaendelea kimyakimya... Chinichini lakini kwa haraka na wepesi wa ajabu
The race against time...! Kama kutakuwa na huo uchaguzi (achana na neno HURU na HAKI) Tanganyika inaweza kuishangaza dunia.. Kila zama huwa na kurasa zake... Na unapofika wakati wa kufunua ukurasa husika huna budi.. huna jinsi.. Huna namna.. Huna hiari... Inabidi kuufunua...!!!

Kila jambo huwa na kikomo cha kuwa... Kikomo cha zama.. Kikomo cha nyakati... MWANADAMU ni mtumwa wa muda... Achana na maneno HURU na HAKI kuna watu walivikwa ukuu wakiwa hawapo... Kuna watu walikabidhiwa majukumu makubwa wakiwa mbali uhamishoni..

Kuna baadhi ya imani ukitaka kuoa mke si lazima uwepo eneo la tukio... Ndugu yako anaweza kukuolea kwa maneno halafu vitendo ukaja kufanya mwenyewe
Hili ni pambazuko la kipenga cha mwisho.. Kila alfajiri ipitayo haitarudi tena... Nje upepo unavuma lakini unavuma na mengi... Ni alfajiri nyingine tena...

Natambua wazi jana ulilala fofofo baada ya uchovu wa kazi na mihangaiko ya siku nzima... Juma zima... Lakini wapo ambao hawalali... Hawakulala na hawatalala mpaka kipenga cha mwisho kitakapodhihiri mwangwi wake na kupotelea kwenye kadamnasi ya hadhira yenye tashwishwi kubwa ya mabadiliko

Ni alfajiri nyingine tena.. Wanaume hawajalala ni mwendo wa kuandaa mazingira ili timu pinzani isiliguse dimba.. Kisha tutangaziane ushindi mnono wa kishindo!!!!
Kwenye kila andishi kuna TAMATI... Kama tamati ya andiko lako imetimia funika buku lako ulirudishe kabatini kwakuwa hakuna kurasa zaidi... Huhitaji kufanya marudio ya kurasa
Kuna kitabu kipya na wasomaji wapya.. Wape nafasi kwa upendo na bila ghiliba wasome kwa utulivu na amani kurasa zao... Nao kuna siku watafikia TAMATI... Usilazimishe makhaba kama hisia zumeshakufa
Kumbuka ni wafu pekee ndio wasiokula wala kunywa... Chumvi ikiisha ladha haifai tena kwakuwa hakuna cha kuipa ladha tena..
Ni alfajiri ya kipenga cha mwisho... Pambazuko lenye tumaini jipya... Achana na maneno HURU NA HAKI.. Uchaguzi utafanyika.. Maajabu yatatokea na dunia itashangaa

Jr[emoji769]
Wavoka kubigha ramli ja kimbare!
Uho kwa Kimbwereza,Mavura kana Kilenga??
 
Wamesahau cheo cha RC wa Dar katika hiyo safu ya immunity
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji40][emoji40][emoji87][emoji87][emoji87][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom