Pamoja na bei ya mafuta kupanda, watu wanaendelea kutumia magari na vyombo vingine vinavyotumia mafuta. Je ni kweli wako vizuri kipesa?

Pamoja na bei ya mafuta kupanda, watu wanaendelea kutumia magari na vyombo vingine vinavyotumia mafuta. Je ni kweli wako vizuri kipesa?

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Kwa maelezo ya waziri mkuu mstaafu mhe. Msuya akiwa kwenye kipindi cha dk 45 cha ITV, ni kama amemaanisha kwamba uwepo wa magari mengi mjini au barabarani ni kutokana na hali za maisha kutofanana.

Ni kama vile wanaotumia vyombo hivyo hawaoni tofauti ya kupanda kwa bei. Na kwamba wana hali nzuri kifedha.
Je, ni kweli? Au wanapambana tu na hali kwa kuwa hakuna namna nyingine?
 
Ambao bado wanaendesha magari ni wanawake na usiulize pesa wanatoa wapi. Ukiona mwanaume anaendesha gari lake binafsi ujue ni mambo safi au menu ya nyumbani ni chai ya rangi viazi vitamin kwa dona na sukumawiki.
 
Kwa maelezo ya waziri mkuu mstaafu mhe. Msuya akiwa kwenye kipindi cha dk 45 cha itv, ni kama amemaanisha kwamba uwepo wa magari mengi mjini au barabarani ni kutokana na hali za maisha kutofanana. Ni kama vile wanaotumia vyombo hivyo hawaoni tofauti ya kupanda kwa bei. Na kwamba wana hali nzuri kifedha.
Je, ni kweli? Au wanapambana tu na hali kwa kuwa hakuna namna nyingine?
Tuwaulize nyie mnaolalamika hovyo mitandaoni..

Hata hivyo Takwimu za Uchumi kwa robo ya kwanza ya mwaka 2022 zinaonyesha kupungua kwa ukuaji kwa sekta ya uchukuzi kutoka 8.5% hadi 3% bila shaka sababu kubwa ni gharama za usafiri kuwa juu.
 
Tuwaulize nyie mbaolalamika hovyo mitandaoni..

Hata hivyo Takwimu za Uchumi kwa robo ya kwanza ya mwaka 2022 zinaonyesha kupungua kwa ukuaji kwa sekta ya uchukuzi kutoka 8.5% hadi 3% bila shaka sababu kubwa ni gharama za usafiri kuwa juu.
Tunalalamika kwasababu, utake au usitake ili kuweza kufika eneo la kujipatia riziki (ofisini) ni lazima utumie usafiri. Kwahiyo kupanda kwa bei ya mafuta kumeathiri uchumi. Kama ulikuwa unatumia kwa mfano elfu 2000 kwa siku kwa ajili ya nauli utatumia 4000!

Na pia bidhaa zote zimepanda bei kwa kisingizio cha vita. Hadi zile zinazotoka shambani moja kwa moja mfano mbogamboga, matunda nk.

Inabidi wamshauri mkuu wa nchi akemee kupanda kwa bei ya bidhaa kiholela kwa kisingizio cha vita vya urusi na Ukraine.

Yaani vita vinapiganwa Ukraine, Mabomu yanarushwa Tz! Duh!
 
Tunalalamika kwasababu, utake au usitake ili kuweza kufika eneo la kujipatia riziki (ofisini) ni lazima utumie usafiri. Kwahiyo kupanda kwa bei ya mafuta kumeathiri uchumi. Kama ulikuwa unatumia kwa mfano elfu 2000 kwa siku kwa ajili ya nauli utatumia 4000!

Na pia bidhaa zote zimepanda bei kwa kisingizio cha vita. Hadi zile zinazotoka shambani moja kwa moja mfano mbogamboga, matunda nk.

Inabidi wamshauri mkuu wa nchi akemee kupanda kwa bei ya bidhaa kiholela kwa kisingizio cha vita vya urusi na ukraine.
Yaani vita vinapiganwa ukraine, Mabomu yanarushwa Tz! Duh!
Serikali ijitahidi kuwa na ceiling kwamba Bei isizidi kiasi fulani then hata upande zaidi kwingine wao waongeze ruzuku.
 
Tafuta hela dogo acha kushinda mitandaoni. Nenda kakate miwa Kilombelo ama katani kule Tanga.

Kwahiyo ulitaka watu wote wapaki magari yao ndiyo ujue mafuta yamepanda bei? By the way.mafuta yamepanda bei za vitu pia vimepanda. Ngoma droo.

Kama una cha kuuza pandisha bei. Na kama huna pandisha hata bei ya penzi lako.
 
Kwa nionavyo, wengi wanapambana tu na hali.
Hili ndio jibu sahihi.kwasababu maisha lazima yaendelee.Unajibana uku ili ufanye uku.Kwa vyovyote vile tathmini ya mwisho ndio itakayotoa majibu na kwa hakika lazima kuna sekta zitakua zimeanguka au hazitafanya vizuri au kufikia malengo kwasababu ya hali ya kiuchumi,mfumuko wa bei na mafuta kwa ujumla.Kwakuanzia tu hali ya bei ya mafuta lazima itaathiri uchumi wa mtu mmoja mmoja kwa kiwango kikubwa.Hizo zingine ni porojo za wanasiasa wanaolamba asali ambazo zipo miaka na miaka.
 
