Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
PAMEPOA SANA.......
Hebu tujadili kidogo kwa kutumia mada ninayoileta Kwenu kwa Mfumo wa Swali.
Je umewahi kukutana na Mnyama yeyote hatari iwe wa kufugwa au wa Mbugani?
Kama jibu ni NDIO,uliwezaje kujinusuru?
Kumbuka kutaja Jina la kiumbe husika iwe mkubwa au mdogo na mbinu uliyoitumia ili imfae na mwingine anayeweza kukutana na tukio kama hilo huko Mbeleni.
.........................
Kwa upande wangu niliwahi kuingia kwenye Boma moja nikakuta Mbwa kama 6 hivi wakali sana.Mbwa wale baada ya kuniona wakaja kwa kushtukiza na kunizingira.
Wakati huo wenyeji wako ndani na Nyumba iko mbali kidogo ingawa ni ndani ya Uzio.Basi baada ya kuona nimejaa kwenye Mfumo nikafunga mikono yangu Kifuani halafu nikasimama Mguu sawa bila kujitikisa hata kidogo.Nikainua uso juu na kufumba Macho.
Wale Mbwa wakanizunguka mara kadhaa kisha mmoja wao akanigusa mguu kwa nyuma kwa kutumia pua yake lakini sikujigusa.
Walipoona utulivu ule Wakaniacha,Wakasogea Mbali na muda huo wenyeji wakawa wamefika eneo lile.
Kwa aina ya tukio lilivyokuwa niliokoka siku ile.
Wewe ulichomokaje na ugomvi wako ulihusisha kiumbe gani?
Karibuni sana kwa kuchangia!