Pamepoa sana

Pamepoa sana

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
PAMEPOA SANA.......
1739797452111.jpg

Hebu tujadili kidogo kwa kutumia mada ninayoileta Kwenu kwa Mfumo wa Swali.

Je umewahi kukutana na Mnyama yeyote hatari iwe wa kufugwa au wa Mbugani?
Kama jibu ni NDIO,uliwezaje kujinusuru?

Kumbuka kutaja Jina la kiumbe husika iwe mkubwa au mdogo na mbinu uliyoitumia ili imfae na mwingine anayeweza kukutana na tukio kama hilo huko Mbeleni.
.........................

Kwa upande wangu niliwahi kuingia kwenye Boma moja nikakuta Mbwa kama 6 hivi wakali sana.Mbwa wale baada ya kuniona wakaja kwa kushtukiza na kunizingira.

Wakati huo wenyeji wako ndani na Nyumba iko mbali kidogo ingawa ni ndani ya Uzio.Basi baada ya kuona nimejaa kwenye Mfumo nikafunga mikono yangu Kifuani halafu nikasimama Mguu sawa bila kujitikisa hata kidogo.Nikainua uso juu na kufumba Macho.

Wale Mbwa wakanizunguka mara kadhaa kisha mmoja wao akanigusa mguu kwa nyuma kwa kutumia pua yake lakini sikujigusa.

Walipoona utulivu ule Wakaniacha,Wakasogea Mbali na muda huo wenyeji wakawa wamefika eneo lile.

Kwa aina ya tukio lilivyokuwa niliokoka siku ile.

Wewe ulichomokaje na ugomvi wako ulihusisha kiumbe gani?

Karibuni sana kwa kuchangia!
 
Mbwa,niliganda,aling'ata makalio kunishtua nikakomaa kwa kuyabana sana...alivyoona sishtuki akaanza kuondoka....mbwa ukionyesha woga au kukimbia ndiyo hujaa kichwa🙄

Nyoka,nipo busy kula msosi kwa sebule,huyo anaingia kwa madaha...kabla hajaniwahi nikamuwahi kwa kumwacha aendelee kuingia chumbani afu mie nikaanza kumnyatia kwa nyuma...ni chap...nikabana shingo...vingirisha mkono ..mi nikakomaa kukaba....tutumka ....mi nimo...nikamrushia nje....kushuka chini ashalewa... Mie bila kumchelewesha nikampa fimbo ya kichwa...kimya! 😏
Chai ya baridi
 
Hii fix sasa
 
Ila utoto laha sana.
Kuleni maisha vijana.
 
Hayo mambo ya mbwa achana nayo mzee!!!

Kuna sehemu nilienda kikazi pembezoni huko mwa dar, hii njia ya kwenda kibaha kupitia pale baobab bunju, kuna mtoto mmoja wa kishua alipata kipaimara huko simu zikaita nikaingia kazini.

Kazi yangu ilikua kulisafirisha na kulisimamia lile puto linalojazwa upepo halafu watoto wanacheza. cheza.

View: https://youtu.be/Om6HbM-8Xrw?si=V6kcwJ39zELRBo6c

Baada ya kuufinya pale, niko pembeni na Coca-Cola yangu nawaangalia watoto wanacheza, mara mc anasema, jamani junior haonekani. mama yake anamtafuta, junior ana umri wa miaka , rangi yake maji ya kunde.

Ikabidi sisi sote tukajipa majukumu ya kugawana maeneo kwenda kumtafuta wengine kusini kaskazini,mashariki kwa magharibi

Nyumba za kule ni za mbali mbali halafu vi misitu misitu, tukajikuta tumegawana, mie nikaenda kwenye nyumba flani haina uzio ipo kimyaaa.

Ile naanza tu hodi hodi, ikachomoka mijibwa 6 ghafra nikawekwa mtu kati, mijibwa inabweka ile mbaya, sasa kama zari kuna video niliangaliaga YouTube inaelezea nini ufanye mbwa akikushambulia.

View: https://youtu.be/vX-OOfbnD9w?si=CtnEYrF3W3Je5w1x

Asee nilitoka salama salmini bila kuguswa hata ukucha na yale mabwa, nikageuza kurudi eneo langu la kazi kimya kimya, nafika namkuta baba junior keshamtia ma junior mikofi kama miwili hivi kwa uzembe.

Ila dogo alipatikana.
 
Back
Top Bottom