Kuna wakati ukiona maisha magumu usifikiri na wenzio wanalia kilio hichohicho unaweza kujikuta uko peke yako na unapolalamika wenzio wanajifanya mnalalamika wote kumbe wanakuchora.

Kuna wakati tujikite kutafuta mbinu za kutukwamua na kuendana na kasi ya ulimwengu, vinginevyo hii dunia itakutesa peke yako.

Wakati unalalamika maisha magumu kuna wenzio kule Mbweni, Goba, Madale nk wanashusha maghorofa na kuweka mpaka swimming pools.
 
Kwa maelezo ya waziri mkuu mstaafu mhe. Msuya akiwa kwenye kipindi cha dk 45 cha itv, ni kama amemaanisha kwamba uwepo wa magari mengi mjini au barabarani ni kutokana na hali za maisha kutofanana. Ni kama vile wanaotumia vyombo hivyo hawaoni tofauti ya kupanda kwa bei. Na kwamba wana hali nzuri kifedha.
Je, ni kweli? Au wanapambana tu na hali kwa kuwa hakuna namna nyingine?
Hii ni kweli, na yakipotea utaona impact yake watu wataandamana. Pesa ipo japo kwa mbaali sana
 
Walati unalalamika maisha magumu na mafuta yamepanda bei, kuna wenzio kwenye parking wana magari zaidi ya mawili na yote ni kuanzia 2500cc na kuendelea.

Huko kwenye mafoleni unakuta wenzio wanatumia gari za 3000C full tinted anakula na kiyoyozi, naye mkikutana anakuunga mkono maisha magumu kweli aisee. Waarabu na wahindi wanasukuma tu Nissans V8 new model, Lexus V8, idadi ya landrover vela zinazidi kuongezeka mjini tu.

Hizi nyimbo za maisha magumu ukiziimba sana yanaweza kuwa magumu sana kwako badala yake ni kuumiza kichwa tu "what the way forward"?
 
Siku hizi Vitz na Passo zimegeuzwa daladala na wamiliki wake, ukiwa unaenda kazini asubuhi usipate tabu, simama kituoni atakuja mtu na Vitz yake akupange unaenda wapi then anakwambia gari ipo utachangia mafuta buku.

Akiwakusanya watano safari inaanza, nimeshuhudia huu mchezo ukiendelea kwa kasi Bagamoyo Road, hao wamiliki wa hayo magari wameamua kujilipua, hivyo usishangae pamoja na bei ya mafuta kupanda, bado gari zipo nyingi barabarani, tuna share cost.
 
Kwa maelezo ya waziri mkuu mstaafu mhe. Msuya akiwa kwenye kipindi cha dk 45 cha itv, ni kama amemaanisha kwamba uwepo wa magari mengi mjini au barabarani ni kutokana na hali za maisha kutofanana.

Ni kama vile wanaotumia vyombo hivyo hawaoni tofauti ya kupanda kwa bei. Na kwamba wana hali nzuri kifedha.
Je, ni kweli? Au wanapambana tu na hali kwa kuwa hakuna namna nyingine?
Mbona magari yamepungua sana tu majuzi nilikuwa kkoo mitaa ni empty ukitaka kuvuka barabara ni rahisi...magari mengi yanaonekana jioni na asihuhi ...sasa hivi watu wana punguza matumizi polepole ili kuzoea njia mpya za usafili hadi miezi 2 kutoka sasa utaona magari yatauzwa sana tena yatashuka bei sana ....kwa sasa watu wanasikilizia kama mafuta yatashuka ....kwa sasa kumiliki gari ni sawa na kuuguza mgonjwa wa figo.
 
Ambao bado wanaendesha magari ni wanawake na usiulize pesa wanatoa wapi. Ukiona mwanaume anaendesha gari lake binafsi ujue ni mambo safi au menu ya nyumbani ni chai ya rangi viazi vitamin kwa dona na sukumawiki.
Unataka sema masikini ni wengi sana Tz
 
nimefanya research kuanzia April mpaka hii August kwenye mikoa kadhaa kuanzia Ijumaa to Sunday sehemu za starehe zinafurika watu na parking zinakuwa full magari watu wanatumia hela za kutosha. Lakini chakushangaza watu hao hao utawasikia maisha magumu sana aisee.
 
Tatizo ni watumishi mishahara haipandi ila wajasiriamali wanahamishia kilichopanda kwenye huduma zao. Kama nondo aliuza tsh 100 anauza tsh 200.
 
Kuna watu naamini kbsa hawana uchumi mkubwa ila Yuko taayar kueeks gar lake full tank laki tatu ili tu asipate adha ya usafi hata yakifika elf tano usitegemm gar kuoungua njiani Zaid.sans watu wananagiza magar mapya
 
Back
Top Bottom