Uchaguzi 2020 Pambazuko: Lazaro Nyalandu kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA

Uchaguzi 2020 Pambazuko: Lazaro Nyalandu kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Wakati wowote kuanzia sasa aliyekuwa mbunge kwa tiketi ya CCM na baadae kujiuzulu na kuhamia Chadema Mh. Lazaro Nyalandu atachukua fomu za kugombea urais.

Taarifa za chini ya kapeti zinasema Nyalandu ana baraka zote za uongozi wa juu wa chama chake na atakachosubiri ni kukubaliwa tu chama mshirika endapo Chadema na ACT Wazalendo watakubaliana kusimamisha mgombea mmoja wa urais.

Tarehe 15/06/2020 ndio siku ya mwisho kwa watia nia kuchukua na kurejesha fomu kwa nafasi ya Rais.

Mungu ibariki Tanzania

Maendeleo hayana vyama!
 
Ina maana anamgeuka rafiki yake wa karibu yule yule wa kwao anaeishi nje kimatibabu (kama inavumyosemekana)
 
Mtoa mada unapotosha, sio kweli kwamba tarehe za kuchukua fomu kwa chadema za wagombea urais Ni kati ya tarehe 3 na 15. Bali Ni kutia nia. Hats nyarandu akitia nia sawa tu.Demokrasia itaamua
Hivyo hivyo bwashee kwani hiyo nia unatiaje?

Tuache demokrasia ichukue mkondo wake.

Maendeleo hayana vyama!
 
nyalandu atupishe kidogo , tunamtaka kiboko ya jiwe, Antipas Mungwai Lissu
Lissu atagombea akiwa nje ya nchi? arudi kwanza home kabla ya hiyo tarehe 15 June 2020 kwa uhakika wa yeye kugombea. Hata hivyo binafsi namwona kama bado hajakua; huenda akawa msemaji zaidi kuliko kusikiliza
 
Kimalengo ya baadae wamuache Nyalandu agombee kwa sasa,kwa sababu.
Wanatakiwa wamuandae mgombea mwingine ambae atakuja kupambana kwa nguvu nyingi katika uchaguzi wa mwaka 2025,ila kwa sasa bado nguvu itakua ndogo sana
Miaka hii mitano watatkiwa kupika vijana sana katika masuala ya kisiasa ikiwezekana kuwapa elimu kubwa ya namna gani uongozi ulivyo pamoja na kuwafunza vijana katika masuala ya kiteknolojia.
Miaka hii mitano watatikiwa kutazama ni wapi wamekosea na wapi waanzie na wapi waje kumalizia.
 
Lissu atagombea akiwa nje ya nchi? arudi kwanza home kabla ya hiyo tarehe 15 June 2020 kwa uhakika wa yeye kugombea. Hata hivyo binafsi namwona kama bado hajakua; huenda akawa msemaji zaidi kuliko kusikiliza
Mkuu ndo uzuri Wa demokrasia wacha achukue fomu, wenzake wataamua.sio maccm wanalazimisha mgombea mmoja tu hats kama wanaccm wengine wanatamani kuomba nafasi hyo.
 
Back
Top Bottom